Uzito huu nao ni kero

mi ninataka kuongezeka nina urefu sawa na huyo bwana 5'9 ila nina kilo 63 natamani zifike 75 nifanyeje ,kula nakula ,sina stress,

Ht mm nilikuwa na kilo km zako ila kuanzia mwaka jana nimepanda mpk 70 na nikishuka inafikia 67. So nacheza kati ya 67 to 70. Japo natamani nifikie 75 siku moja.

Ukiniuliza uzito umeongezekaje ntakwambia ni kula sio kila chakula ila aina fulani ya vyakula vya nguvu na mchanganyiko wa mboga mboga na matunda. Bila kusahau kupumzisha mwili kwa mda mrefu.

Ni hayo tu.
 
Body mass index yako inaonyesha uko severely obese or obese class two.

5.9ft=179.83cms,118 kg, BMI yako ni 36 kaka unaelekea kubaya,badili mfumo wako wa chakula na lishe.

Unajiweka katika hatari kubwa ya kupata heart related complications kama cardiopulmonary arrests nk. Uko extremely overweight ukilinganisha na urefu wako.

Mimi sio daktari ila nakushauri kama unakunywa pombe,kula vitu vya mafuta uache. Kupunguza huo uzito inabidi ukubali kujitesa mkuu.kuongezeka kilo moja ni rahisi ila kuitoa ni mbinde.
 

Najaribu kila kitu mkuu but all with no avail. Najinyima kwa muda lkn nikija kula njaa inakuwa kali sana. Bia sinywi nakunywa sana maji na nakula matunda na mboga za majani kuliko vyakula vingine. Siongezeki tena lkn pia sipungui!
 
Tunaweza kuchat kupitia
+255657830098
Ili nikupe njia nyingine rahisi ya kupunguza uzito bila kufanya mazoezi.. Inawezekana kisayansi. Just text me.

Tupia hapa nasie tuelimike! Mi Nina kilo 92 urefu ni 5.8 mahitaji kupunguza hizi kilo kadhaa
 
Kwa kifupi ni kwamba,kazi moja wapo ya ini(liver) ni ku-produce mafuta kwny mfumo wa cholesterol.. Cholesterol kwny mwili wa binadamu ina kazi nyingi.. Tuelekee kwny mada husika. Endapo mwili wa binadamu unapokuwa umezidiwa na sumu, kinachofanyika ni kwamba, liver inatoa zile cholesterol(mafuta) kwenda ku-protect vital organs kama moyo,utumbo n.k. na ndio maana watu huanzia kunenepa tumboni.

So ili kupunguza unene inabidi tupunguze kwanza sumu mwilini. Ni hilo tu, hata hakuna haja ya mazoezi.
 
Kama ni wafuatiliaji wazuri.. PROVE>> kwamba
Unaweza kufanya mazoezi lakini usipungue unene, au ukapungua kwa kiasi kidogo. Hii ni kwa sababu sumu bado ipo mwilini,kwa hiyo ini(liver) linaendelea kuproduce cholesterol kwa wingi ili kuprotect vital organs.. Ni hayo tu ndugu zangu.
Kwa msaada zaidi tuwasiliane kupitia:
+255657830098
Email: shelbytheseeker@outlook.com
 
wakuu me pia nina uzito mkubwa urefu 5,6 kilo 82 jee hapo natakiwa nipunguze ngapi?umri wangu 22 years
 
wakuu me pia nina uzito mkubwa urefu 5,6 kilo 82 jee hapo natakiwa nipunguze ngapi?umri wangu 22 years

wakati Mimi nikiwa na 22 yrs nilikuwa na kilo 91 na nilikuwa nafanya sana mazoezi ya viungo najipinda kama kambale sa hivi cwezi kunjika kabisa. Nina 40 yrs now.
 

Mkuu SHELBY THESEEKER, umesema kweli, mie mazoezi nimefanya ya kila aina lakini nashangaa uzito haupingui ingawa cjiskii maumivu yoyote na pia sina kisukari wala pressure!
Hiyo namba kwa watsup nakupata?
 

Mimi nafikiri upunguze kula vyenye mafuta
 
Najaribu kila kitu mkuu but all with no avail. Najinyima kwa muda lkn nikija kula njaa inakuwa kali sana. Bia sinywi nakunywa sana maji na nakula matunda na mboga za majani kuliko vyakula vingine. Siongezeki tena lkn pia sipungui!

jipe moyo mkuu utapungua ingawa najua mziki wake,mimi nilikua na kilo 96,ilikua ishu kuzipunguza hadi 88,kupunguza uzito sio mchezo,BMI yangu ilikua 26.something na sikutaka izidi 25 kwa hiyo nilipta tabu sana kurudi 25 na hua sitaki izidi hapo.
 
Usile wali mkuu, usile ugali mkuu, mikate sijui maandazi achana navyo, mikate acha, viazi ulaya acha, pendelea kula viazi vitamu badala ya ulaya, nyama kula, lakini pendelea sana ya kuku, samaki na mboga mboga kwa wingi, kama ni lazima kula wali ama ugali, basi angalia vinavyotakiwa vikushibishe siyo wali wala ugali, mboga ndiyo hiwe nyingi, wali ama ugali kiduchu mno,pendelea kula mara kwa mara lakini kidogo tu, siyo unakunywa chai asubuhi mpaka usiku, kula ili usiwe na njaa na wala usishibe na endelea na mazoezi yako, nina umri kama wako na kilo zilikuwa zinakaribia mia , sasa niko kwa 80 na toka nianze ni miezi kama sita tu, nataka nifike 74, ayo mengine maji ya moto sijui nini vya ziada tu, vyakula ndiyo vya kuzingatia nini unakula, kila la heri mkuu, mwanzo mgumu kaza moyo utaweza
 
Mkuu TRIPLE H Kwa umri wako wa miaka 40 ulitakiwa uwe na uzito usiozidi wa kilo 80 sasa wewe una kilo 118 umezidi kilo38 unatakiwa upunguze hizo kilo 38 ili uwe na afya nzuri. Ukitaka Dawa ya kupunguza kilo kwa kila mwezi utapunguwa kilo 4 dawa ninayo ukitaka Dawa bonyeza hapa.DAWA YA KUPUNGUZA UNENE, MAFUTA, KILO NA TUMBO


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…