Uzinduzi wa Ripoti ya 'Wanawake Wanaoongoza katika Huduma za Fedha

Uzinduzi wa Ripoti ya 'Wanawake Wanaoongoza katika Huduma za Fedha

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
International Finance Corporation (IFC) leo Juni 24, 2021 inazindua Ripoti ya 'Wanawake Wanaoongoza katika Huduma za Fedha: Uchunguzi wa Usawa wa Kijinsia katika Sekta ya Huduma za Kifedha za Tanzania'

#JamiiForums

=====

UPDATES;

======

Jumoke Jagun-Dokunmu: International Finance Coroporation (IFC) imekuwa ikifanya kazi na Sekta Binafsi kwa miaka mingi kuinua Usawa wa Kijinsia na kuziba pengo

Wanawake wengi wanahitajika katika nafasi za juu ili kuonesha mfano

Jumoke Jagun-Dokunmu (IFC): Ikiwa Wanawake watawakilishwa kwa Usawa kama Watendaji, Mameneja, Wanabodi, Wajasiriamali, Wateja na Wanajamii wanaweza kusaidia kubadilisha Uchumi wa Afrika

Jumoke Jagun-Dokunmu (IFC): Utafiti uliofanywa na Benki ya Dunia hivi karibuni unasema Mataifa Ulimwenguni yanapoteza Dola Trilioni 172 kutokana na utofauti wa mapato kati ya Wanawake na Wanaume

Aida Sykes (IFC): Mapungufu katika usawa kwa kijinsia yapo kwenye huduma za kifedha kwa upande wa wateja na maeneo ya kazi

Kutokana na utafiti wetu kwenye Ripoti hii, tunajua kuna mapengo ya kijinsia ktk Uongozi; 34.6% (Ngazi ya Bodi), 43.8% (Ngazi ya Juu ya Menejimenti)

Aida Sykes (IFC): Ripoti hii inathibitisha
vitu vinavyokubalika kwa kiasi kikubwa kama vikwazo kwa Wanawake katika maeneo ya kazi:

- Kukosekana imani kuwa Wanawake wanaweza kuongoza

- Unyanyasaji na Ubaguzi wa kijinsia

- Majukumu ya Malezi kwa Watoto

Aida Sykes (IFC): Kampuni 4 kati ya 5 zilizofanyiwa utafiti zimetoa kipaumbele kwa usawa wa kijinsia. Kati ya Kampuni zote 5, ma-CEO ni wahamasishaji wa usawa wa kijinsia

60% ya Wanawake kwenye utafiti wanachukulia Wanawake katika Nafasi za Juu za Uongozi kama mfano wa kuigwa

Aida Sykes(IFC): Kampuni zote 5 zilikuwa na Sera za Usawa ktk Fursa za Ajira. Ziliripoti kutumia lugha isiyoashiria usawa kwenye maelezo ya kazi

Pia, ziliripoti Wanawake na Wanaume hupata Mshahara sawa kwenye kazi zinazofanana, japokuwa Kampuni moja pekee ilikuwa na Sera rasmi

Aida Sykes (IFC): Kampuni moja inatoa wiki 20 za mapumziko ya uzazi, ikiwa ni wiki 6 zaidi ya Sheria za Tanzania zinavyoelekeza

Pia, inatoa wiki 11 ya mapumziko ya Uzazi kwa Baba, ikiwa ni siku 11 zaidi ya mujibu wa Sheria za Tanzania

Aida Sykes (IFC): Ripoti yetu inajumuisha mapendekezo kadhaa kuhakikisha usawa wa kijinsia

Baadhi ni:

1) Kuziba pengo kati ya Sera na Vitendo

2) Kutoa mafunzo ya lazima kwa Wafanyakazi na Mameneja wote kuhusu masuala muhimu kuhusu Usawa wa Kijinsia

Mwanahiba Mzee (Ecobank): Ninachoweza kupendekeza kama Kiongozi ni tunahitaji kuwa karibu na Wanawake tunaotaka wakue

Inatakiwa kuwa na jicho la kuwatambua na kisha kuwahusisha katika kazi unayodhani wanaweza kufanya vizuri

#Finance2EqualTanzania #JamiiForums

Mwanahiba Mzee (Ecobank): Wanawake tumebarikiwa, tunasikiliza. Hiyo inatokana na masuala ya uzazi

Hivyo, tuweke masikio yetu kusikiliza na kusaidia Wanawake wengine ili waweze kukabiliana na changamoto walizonazo na kusonga mbele

#Finance2EqualTanzania #JamiiForums
 
Mwanahiba Mzee (Ecobank): Ninachoweza kupendekeza kama Kiongozi ni tunahitaji kuwa karibu na Wanawake tunaotaka wakue.

Inatakiwa kuwa na jicho la kuwatambua na kisha kuwahusisha katika kazi unayodhani wanaweza kufanya vizuri

#Finance2EqualTanzania #JamiiForums
 
Ni pale tunapopigania jinsi / kiasi cha kugawana Keki, tunasahau kutengeneza Keki yenyewe....

Anyway acha tu tugawane umasikini...
 
Wanawake wakipewa nafasi wanaweza kufanya vizuri sana.

Ni muhimu taasisi za fedha zikawaamini na kuwapa nafasi za juu ili waweze kuonesha ufanisi wao.
 
Back
Top Bottom