Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
- Thread starter
- #21
Wana....Sh Mohamed
Leo nimejaaliwa kukipata kitabu
Ahsante
Nimefurahi kusikia hivyo.
Usisite kutueleza uliyoyakuta humo.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wana....Sh Mohamed
Leo nimejaaliwa kukipata kitabu
Ahsante
Sh MohamedWana....
Nimefurahi kusikia hivyo.
Usikise kutueleza uliyoyakuta humo.
Wand...Sh Mohamed
Kitabu nilikipata ikiwa tayari usiku na sikuweza kustahamili kukiwacha bila ya kukisoma
Kitabu nimekimaliza muda mfupi uliopita, Kweli kuna mengi ambayo muandishi ameyaeleza.
Kama ulivyosema ukikianza kukisoma basi unaingiwa na shauku ya kutaka kujua ukurasa wa pili una kitu gani.
Ahsante
Sh MohamedWand...
Ibrahim Hussein kafanya kazi mzuri Mashaallah.
Mwandishi maarufu wa hekaya Adam Shafi naye ni mmojawapo wa waliofungwa huko baada tu ya kuuliwa Abeid Aman Karume. Kaandika chochote kwenye hicho kitabu?UZINDUZI WA KITABU KIPYA CHA HISTORIA YA MAPINDUZI ZANZIBAR
Speaker: Mohamed Said
Chairperson: Hamza Zubeir
Date and Time: SUTURDAY 17 August 2024, at 4.00 PM
Venue: ZIRPP Conference Room, Tiger House
(Behind Majestic Cinema), Vuga.
''Mwandishi wa kitabu hiki Ibrahim Hussein amekianza kitabu chake kwa kumfanya msomaji kwa muda ahame kutoka jina la kitabu ahamie kwenye rejea za vitabu kuhusu wafungwa maarufu duniani.
Mwandishi anavipitia vitabu walivyoandika wafungwa hawa na wengine ambao si wafungwa bali ni waandishi wa riwaya lakini zinazohusu vifungo vya kutisha.
Katika wafungwa hawa yumo Ngugi Wathiong’o ambae zamani akijulikana kama James Ngugi.
Ibrahim Hussein kwa namna ya pekee kaingia katika orodha ya Wazanzibar walioandika historia ya mapinduzi na kutuwekea mengi ambayo kabla hayakufahamika.
Ibrahim Hussein katika kitabu chake hiki ameliondoa pazia kumwezesha msomaji kuwajua wale waliokuwa Kwa Bwamkwe kwa kutaja majina yao na kuweka picha zao.
Kwa ustadi mkubwa mwandishi anakuchukua katika safari yake ya kwenda Kwa Bamkwe kituo kwa kituo.
Anaanza kwa staili ya ‘’dramatis personae’’ kama William Shakespeare anavyowatambulisha wahusika katika michezo yake.''
View attachment 3069090
Itabidi nikitafute hicho kitabu, namfahamu Adam Shafi, kweli alifungwa wakati huo.Kwa Bamkwe ni jela ya kinoa miguu Zanzibar. Mateso yaliyowapata wafungwa wa uhaini baada ya kuuwawa Karume mwaka 1972
Kitabu cha Haini cha Adam Shafi pia kimeeleza mateso hayo ingawa yeye kaficha majina na kaiweka kama story.
Nilikuja kujua baada ya miaka kadhaa kuwa muhusika mkuu kwenye kitabu cha Haini 'Hamza' ndio yeye mwenyewe mwandishi Adam Shafi
Kitabu cha Haini ni kitabu ambacho ukianza kukisoma hutatamani kukiweka chini mpk ukimalize. Na ukizingatia lugha tamu ya mwandishi kimenoga hatari
Wandugu...Sh Mohamed
Hakika Sh Ibrahim amefanya kazi nzuri
Samahani Sh Mohamed, ninajaribu kukitafuta kitabu cha “Kwaheri ukoloni kwaheri uhuru”
Jee nitaweza kupata soft copy?
Natanguliza shukurani
Sh Mohamed…Wandugu...
Ingia Google kipo hapo.
Afwan.Sh Mohamed…
Shukurani kwa msaada
Ahsante
Sheikh navipata wapi hivi vitabu.....?Afwan.
Babu...Sheikh navipata wapi hivi vitabu.....?
Nataka kuvinunua
JK,Mohamed Said ,
..tafadhali mtafute Brig.Gen.Simba Waziri Simba, mtoto wa Kariakoo, na shujaa wa vita vya Kagera.
..huyu bwana alikuwa Mkuu wa kikosi wakati wa vita, na akawa muanzilishi wa chuo cha jeshi la Uganda kilichoko Jinja.
..kwa kweli tusiache historia ya mashujaa kama hawa ikapotea.
Proud of you mzee wangu. Shukran sana kwa elimu ya bure unayotupatia hapa.UZINDUZI WA KITABU: ''MIMI UMMA PARTY NA MAPINDUZI YA ZANZIBAR'' 2019
Kwa wale walionisoma siku tatu zilizopita nilipokieleza kitabu, ''Mimi, Umma Party na Mapinduzi ya Zanzibar,'' kilichoandikwa na Comrade Hashil Seif Hashil niliweka miadi ya kurejea mara nitakapokimaliza kitabu.
Nimekimaliza kitabu leo asubuhi.
Kitabu hiki ni kitabu kizuri sana na ukikianza huwezi kukiweka chini.
Wengi wa wanachama wa Umma Party ambao Comrade Hashil amewataja ni watu ambao wengine tunafahamiana kwa karibu kwa miaka mingi na wengine nawafahamu kwa kuwaona kwa mbali.
