Uzinduzi wa Blog ya Le Mutuz WADODA!

Uzinduzi wa Blog ya Le Mutuz WADODA!

Status
Not open for further replies.

Tusker Bariiiidi

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2007
Posts
5,551
Reaction score
2,153
Ule uzinduzi wa Blog ya Wananchi ya Mmiliki Le Mutuz,Le Baharia William Malecela uliofanyika siku ya Jumamosi tar.04.01.14 ULIDODA! Le mutuz ambaye mpaka leo ana "KULA KULALA" kwa Wazazi wake Mtaa wa Ufukoni Seaview ulihudhuriwa na watu wachache sana ambao hawazidi 25 huku wengi wa waalikwa kuomba udhuru kwa wingi kwa kutoona la maana zaidi la kuifanya Blog hiyo kuzinduliwa rasmi! Pole sana Kula Kulala Le Mutuz kwa kupoteza muda!
 
Ule uzinduzi wa Blog ya Wananchi ya Mmiliki Le Mutuz,Le Baharia William Malecela uliofanyika siku ya Jumamosi tar.04.01.14 ULIDODA! Le mutuz ambaye mpaka leo ana "KULA KULALA" kwa Wazazi wake Mtaa wa Ufukoni Seaview ulihudhuriwa na watu wachache sana ambao hawazidi 25 huku wengi wa waalikwa kuomba udhuru kwa wingi kwa kutoona la maana zaidi la kuifanya Blog hiyo kuzinduliwa rasmi! Pole sana Kula Kulala Le Mutuz kwa kupoteza muda!

Kulikuwepo mabebs wa ukweli kibao acha wivu
 
Lumumba fc hawakuwepo? Au bado wanakula vya zitto?
 
Kunasiku niliona adai eti amepata cheque ya pound 2000 kutoka google kama malipo ya adsense kwa mwezi mmoja. Wakati blog yenyewe haina hata adsense za kutosha. Hivi kweli blog yake inaweza kuingiza pound 2000 kwa mwezi?
 
Kunasiku niliona adai eti amepata cheque ya pound 2000 kutoka google kama malipo ya adsense kwa mwezi mmoja. Wakati blog yenyewe haina hata adsense za kutosha. Hivi kweli blog yake inaweza kuingiza pound 2000 kwa mwezi?

Mbona alipata
 
Ilifana saana kwakweli
Wala haikudoda
Mabebs wakareeeeeeeez kama kawa tulifunika

Big Up Le Mutuuuuuuuz
 
huu sasa unaitwa umbea na chuki + roho mbaya nini dhumuni la habari hii
 
Yaan sijaelewaa bado anaishi kwao na ule mwili wote kwa hiyo yule mwanamke akiolewa anaenda kuishi ukweniiiii
 
Ule uzinduzi wa Blog ya Wananchi ya Mmiliki Le Mutuz,Le Baharia William Malecela uliofanyika siku ya Jumamosi tar.04.01.14 ULIDODA! Le mutuz ambaye mpaka leo ana "KULA KULALA" kwa Wazazi wake Mtaa wa Ufukoni Seaview ulihudhuriwa na watu wachache sana ambao hawazidi 25 huku wengi wa waalikwa kuomba udhuru kwa wingi kwa kutoona la maana zaidi la kuifanya Blog hiyo kuzinduliwa rasmi! Pole sana Kula Kulala Le Mutuz kwa kupoteza muda!

- Heshima yako sana kaka, nakushuru sana kwa ujumbe huu maana unajua I live for this yaani kuwajibu haters kama wewe ambaye una historia ya muda mrefu sana ya uadui against me, ingawa sikujui na wala sijakukosea anything zaidi tu ya kutofautiana itikadi wewe unapenda itikadi za Chadema mimi ni CCM, nakumbuka toka nikiwa Marekani umeanzisha thread nyingi sana JF za kunichafua lakini umekuwa ukigonga mwamba sana kwa sababu ya uongo huwa hauwezi kusimama kwa ukweli, mimi nina tabia za ukweli na ndio maana natumia jina langu halisi wakati wewe unatumia jina la bandia hiyo peke yake inaonyesha tofauti ya mimi na wewe, anyways sasa naomba nikujibu kwa faida yako na wengine wote wenye mawazo kama yako ifuatavyo:-

