The redemeer
JF-Expert Member
- Jan 28, 2025
- 4,778
- 8,232
Wengi tulikuwa hatufahamu wale wasichana wadogo wanaotaniwa na babu zao kwa jina la "mke wangu" au "Mchumba" alafu baadae siku akija kumuoa kuna fedha huwa zinatolewa kwamba ni kumwachanisha mtu na mkewe, yaani babu kumwachanisha na mjukuu wake wa kike, usifikiri ule ni utani sio utani.
Babu anaamua kumwita mjukuu wake mke ili kwenye macho ya watongozaji anawatengenezea picha kishirikina aonekane mzee.
Miongoni mwetu kuna wadada hawatongozwi kwasababu wanaonekana ni vibibi hiyo ni roho ya kipepo wanakuwa wametengezewa, maagano tunayoweza kuyavunja ni maagano yale ya wachawi yale ya ngono huwa hayavunjiki.
Watu wanapomaliza kuapa huwa wanaambatanisha na fedha kama inavyofanyika kanisani au msikitini wanavyoambatanisha na pete. Yupo mtu anamhudumia mpenzi wake kwa kumnunulia Luninga, Friji, simu nk ile nguvu ya kumhudumia inasukumwa na msukumo wa kiapo kwa lugha nyingine bila kiapo asingetoa hivyo vitu.
Kwa hiyo mwili wako umefungwa na kiapo, mwingine analalamika hata njiani hasalimiwi, anasahau kuwa sehemu ya unene wa mwili wake umetokana na mali au vyakula vya kiapo, wapo wasichana wana magauni wameyapata baada ya kiapo kutolewa kwanza.
Kuna kiapo watu walijiapiza kwa jina la mwenyezi Mungu, "Mungu wangu sitakuacha Senzota milele" mbingu inazuia usijiapize kwa neno la Mungu, lakini wewe ukaamua kumuapia mpenzi wako kiapo chako cha ngono unajiapiza kwa Mungu wako wa mbinguni.
Biblia imesema usijiapize kwa jina lake unapoapa, wanataka utekeleze viapo sawa na ulivyoapa, watu wengi wanafirisika, maisha yanaharibika kwasababu mwanamke uliyenaye ana viapo vya watu wengiwengi na kila kiapo chake lazima kitimilizwe.
Ndio maana mbinguni walitaka uwe huru usiape, wanajua ukiapa lazima utimize.
Mwili wa msichana yeyote wa rika lolote kama una viapo vya wapenzi wako jiandae kukaa ndani ya ndoa bila amani, kwanini? kwasababu uliapa kipindi ambacho nafsi yako ina msisimko wa mapenzi, Pia kila mwili wa mwanaume yeyote aliyejiapiza kwa watu tofauti tofauti hatakuwa na ndoa hata moja ya kumfurahisha mke wake.
Labda apate aliyekongoroka, jua limezama, matumaini hayapo, amekaa kama vile bamia na yeye anatafuta wapi mtu wa kudondoka nae, Utasikia "Natafuta mtu wa kuzeeka nae."
Jinsi unavyoendelea kutafuta wapenzi wapya ili kutafuta amani ya mapenzi ndivyo unavyozidi kuvunja idadi ya viapo vyako, ndio maana ukitaka kuoa binti hupaswi kuongea na binti huyo unapaswa kuongea na baba yake moja kwa moja.
Wanawake wa kuoa wote huwezi kumkuta barabarani, wanawake wote katika vitabu vitakatifu walioolewa walikuwa wanafanya kazi za baba zao na kazi za nyumbani.
Yesu anakataza usiape kabisa hata kwa mbingu maana ndicho kiti cha enzi wala kwa nchi maana ndipo anapoweka miguu yake wala kwa Yerusalemu maana ndio mji mkuu, wala kwa kichwa chako maana huwezi kufanya unywele wako mweupe ukawa mweusi.
Kwakuwa Mungu kakataza watu wasiape na usiape kwa nchi mbingu au kanisa hivyo kuna wazazi wengi wanapitia changamoto za afya na hawaponi hata wanywe damu ya Yesu kwasababu kiapo cha sehemu za siri mwao bado kinaendelea kutumika na binti yake ama kijana wake ambaye ni mzinzi.
Pia utasikia baba au mama kavamiwa ghafla na tabia mbaya kumbe ana binti yake kaapishwa kizinzi na hicho kiapo kakabidhiwa binti huyo, yaani "Mimi ukinikuta na mtu mwingine ukoo wangu wote wafe" Ukiapa kwamba mwili wako hautaguswa na mtu yeyote siku akija mtu mwingine kuugusa mtu huyo atadaiwa kuwa kavamia kiapo, ni sawa na ukimtongoza mwanamke mwenye pete kwasababu pete inamzuia mtongozaji asikutongoze.
Ukilala na mtu mwenye kiapo cha sehemu za siri kilichotolewa wakati watu wanazini utashtakiwa na ulimwengu wa roho wa mapenzi, kuwa umeingia mahali ambapo sio pako, hivyo utalazimika kulipa gharama.
Yupo mtu analalamika "Oooh mimi mwanaume nikilala nae hanirudii tena" jiulize una kiapo cha nani? kuna mtu anafanya kiapo cha uzinzi alafu anarudi kwenye nyumba ya baba na mama yake.
