Uzinduzi rasmi wa JF Aprili 2010

Uzinduzi rasmi wa JF Aprili 2010

Status
Not open for further replies.
kazi nzuri sana!
invizibo nitafute kwa tots kadhaa za whiscky
 
mnakutana kwa majina yenu halisi siyo majina ya JF.. which will be fun kwa sababu huwezi kumsema mtu vibaya hapo (labda sisi wengine ambao tunajulikana tulipo) maana unaweza ukawa ndiye uliyemchunuku.

ni wazo zuri but with all due respect mzee ... its kinda risky ... puppets tunao wengi sana humu ndani as JF members ... wengine wako kwenye payroll specifically kwa kazi hiyo so i beg to differ ...!
 
Kazi nzuri sana Mheshimiwa Invisible.

Najua si kazi ndogo kufanikisha yote haya
, tulio wengi tunaipenda sana JF na huwa tunachanganyikiwa kuikosa kwa mimi Binafsi nimejifunza mengi sana hata ambayo sikudhani kama ningeyafahamu.

Cha msingi tuichangie JF ili iendelee zaidi na zaidi..kwani kuna gharama zinazotumika hapo

Zinatoka wapi? Mie na wewe hatujui

All the best JF
 
ni wazo zuri but with all due respect mzee ... its kinda risky ... puppets tunao wengi sana humu ndani as JF members ... wengine wako kwenye payroll specifically kwa kazi hiyo so i beg to differ ...!

Langu litabakia kuwa hili la nyuma ya pazia
Heshima kwako Mkuu
 
All the best JF Team, kuna watu walikimbia naamini watarudi wenyewe
 
Thanks Mkuu Invisible;

Tunatarajia uzinduzi rasmi hautakuwa April mosi (wengine watafikiri utani)
 
Tatizo la Watanzania ni kupenda sana misifa na kupenda kupeana misifa hata isiyo na maana.

Hii JF inachemsha kila mara na tayari wanaongelea mambo makubwa wakati madogo bado yanawashinda.

Kitu cha kwanza lazima mtuhakikishie kwamba JF itakuwa online kwa asilimia 99.9999 kitu ambacho sasa sivyo. Angalieni mwenzenu Michuzi sijawahi kuona blog yake iko offline.

Baada ya hapo ndio imaarisheni mambo mengine hata kwa kushirikiana na watu wengine. Kwa mfano mnaweza kuungana na mzee Mwanakijiji ili kutengeneza online radio ya maana na kisha kuingia kwenye magazeti.

Lakini sisi hapa kazi ni kusifia tu hata wanapolikoroga.

Msiniue wakuu, nawatakia mema tena kwa vitendo lakini nakerwa na hizi sifa zisizo na maana yoyote. Ukitaka uharibikiwe basi kumbatia misifa isiyo na mpango.
 
Forum kama hii ilipaswa kuwa na mod si chini ya watano (5)...
Mkuu X-Paster, kupata moderator ni kazi ngumu, tushawahi kupokea maombi toka kwa members kadhaa wakitaka kuwa moderators, wengi tuliwachunguza kwanza na baadae kugundua ndio waporomosha matusi maarufu... Haikusaidia, kuna wawili wanaonekana wanafaa wakiwa trained vema, tunalifanyia kazi.

Moderators/Administrators wa JF ni hawa:

  1. Ab-Titchaz
  2. Brutus
  3. Silencer
  4. PainKiller
  5. Mtumishi
  6. Invisible
  7. Spiderman
  8. Farida
Mkuu invisible hii kiboko sijawahi kuona Forum yoyote ya Kiswahili tangu niingie kwenye Mtandao wa internet inayopata Hits 45 Millioni itabidi muwe na Moderator wa kutosha Mkuu invisible poleni sana kwa kazi nzito
Mkuu MziziMkavu; growth ya JF ni 25.62% per month, na kwa sasa members wengi wanaoitembelea JF wanatokea Tanzania, hivyo hatuwezi kuepuka kufanya mabadiliko muhimu ili wanachama hawa wafikishe ujumbe kwa jamii ya watanzania ambayo haina access na mtandao wa intaneti.