1. Blogu ya Wananchi niliifungua Tarehe 29/5/2012 kwa ajili ya majaribio ya kisayansi kujua ni how inaweza kuwa a powerful tool ya information na biashara kwa wakati mmoja, nimeijaribu kwam mwaka mmoja na nusu sasa, nilianza na visitors 200, leo mwaka mmoja na nusu later inapitiwa na visitors 50,000 kwa siku ukichanganya na Facebook wall yangu ambayo ipo automatically connected na blog unapata visitors 55,000 kwa sababu nina max out ya friends Elfu Tano wanaoruhusiwa na Facebook so ni guarantee post ndani ya Blog kupitiwa na all my Facebook friends na pia kuna wengine 5,000 from my Page ya Facebook kwa hiyo ni guarantee any post ndani ya blog kupitiwa na visitors 60,000 kila siku, nilianza na Tangazo moja la biashara yaani Delina, leo nina matangazo ya bisahara 19 na bado yapo 10 pending tunakamilisha mkataba wa kuanza kuwatangaza.

2. Kwa hiyo nikaamua kwamba Tarehe 4/1/2014 ni siku muafaka kuifingua rasmi officially nikilenga biashara zaidi, kwa kuyaalika makampuni makubwa 20 hapa mjini kama my target ya kuapata matangazo yao baada ya ufunguzi, makampuni 18 yalikuja kati ya hayo 20, na since then I mean ile siku ya sherehe nimeweza kupata matangazo mapya 5, na mengine 10 bado tunamalizia mazungumzo ya mkataba.

3. Sherehe ila kijumla wake nilialika watu 150, lakini 120 walikuja na 30 hawakuja ukumbi wa sherehe unachukua watu 150 kwa hiyo kukosekana kwa watu 30 kulisaidia sana, walikuwepo Wabunge 3 na wajumbe 3 wa NEC CCM Taifa, Wasanii 10 na watu maarufu katika jamii hii 10, na Media outlet 10 na wawakilishi wa makampuni 18 na wananchi wa kawaida, na hata ukienda kwenye blog utaona maelezo tuliyoyatoa kesho yake baada ya sherehe yapo wazi sana ya kilichotokea ule usiku na ambacho hakikutokea tofauti kabisa na uongo wako mtumzima tena mwanaume mzee ungekuwa mtoto ningeelewa, lakini wka mtu mzima kama wewe kuandika uongo wa kitoto kama huu nachukulia ni wivu na chuki binafsi ambazo siku zote nazipenda sana maana zinanisaidia sana kusonga mbele huku nikiwaacha watu kama wewe wakilia lia huku kwenye mitandao.

3. Again naomba niliweke wazi sana hili la ninapoishi, ni kweli ninaishi nyumba ya baba yangu kwa sababu baba yangu anaishi Dodoma haishi kwenye hiyo nyumba, binafsi nina nyumba yangu na shamba kubwa sana ambayo niliijenga toka Mwaka 1995 nikiwa Marekani, baada ya kuishi Marekani na Belgium kwa miaka 30 nilirudi miaka 2 iliyopita moja kwa moja nilipofika ninakuta nyumba ya baba yangu mzazi pale Seaview haina mtu anayeishi hapo na shuguli zangu zote za kibiashara zipo hapa mjini, so nikaamua kuishi kwenye ile nyumba ya baba yangu. Since then nimesikia maneno mengi sana ambayo ni dalili za wakosaji, infact inanifurahisha sana ninaposikia haya maneno kwa sababu ni bora haya maneno kuliko yale ya kawaida kwamba ni mtoto wa fisadi, baba yake mwizi, au mimi mwenyewe mwizi haya sijawahi kuyasikia kwa sababu mimi sio mwizi, sijawahi kunywa pombe toka nizaliwe wala kuvuta sigara, sijawahi kuiba mke wa mtu wala mwanamke wa mtu, sijawahi kumuibia mtu hela zake wala za umma, ninasikia raha sana ninarushiwa maneno ya kitoto kama ya kuishi kwa baba yangu, maana ipi bora kuishi kwa baba yangu kuishi jela, au nyumba ya kifisadi? ha! ha! ha!

- Miashani mwangu sijawahi kusikia mtu anashitakiwa mahakamani kwa kuishi kwenye nyumba ya baba yake mzazi, kwa hiyo naomba kukukumbusha wewe na wenzako kwamba nipo sawa sana na maisha yangu, kuhusu blog ni majuzi tu niemajiri vijana wawili wa kunisaidia kuendesha blog, huku nikiwa ninajitayarisha kufungua Radio na TV station kwa kushirikiana na muwekezaji Tajiri mmoja mkubwa sana hapa mjini, pia ninafanya biashara zangu nyingi sana hapa mjini zote zikiwa ni za halali ndio huwa sina tatizo hata kuzisema wazi, pole sana mkuu wangu ile blog ni kubwa sana kuliko haya maneno yako ya kitoto sana, ile blog sasa inaajiri vijana wawili vipi wewe na haya maneno yako umeajiri vijana wangapi kaka?