Katika hawa wengi wao na naweza kusema takriban wote si watu wanaopenda kuzungumza kuhusu Umma Party na mchango wao katika historia ya vyama vya siasa Zanzibar hadi kufikia mapinduzi ya mwaka wa 1964.
Hili linaeleweka kuwa wengi wa wanachama wa Umma Party walikuwa awali wanachama wa ZNP yaani Hizbu na kuna wakati neno ''Hizbu,'' lilitisha na kwa ajili hii hakuna aliyetaka kunasibishwa na jina hilo.
Hali kama hii Waingereza wanaita, ''stigma.''
Comrade Hashil Seif hakukumbwa na maradhi haya na hakika anajifakharisha kwa kuwa mwanachama wa Umma Party, chama ambacho kwake kilikusudia kuwaletea Wazanzibari uhuru wa kweli na haogopi kusema kuwa yeye ni mfuasi wa Babu na Karl Marx.
Comrade Hashil Seif kaeleza haya na kaiweka, ''Manifesto,'' ya Umma Party ndani ya kitabu chake kwa wote kuishuhudia.
Hakuishia hapo kama nilivyosema awali kaeleza bila ya hata kuuma maneno mipango waliyokuwanayo ya kupindua serikali ya Zanzibar na kuweka serikali mbadala itakayofuata siasa za Karl Marx.
Hakika Wazanzibari waliwatangulia wengi Afrika na katika mengi.
Iko siku ya miaka mingi iliyopita nikiwa na Ahmed Rajab tukikata mitaa ya London tukapita mahali akanionyesha nyumba akaniambia, ''Hapo ni ndipo Karl Marx alipokuwa akija akikaa hapo na kuandika fikra zake na Haroub Othman alipokuja London kwa mara ya kwanza aliniomba nimlete hapa apazuru."
Sidhani kwa nyakati zile kama kuna Mtanganyika yeyote ambae alikuwa na ghera ya kuweza kuchukuliwa kiasi kile cha mapenzi ya siasa za Karl Marx za Kisoshalisti.
Wazanzibari walikuwa wameshatangulia na vijana akina Hashil na wenzake kutoroka Zanzibar kwenda Cuba kwa mafunzo ya kijeshi na ambayo yalikamilika.
Kueleza haya kunahitaji ujasiri mkubwa.
Kubwa katika kitabu hiki ni kauli ya Comrade Hashil kumsifia Dr. Ghassany kwa kitabu chake, ''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru,'' ingawa yapo ambayo
amesema hakubalianinayo.
Lakini muhimu Comrade Hashil Seif kukiri kuwa Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka wa 1964 hayakutokana na mipango ya Babu na Umma Party au ile iliyokuwa katika fikra za baadhi ya wanachama wa ASP kama Abdallah Kassim Hanga na Hassan Nassor Moyo.
Kilichonishangaza sana katika maelezo ya Comrade Hashil ni ukimya wake kuhusu askari mamluki wa Kimakonde kutoka Kambi ya Kipumbwi walioingia Zanzibar kwa siri kuja kuisaidia ASP katika mapinduzi.
Kitabu cha Comrade Hashil Seif ni muhimu sana kwa kuielewa historia ya Zanzibar na mashujaa wake Umma Party wakiwa ni wamojawapo kwa mchango wao mkubwa waliotoa katika uongozi baada ya serikali ya Mohamed Shamte kuanguka.
Bila ya uongozi wa Umma Party na watu kama Badawi Qulatein damu nyingi ingemwagika na Mji Mkongwe ungetiwa Kibiriti uteketee.
Mwaka wa 2022 nikaalikwa tena Zanzibar kwenda kukieleza kitabu hicho hapo chini:
KUMBUKUMBU ZA "THEORETICIAN" KHAMIS ABDULLA AMEIR "MAISHA YANGU" 2022
Ndugu zanguni taarifa hiyo hapo chini kutoka Zanzibar kuhusu kitabu hiki ambacho naamini ndicho kitakuwa kitabu cha mwaka kwa kuufungua na kuufunga In Shaa Allah.
Kitabu kitawasili Zanzibar In Shaa Allah mwisho wa mwezi huu wa May au mwanzoni June.
''Maisha Yangu: Miaka Minane Ndani ya Baraza la Mapinduzi- Khaini au Mhanga wa Mapinduzi ya Zanzibar.”
Watu wengi wakiniandikia kutaka kujua kitabu kitafika lini na kitapatikana wapi?
2024 nimealikwa tena Zanzibar kukifanyia pitio kitabu cha Ibrahim Hussein:
Proud of you mzee wangu. Shukran sana kwa elimu ya bure unayotupatia hapa.
Ahsante.Ahsante.
Hivi ni kwanini licha ya vitabu mbalimbali vinavuhusu mapinduzi ya Zanzibar kuandikwa lakini Bado wazanzibari (hasa wananchi )A
Ahsante.
Usidhani kila anayekwenda kwenye sherehe anasherehekea.Hivi ni kwanini licha ya vitabu mbalimbali vinavuhusu mapinduzi ya Zanzibar kuandikwa lakini Bado wazanzibari (hasa wananchi )
Bado wanajitokeza kusherehekea sherehe hizo ...???
FaizaFoxy Mohamed Said Angel Nylon
UnafikiHivi ni kwanini licha ya vitabu mbalimbali vinavuhusu mapinduzi ya Zanzibar kuandikwa lakini Bado wazanzibari (hasa wananchi )
Bado wanajitokeza kusherehekea sherehe hizo ...???
FaizaFoxy Mohamed Said Angel Nylon