Uzoefu: Naishi kwa Shemeji yangu huu mwaka wa tatu

Duh una moyo..
Dada angu kaolewa huko pwani.
Nikienda kumsalimia hata kulala siwezi.
Nafika asubuhi jioni nasepa.

Sina maana mbaya ila KULALA KWA SHEMEJI HAPANA SIWEZI..

#YNWA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nmecheka hatari
 
Hakikisha unampigia na shemeji yako kiwi viatu vyake.
 
4,&6 umenivunja mbavu balaa,miaka ya 2000,wakati nasubili kurudi chuo kupiga shahada baada ya kukaa kitaa mwaka mzima bila kuwa na ishu na ka diploma kangu,nilikaa kwa shemeji,nyumbani kwa Bro mkubwa,wa mbaaali kidogo upande wa umamani,daaa Yule wife wake(shemeji)alikuwa bonge la pisi kali(kipindi hicho)ila alifsnya maisha yangu yawe ya tabu sana,alikuwa na kejeri mbaya hatari,msosi mchana hakuna,nilisimangwa hatari,mpaka na bro akanichukia,nikatimuliwa,nikaenda kukaa zangu ghetto mpaka nilipojiunga na chuo, hiyo nyumba sikukanyaga Tena mpaka tulipokutana msibani huko kwetu Kijijini Mbeya.
 
Hahahahahaha shem ndio tegemezi nyumba zenyewe za kupanga hizi hakuna cha maana zaidi ya vitu vya ndani
Usimvue nguo shemeji yako yeye kakufunika nguo,hapa JF si pa kuanika kila kitu, hata kama kapanga na yeye anapambana kama unavyopambana upate pakutokea.
usikate tamaa jaribu hata kazi za kujishikiza hata kibarua cha kawaida kwa ajili ya mambo yako madogo madogo siyo vema kuomba kila kitu kwa shemu.
 
Hahahaha maisha magumu huleta ubunifu wa roho mbaya, lol kukesha unamkunja kama chapati mtoto wa watu kisa mdogo wake kajaza foleni! Lol lol
 
Miaka mitatu ukishuhudia dadaako analiwa? Unajisikiaje? Au bwashee kaoa wote
 
Umesahau kanuni nyingine...

...Ukiishi kwa shemeji yako hutakiwi kufuga nywele manake sabuni hata ikichukuliwa na panya, utasemwa wewe ndo huwa unamaliza sababu na hiyo minywele yako!
 
Mimi nakaa kwa shangazi tangu nikiwa darasa la sita mpaka sasa nimemaliza diploma 2020 na bado niko kwa shangazi.
ila sio utani hakuna mtu anayependa kukaa kwa watu ila ni mambo flan tuu hayajakaa vizuri, mm natamani hata niondoke leo ila nitaanza vipi.!
 
Ila mtoa mada 😂😂😂 tupo wengi wa namna hiyo
 
Ha ha ha nimecheka sana,mimi sikuwahi kupata fursa ya kukaa kwa shemeji japo siku 2 tu
 
Mkuu mwaka was nne huu Kama ni kid tayari Ana miaka minne. Bado upo kwa shemeji?
 
Sorry to say that but ur stupid! Alafu uko proud kabisa kukaa kwa shemejio miaka mi3? Unasubiri ugali kwa kengele? Mwanaume huyo! Hebu ona aibu kidogo, katafute hata vibarua vya ujenzi huko kwny masaiti kha!
St daddy na st mummy

Hawajui kuchakalika kabisa
 
Mie niligoma kuishi kwa bro kabisa nikazamia mjini kusaka kazi

Mwanaume mpaka nalala mtaroni lkn pakikucha mishe tu leo Mungu kasaidia


Kijana lzm apigane kunikwamua najua kazi zipo nyingi zisizo za rasmi lkn mdogo mdogo unafanikiwa

Ukijifanya Mie Nina elimu kubwa sijui nn utahangaika sana

Piga jobu yeyote ili mradi huharifu Sheria ya jamii
 
Dah nimecheka sanaaaa

Nimecheka mnooo dah sio powaa kukaaa kwa Shemeji
 
Kuna ndugu ukiishi nao hujuti, hata akiwa hayupo unahisi kuna kitu kimepungua, shida ni hawa ndugu mzigo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…