Thanks Invisible... nadhani tungeongeza benefits za premium members, na kuweka ukomo wa mtu kuwa premium member; kila membership ina ukomo unaoweza kuwa renewed kwa terms fulani
Mkuu; tuna members zaidi ya 15,000/= na Premium Members ni 188 tu, nadhani hawa bado wanastahili pongezi kwa uamuzi wao wa walau kuchangia chochote walicho nacho kwa ajili ya ufanisi wa JF, tunaweza kufikiria kufanya unavyopendekeza siku za usoni lakini nadhani kwa sasa bado tuendelee kuwapa heshima kwa moyo wao wa kujitolea.
 
Woooooo Waoh!!! Keep it up JF Administration!!! Yaani baada ya kuizindua nafikiri nitajisikia even more official kujidai mimi "Mwana JF" wa awamu ya Pili, awamu ya kwanza nafikiri ni wale wa Jambo F. I believe kama tutakuwa na JF TV and Radio, basi ni burudusho tosha!!! Ila sasa, je tutaendelea kuwa " a place where we dare talk openly" kwa njia ya TV na Radio? Hii ni hatua kubwa sana ya jukwaa hili.

Again, thanks Invisible and the entire crew, especially the THREE who are working tireless to re-shape the JF and finally its official launch!!!
 
NYIE MKIFA, SISI TUMEOZA!!
I just want to show what you mean to us!...Congrats sana kwa mabadiliko, na tunayapokea kwa mikono na miguu!
 
Wakuu JF big up sana. Naomba kama inawezekana kwa kuwa Zain wanaonekana big up basi angalau muingie nao mkataba ili kuwe na namba ya kuchangia. Kwa mfano tuma neno Jamii kwenda namba xxxyyy gharama ni shs 300/= kwa msg, mimi binafsi na jamaa zangu wengi tu humu jamvini tutatuma msg kila siku kwa wingi tu. Hii ni njia rahisi kuchangia JF kwa mtazamo wangu.

Sijui mnasemaje wakuu. Si lazima Zain hata mitandao mingine ikiwezekana, ila nimeona kuwa Zain wamekuwa wa kwanza kutangaza JF kwa hiyo nimewakubali sana, nawapa big up saaaana.
 
Mkuu invisible, asante sana kwa taarifa....you are one in a million. Nimejisikia vizuri, nimejisikia kuthaminiwa na leo haswa ndio nimejisikia kwa hakika niko kwenye nyumba ya ma-great thinkers. Watu wanaothamini members na kuwapa up-date ya nini kinaendelea, matarajio na malengo ya siku za usoni.

Honestly, njia mnayotaka kuiendea sio njia rahisi, haina lami, makorongo ni mengi, haina madaraja na nimaporini kuna wanyama wakali, lakini inawezekana kabisa kufika salama.Mtafika salama pale mtakapo mtanguliza "Jehova El-Shadai" kwa maana kwake hakuna msamiati wa "kushindwa". Nawaombea kwa Mungu mfanikiwe malengo yote mliyojiwekea, muenee na msambae na kusiwe na mtu duniani ambaye ukimtajia JF asijue ni kitu gani.
Bring it on bro.........i cant wait😀🙂.
 
Mkuu Invisible,

Pongezi nyingi toka huku mstari wa mbele vitani...
I wish kama vile wa-tz wote tufikie hatua tunatembelea humu. Kuna mambo mengi ya maana.

Ni moja ya sehemu mimi kama m-tz naweza elewa haki zangu kikatiba.
Kaza buti tusonge.

Hongera wakuu.
 
Hivi kuna sehemu yoyote ndani ya forum hii ambako kumeandikwa mission statement?? Je JF ni jamvi la mijadala tu... chombo cha kufikisha habari na kuwaamsha watanzania ? chombo cha harakati za ukombozi? au ni chombo chenye malengo ya kukua kibiashara? nafkili hayo yanaweza kutolewa ufafanuzi na waendeshaji ili tukianza tujue tuko hapa kwa malengo gani??

Mbali na yote haya na vyovyote malengo yenu yalivyo bado nafurahia na nafaidika kuwa mmoja wa wanaJF..!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom