Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
UZINDUZI WA JUKWAA LA UWEZESHAJI WANAWAKE KIUCHUMI KATA YA MAKONGO
Mbunge Viti Maalum Wanawake Mkoa wa Dar Es Salaam na Mwanzilishi wa taasisi ya Tisha Mama Foundation, Mhe. Mhe. Janeth Elias Mahawanga amekuwa mgeni rasmi katika kuzindua rasmi Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Kata ya Makongo.
Mhe. Janeth Mahawanga ametoa pongezi nyingi kwa Serikali ya awamu wa sita kwa kutambua mchango wa Wanawake katika kukuza Uchumi wa Taifa na pato la Taifa kwa ujumla kwa kuendelea kuongeza fursa mbalimbali zinazozidisha chachu kwa Wanawake na Mabinti kupata mitaji ya shughuli zao mbalimbali za Kiujasiriamali.
"Ukiacha fursa ya mikopo ya Halmashauri, mikopo ya Wanawake, Vijana na Watu wenye mahitaji maalum kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum na sasa kuna hii fursa ya Majukwaa ya Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi."
"Niwaombe sana Wanawake na Mabinti tuzitumie hizi fursa kiufasaha lakini zaidi ya yote tuchape kazi ili fursa hizi ziwe na tija kwetu mtu mmoja mmoja, Familia zetu na Taifa letu." #Kamatafursatwendezetu #Wanawaketunaweza #TishaMamaFoundation
#TishaMama
#MamaVicoba
#ItazameDarKiutofauti
#Kaziiendelee