Akirudi anamdanganya mama yake kuwa katoka mjini alafu anamwapia mama yake kiapo cha uongo hata kwa kutema mate chini. Mara alipoingia tu ndani kuna sensa ipo tumboni, nafsini mwa mama yake ikahisi kuna kitu tofauti, sensa inajaribu kumwambia mama msaidie mwanao ana kiapo akitengue kabla hajalala.
Binti anajikuta anaua sensa ya mama yake kwa kiapo cha pili cha uongo kisisensi mambo yake, anaua kipawa cha mama yake kinachotambua mambo yanayompata, kipawa kinauawa hivyo nguvu ya roho mtakatifu inakufa kwa mama huyo hivyo atashindwa baadae kumuombea mambo yake hata akiwa na nia ya kumsaidia hayatatokea.
Pia unaweza usijiapize lakini ukamjibu mama kwa kiburi, Wazazi wengi yale macho ya rohoni au ile nguvu ya kujua mtoto wao kesho atapata majanga gani imeuawa, hawaioni tena sababu vijana wao wamefunga maagano.
Utasikia "Sikuachi mpenzi wangu labda mama yangu afe" kuna watu leo walemavu, wagonjwa, nk lakini ni matokeo ya viapo vya uzinzi.
Kama wewe ni mke na una watoto au wewe mume na una watoto basi hao watoto ni sehemu ya kiapo chako cha uaminifu ulichoapa hapo zamani ulisema, nitakuwa na wewe tu sitakuwa na mtu mwingine kile kiapo unakivunja kwa kwenda kuvua nguo na kuzini na mtu mwingine.
Viapo vyote chini ya jua vilifundishwa na wale malaika walioshuka mbinguni baada ya kuwatamani wanawake wa kibinadamu, Mwanzo 6. Malaika Cabataliel chini ya Semhazar yeye aliwafundisha binadamu jinsi ya kuapa viapo, aliwafundisha kwasababu malaika hawakuwa wanaoa wanawake wengi waliogopa wasiingiliane.
Ukifanya kiapo unafanya kiapo na vitu vingi sana, kila kiapo unachovunja unakaribisha mapepo yanayokuja kudai kiapo chao.
Mtoto anaposumbuka sana basi ujue maagano yamekusanyika yanadai kiapo chao, kwanini watoto wa miaka hii wanachangamoto za vitu vingi sana ? wanapenda kuwa mashoga, mtoto wa kike anajisikia kusagana, hali hii sio ya kawaida.
Watoto wengi wanakuwa na changamoto ya kuwatii wazazi wao kwasababu tumbo la mama linamuonyesha ana mababa wengi kwasababu ni mtoto wa maagano mengi kwahiyo akikaa anamuangalia mama yake anamuona huyu mama ananizingua.
Ulimwengu wa roho unamsemesha unamwambia achana na mama yako huyo mwili huu sio wake au baba yako siyo huyu, hivyo nafsi ya mtoto inakosa maamuzi imsikilize nani, amuogope nani amuheshimu.
Kwasababu wapo wanawake wana viapo mpaka vinafika 9 wamevitoa kwa watu mbalimbali toka walipokuwa shule ya msingi.
Ardhi hii tunayoilima ina agano la Nuhu, Mungu aliposema usiape wala usijiapize kwa nchi wala kwa mbingu ana maana mbingu na nchi imeshakamata agano la kudumu la majira kwa hiyo unapofanya maagano yote agano la Nuhu linaanza kukukimbiza utoke kwenye nchi ufe mapema, hivyo linaingia kwenye vita na wewe.
Ndio maana Marais wanapoapa wanasema" Mungu anisaidie" ili kama kuna vita ya kimaagano Mungu huwa anawajibika.
Agano zuri ni la bikira siku anapoapiziwa anayeshikilia lile agano inakuwa ni ile damu ya ubikira, tofauti na haya maagano mengine ya kimapenzi ambayo nchi inasikia ukiyatamka.
Agano mama la Nuhu lina milango saba, ndio maana lina aina saba za rangi, ile nyekundu ni kwa agano la damu, njano kwa madini, kijivu kwa toba kuteketea kujitoa kafara, bluu kwa maagano ya kimbingu nk.
Mahali popote penye maagano ya kimapenzi yanayohusianisha ndoa sio ya kuyaingilia, Mungu aliweka mume kwa mke mmoja na mke kwa mume mmoja, bali shetani alijiingiza katikati akawa wa tatu.
Unapotoa sadaka yako kwaajili ya kutengua uzinzi kitu cha kwanza ambacho inabidi ukiweke mule ndani ni viapo ulivyowaapia watu, mahali popote unaposukumwa uweke kiapo elewa huo ni mtego, kumbuka watu wote ambao umeweka nao kiapo na sadaka zako siku ya kesho zikufanye uwe mpya kwa sura mpya.
Amua kutoka ndani kuziamrisha hisia zako zirudi kwenye asili yake, tenganisha mwili, nafsi na sehemu zako za siri zisiwe na ushirikiano kwenye masuala ya uzinzi ili litakapokuja agano la ndoa ndipo viletwe vyote vishirikiane.
Jifundishe kuwa mkweli wa viapo vyako na kuvisimamia na kama hujaoa weka kiapo wewe ni mfanyabiashara mkubwa ngono isiingilie kati, kama hujaolewa weka pia kiapo kuwa mwili wangu ni kwaajili ya mume wangu pia ni mfanyabiashara mkubwa ili ngono ikija ikukute una nadhiri ya ufanyaji biashara.
Mwisho fanya sadaka kila mara ili kuimarisha agano lako la biashara ili upunguze tamaa ya mwili na uharibifu wake.