Uzinzi pekee ndo dhambi isiyofutika kwa watu

Uzinzi pekee ndo dhambi isiyofutika kwa watu

The redemeer

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2025
Posts
4,778
Reaction score
8,232
WANADAMU HAWATA SAHAU JUU YA DHAMBI YAKO YA UZINZI🔥🔥
Mungu husamehe dhambi zote ikiwemo dhambi ya uzinzi au zinaa.

Ikiwa wewe unasema umeokoka ukizini na mke au mume wa mtu au na yeyote;jambo hilo likibainika kwenye jamii yako,basi wanadamu hawatakaa wasahau hilo tukio.Hata kama umeacha na umekuwa mtakatifu sana,bado wanadamu watakuona mzinzi tu.

Ukiamua kuzini jua pia umeamua kuwa tayari kupata fedheha ya kudumu pindi utakapo julikana.Imeandikwa{ mithali 6:32-33,mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa;Afanya jambo litakalo mwangamiza nafsi.Atapata jeraha na kuvunjiwa heshima;Wala fedheha yake haitafutika }.

Hivyo unaweza kusamehewa na Mungu na Yerusalem mpya utaingia kwa sababu ya kutubia dhambi zako,ikiwemo zinaa.Pamoja na kusamehewa na Mungu kabisa kwa 100%, lakini kwenye kumbukumbu za wanadamu hawatakaa wasahau huo uzinzi wako.Utakuwa mtakatifu anayeishi kwa fedheha kutoka kwa wanadamu walioshuhudia huo uzinzi wako.Watakunyoshea vidole mpaka siku unaingia kaburini kwa sababu ya kutenda hiyo dhambi na wakajua.

Ndiyo maana dhambi ya uzinzi siyo ya bahati mbaya ni dhambi ya makusudi kabisa.Hakuna anayeenda guest house au lodge kuzini kwa kupitiwa na shetani,au kwa bahati mbaya tu.Acha uzinzi mpendwa lasivyo hilo andiko litatimia kwako,siku ukibainika kuwa unazini.Fedheha yako haitafutika kamwe kwa wanadamu kwenye maisha yako, hata ukitubu na kusamehewa na Mungu.

Fedheha hii huwaathiri zaidi wanawake kuliko wanaume duniani.Ndiyo maana wanaume wengi wakigundua wake zao wanazini inawawia vigumu sana kuwasamehe na kuendelea kuishi nao.Na hata wakisamehe jambo hilo hutumika Kama fimbo ya mambo mengi kwenye ndoa.

Jiunge na group la Nuru ya Injili International WhatsApp, ili ujifunze Neno la Mungu kila siku kwa njia ya sauti.By pastor Mfinanga+255622668897.
 
Hata kama ulizini ukasameheka haifutiki hio ni aibu yako ya milele utatembea nayo hadi kufa.
Thus wengi huwa wanashindwa wanaamua kutengana tu.
Dhambi ya uzinzi ina nguvu sana na ndo dhambi inayoua upendo kuliko dhambi zote.
 
Kama Mungu amenisamehe mwanadamu atanifanya nini?

Fedheha huonekana kwa anaejihisi
 
Back
Top Bottom