Wadau,
Naandika kuomba msaada kwenu kwa sababu sasa hali hii kwangu imekuwa too much. Miaka miwili iliyopita nilikuwa na uzito wa kilo 94 sasa umeongezeka hadi kufikia 118 licha ya mazoezi ninayofanya. Kwa sasa nina umri wa miaka 40. Ni ME!
Sina magonjwa yoyote lkn siupendi uzito huu. Madaktari kila ushauri wanaonipa sioni breakthrough ya hali hii.
Wana JF Doctor, naomba msaada!
Unafanya mazoezi ukimaliza unakula ma burger,kitimoto na mi bia kupungua ni ndoto jombaa
Check your life style my friend! Unafanya kazi yenye kipato kikubwa siyo? Anyway jaribu ushauri uliopewa na wadau in case utashindwa nijulishe nitakuelekeza progamu itakayokupunguza uzito! kwa kuanzia kila siku asubuhi amka na glasi ya maji moto. Kata limao moja na kamulia kwenye maji hayo. Kunywa ikiwa moto! Punguza vyakula vya nyama na mafuta mafuta na vyakula vya wanga. Hiyo bia aisee punguza. Kula mboga za majani na matunda kwa sana. Fanya mazoezi. Na sio kila wakati uko na hiyo BMW yako. Paki ukitoka job tembea tembea kwa miguu. Kuna programu inayopunguza kilo 3 kwa kipindi cha siku 7. Wala haihusiani na kujinyima chakula kama wafanyavyo wengine. halafu pia epuka madawa na progamu zinazopunguza uzito mkubwa kwa kipindi kifupi. Ni HATARI kwa afya yako. Hebu piga hesabu ideal weight yako unapaswa kuwa utatumia siku ngapi kuifikia kwa progamu hiyo!
Pole wataalamu wanasema 'You are what you eat'.Huo ni utapiamulo pia. Badilisha mlo wako. zidisha, matunda,mbogamboga, maji mengi, vyakula vya protein kula kidogo, mafuta na wanga kidogo zaidi. Fanya mazoezi na kutembea kwa miguu itakusaidia. Waweza kunipigia nikushauri zaidi na program rahisi za kupunguza uzito. Huo ni tatizo kwa magonjwa kama kisukari, moyo,figo yatakunyemelea kama hutapunguza uzito huo. Ingawa sijajua urefu wako ambao ni muhimu kujua pia. 0689417472
Shkamoo mkuu. Mimi kama mwanachama wa EDMARK Tanzania. Tuna lishe na program ambayo itakusaidia kuweza kupunguza uzito.
MRT (Meal Replacement Therapy) complex. Ambapo unafanya mpangilio wa chakula na tunakupa bidhaa ambayo inasaidia kuchoma mafuta na kuweka mwili sawa.
Maelezo ni marefu sio rahisi kuelezea hapa.
Kama utapenda unaweza ukaniambia kwenye namba 0685661790 tukapanga siku nikakuelezea kwa undani zaidi
Sio moto sana kama yale ya chai, hapana kawaida tu!Nashukuru sana kamanda kwa ushauri wako. Madaktari wanaonishauri hawajawahi kuniambia juu ya maji moto, wamekuwa wakinishauri kunywa maji ya kawaida, ya vuguvugu.
Nafanya mazoezi mkuu.
Nitafuata ushauri wako wa kunywa maji moto na limau kama ulivyonishauri!
Nawashukuru nyote mliochangia kwa ushauri wenu. Nikifanya mazoezi situmii ma burger, bia wala kitimoto. Aidha sina ulaji mbaya, nakula kikawaida sana na urefu wangu ni 5.9' na kazi yangu ni ya kipato cha kati kama m.3 @ mwezi.
Nimeshauriwa kunywa maji mengi na matunda najitahidi kutekeleza!
Nawashukuruni wote!
mi ninataka kuongezeka nina urefu sawa na huyo bwana 5'9 ila nina kilo 63 natamani zifike 75 nifanyeje ,kula nakula ,sina stress,ni kweli kabisa. hata akitumia dawa hazitasaidia maana anachotakiwa ni kubadili ulaji wa vyakula na lifestyle.