Uzinduzi wa Kampeni ya matembezi ya hiari kufanyika Februari 2021

Uzinduzi wa Kampeni ya matembezi ya hiari kufanyika Februari 2021

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,790
Reaction score
288,165
Askofu Mwamakula atazindua kampeni kubwa ya "Matembezi ya Hiyari" katika Jiji la Dar es Salaam katika Mwezi Februari 2021 katika siku na tarehe itakayotangazwa. Kampeni hiyo inalenga kuuhamsisha umma kuhusu umuhimu wa kuunda Tume Huru ya Uchaguzi na kuandika Katiba Mpya. Utaratibu wa matembezi hayo utakuwa kama ifuatavyo:

1. Washiriki wanashauriwa kuvaa barakoa (masks) ili kujikinga na Covid 19.

2. Washiriki watakaotembea na Askofu watatakuwa katika makundi makundi ambapo kila kundi halitazidi watu 10 ambapo kutakuwa na umbali wa mita 100 kutoka kundi moja hadi lingine.

3. Kundi la Askofu halitazidi watu 20 watakaoambatana naye

4. Washiriki wengine watatakiwa kujipanga barabarani ambako Askofu atapitia wakiwa wamevalia barakoa wakiachiana umbali wa mita 1 kati ya mtu na mtu.

5. Barabara zitakazotumika ni Morogoro, Malamba Mawili-Kinyerezi, Goba-Mbezi, Bagamoyo, Uhuru, Nyerere, Morogoro, Shekilango, Kilwa Road, Umoja wa Mataifa, Azikiwe, Kawe, Kigamboni, Chang'ombe, Mandela, Tabata-Segerea, Tandale kwa Tumbo, Kawawa, Bibi Titi Mohammed, Lumumba, Msimbazi, Tandika, Sam Nujoma, nk.

6. Siku ya kwanza itakuwa katika Wilaya ya Ubungo katika Barabara ya Morogoro katika Manzese na Mbezi kwa Yusufu.

5. Utaratibu utafanyika ili Askofu pamoja na baadhi ya waalikwa maalum waweze kuhutubia mikutano ya hadhara katika viwanja vya Kawe, Machava, Tabata, Mwembe Yanga, Mbagala, Biafra, Chanika, nk.

6. Washiriki watakaoweza watavaa t-shirts na kofia maalum zenye ujumbe kuhusiana na matembezi. Wasioweza watavaa mavazi ye yote!

7. Pale ambapo itashindikana kuhutubia mkutano wa hadhara, Askofu atahitimisha kwa kunywa maji au chai pamoja na watembeaji.

8. Matembezi yatakuwa yanaanza saa 8:00 mchana na yatakuwa yakifanyika katikati ya wiki ili kutoa nafasi kwa waajiriwa kushiriki.

Baada ya kumaliza kuzindua katika Mkoa wa Dar es Salaam, Askofu na timu yake wataelekea katika Mikoa ya Songwe na Mbeya kabla ya kuelekea Mikoa mingine. Mikoa itakayopewa kipaumbele kuanza ni ile ambayo itakuwa imekamilisha maandalizi mapema. Mkoa wa Songwe umekuwa wa kwanza kumuomba Askofu kuanza nao hivyo atazindua Tunduma! Hata hivyo, Askofu atafika katika kila Mkoa na kila Wilaya na hivyo matembezi yatadumu kwa muda wa mwaka mzima.

Tarehe ya matembezi kwa kila sehemu, wilaya au mkoa itakuwa ikitangazwa siku tano kabla. Utaratibu na mpangilio wa matembezi unaweza kubadilika kulingana na mazingira ya sehemu husika.

Vyama vya siasa, na taasisi za kiraia vinatiwa moyo kuhamasisha watu kujitokeza kwa wingi na hata kusaidia katika uratibu na maandalizi.

Sambaza ujumbe huu kwa kila mtu.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
 
Hao watu atawatoa wapi ikiwa mpaka sasahivi hakuna anayejua kwamba Kuna hicho kitu
 
Hakika siku moja watu hawa watakumbukwa kama mashujaa. Binafsi nimepata nguvu mpya baada ya kuona safari bado ii hai, na Mwenyenzi Mungu yu pamoja nasi. Hasa baada ya yale ya mwaka jana kuivunjavunja mioyo ya wapenda haki duniani kote. Nipo tayari kushiriki muda ukiwadia
Mungu atalinda taifa.
 
Hakika siku moja watu hawa watakumbukwa kama mashujaa. Binafsi nimepata nguvu mpya baada ya kuona safari bado ii hai, na Mwenyenzi Mungu yu pamoja nasi. Hasa baada ya yale ya mwaka jana kuivunjavunja mioyo ya wapenda haki duniani kote. Nipo tayari kushiriki muda ukiwadia
Mungu atalinda taifa.
Amina mkuu,nami nipo katika orodha ya watakao shiriki kwenye hayo matembezi maana hatuvunji sheria
 
Hao watu atawatoa wapi ikiwa mpaka sasahivi hakuna anayejua kwamba Kuna hicho kitu
Tushajiandikisha wengi sana na ma t-shirts yashanunuliwa mengi sana .

Kiufupi haya matembezi yatavunja record hapa Tanzania na wale waliofanya upuuzi wa kukataa au kukandamiza juhudi za kufufua mazungumzo ya katiba mpya wajiandaee
 
Hawa watu wamezuia jogging tu, sasa itakuwa matembezi (maandamano) ya hiari? It won’t happen. Au watu wenyewe kwa hiari yao watagoma kutoka nje kuhofia vipigo vya polisi
 
Hao watu atawatoa wapi ikiwa mpaka sasahivi hakuna anayejua kwamba Kuna hicho kitu

Kwa taarifa yako tupo, anaweza asipate watu wengi sana hasa hapa mwanzoni kutokana na hofu watu waliyojengewa, ila nakuhakikishia watu tupo bila kujali idadi yetu.
 
Yatakapofika Mwanza, nami nitashiriki. Nitachangia pia a galao barakoa 200.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Back
Top Bottom