- Watu kama wewe ndio nimewasema sana kwamba mmeshindwa kuitumia mitandao kwa faida yenu mmeamua kuchafua wale wanaowazidi kwa akili na maendeleo, maana kaka blog yangu ina mwaka mmoja tu na nusu lakini sasa hivi ninashindana na blog moja tu ya Michuzi ambayo ipo kwa miaka mingi sana, hayo ni mafanikio makubwa sana kaka kulinganisha na haya maneno yako ya mkosaji, tumia mitandao kuelimisha wananchi tumia mitandao kutengeneza pesa kaka, wakati wewe unatumia mitandao kuchafua watu usiowaweza kama mimi ambao tunatumia mitandao kuelemisha na kutengeneza pesa kaka,

- Ni matumaini yangu kwamba nimekusaidia wewe na wengine kama wewe mnaotumia mitandao kuchafua watu wanaoleta maendeleo kwa kuwaelimisha wananchi, kaka blo yangu imeajiri Vijana wawili na by mwezi wa Sita ninategemea kuajiri wengine 6 pole sana sasa waambie hawa niliowaajiri hayo maneno yako ya umbeya na uzushi wa kijinga, pole sana kaka na ninaamini nimekusaidia sana kuelewa maana inaonekana una matatizo makubwa sana kama sio ya akili na kama bado una maswali naomba sana uliza tena kwa kutumia njia hii unayoijua sana kaka!!

- WASALAAM!

Le Mutuz
 
Kunasiku niliona adai eti amepata cheque ya pound 2000 kutoka google kama malipo ya adsense kwa mwezi mmoja. Wakati blog yenyewe haina hata adsense za kutosha. Hivi kweli blog yake inaweza kuingiza pound 2000 kwa mwezi?

- Ok kaka ahsante sana naomba kukusaidia habari hii ya google maana umesema sana kwa matusi toka nilipoiweka to the public, ufafanuzi kuhusu check ya google ni kama ifuatavyo:-

Google walinipa offer ya kutangaza matangazo yao kwenye blog yangu kwanza kwa majaribio, nikawakubalia wakaweka matangazo yao matatu, kwa mwezi mzima ulipoisha mwezi wakanionyesha namba zao na pesa iliyoingia ingawa pia walinipa access ya kuona pesa zinavyoingia kila siku kutokana na namba ya watu walipitia matangazo yao katika blog, ilikuwa karibu Euro 15 mpaka 20 kwa siku, lakini yakaja matatizo mawili makubwa kwanza moja ya tangazo lao waliliweka mahali ambapo lilikuwa ni kikwazo kwa visitors kuona post kwa urahisi na pili wakatoa masharti ya kunitaka nibadili lugha ya blog iwe full English, nikawaambia kwamba ule mwezi mmoja wamajaribio unatosha waende zao siwahitaji kabisa as far as biashara ya matangazo is concerned na ni the same thing with Pin Point na wao walitaka waweke matangazo yao kwenye blog yangu lakini niondoe matangazo yote ya biashara kwenye blog, wabaki wao tu nikawakatalia.

- Google wakanitumia check ya mwezi mmoja wa majaribio ndio ile niliyoiweka kuwahamasisha Vijana wengi waache matusi kwenye mitandao na wajikite kwenye kutafuta pesa kwa kutumia mitandao badala ya matusi na maneno ya kitoto kama yako ni waste kaka, umehangaika sana kuandika haya maneno yako kujaribu kuonyesha kwamba ninachosema ni uongo, sijawahi kukujibu kwa sababu nilidhani huna akili sawa sawa kwa sababu siajwahi kuona mtu anahangaika kama unavyofanya na habari ya hiyo check vipi una tatizo gani la binafsi kaka?

- Kama una tatizo la binafsi namba yangu ya simu ni 0717 618 997 nipigie nikusaidie maana umehangaika sana kuhusiana na hiyo check ya google, pole sana mkuu!!

Le Mutuz
 
Kama maelezo ya Le Mutuz ni kweli congrats kaka...ila pale uliposema sahv unashindana na michuzi mmmmmmm si kweli..kuna kijana MilladAyo anakimbiza mbaya...
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom