#COVID19 Uzoefu nilioupata katika mapambano ya kupigania uhai dhidi ya maamubikizi ya maradhi ya virusi vya corona Covid-19/ SARS COV2 variant

#COVID19 Uzoefu nilioupata katika mapambano ya kupigania uhai dhidi ya maamubikizi ya maradhi ya virusi vya corona Covid-19/ SARS COV2 variant

Matanga

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2019
Posts
2,281
Reaction score
3,976
Habari zenu ndugu zangu,

Nami nichukue fursa hii kushare japo kwa uchache uzoefu nilioupata katika mapambano ya kupigania uhai dhidi ya maamubikizi ya maradhi ya virusi vya corona Covid-19/ SARS COV2 variant.

Hali yangu kiafya ilianza kuwa dhoofu mnano tarehe 23 January 2021 ambapo nilitoka nyumbani kuelekea ofisini kama kawaida ila hali yangu kimwili haikuwa nzuri maana usiku wa jana yake sikulala vizuri sababu ya uchovu ingawaje ilikuwa weekend.

Nilipofika ofisini nilielekea moja kwa moja katika dispensary yetu na kujisalimisha kwa daktari ambapo nilifanyiwa vipimo kadhaa vikiwemo vya Malaria, FBP, Widal Test, QBC, Urine and Stool tests, Wingi wa Damu, Kiwango cha Sukari, BP n.k. lakini cha ajabu ni baada ya majibu kutoka sikupatikana na shida yoyote katika vipimo vyote. Hivyo daktari aliishia kunishauri nipumzike ninywe maji mengi.

Siku iliyofuata hali iliendelea kuwa mbaya pale ilipofika usiku nilipata homa kali sana na kichwa kuuma sana kwa nyuma huku joto la mwili likipanda balaa. Kwa miaka kadhaa sikuwahi kujifunika blanket japo hali ya hewa ya Arusha ni baridi kiasi. Lakini ilinibidi nimwambie mke wangu anifunike duvet na akaongeza blanket.

Nilipoamka kesho yake nilirudi Hospital na kumueleza dakatari juu ya ile hali na nikamwambia pamoja na vipimo havioneshi maambukizi ya malaria mie nahisi nina malaria hivyo nikamuomba akaniandikia dawa za malaria nikaanza kumeza kwa siku 3. Ikawa kila ikifika alfajiri ninaamka natapika sana nyongo ndio hali itulie na nipate nafuu. Lakini wakati wote nilikuwa naendelea kwenda kazini mchana nashinda vizuri usiku ndio inakuwa balaa.

Katika kipindi chote nilikwishapitia na kuanza kuhisi zile dalili za awali za maambukizi ya virusi vya Covid-19 ambazo kwa hatua ya kwanza ni:
mwili kuchoka, maumivu ya mwili mzima na viungo vyote, kichwa kuuma na kuhisi kizunguzungu pale ninapoamka kutaka kutembea.

Hivyo ilinibidi nianze matibabu ya tiba mbadala kuweza kupambana na hali ile. Nikawa najifukiza mara moja au mbili kwa siku na nilikuwa natumia Eucalyptus Concentrated Oil 50ml nilizonunua Zanzibar State Trade Corporation na nachanganya na Almint ambazo nilinunua toka maduka ya dawa asilia na wakati wa kujifukiza naweka matone 3 mpaka 5 kwenye ndoo ya lita 10 na najifukiza kwa dakika 10 tu.

Pia nikawa nakunywa hiyo almint kwenye maji ya moto. Na kuendeleza herbal cocktails tofauti kama Tangawizi, mdalasini, manjano, malimao. Pia, sikuacha kabisa matumizi ya vimiminika kwa wingi kama natural juices.

Wakati huo huo nilioandikiwa dawa zifuatazo na dakatari Azithromycin 500mg od 6/7 na Junior Asprin 75mg od 7/7 ambazo nilitakiwa kuzitumia kwa siku saba ili kusaidia kuyeyusha damu.

Siku kadhaa zilizofuata ghafla nikajikuta tayari nimeshaingia katika awamu ya pili ya maambukizi ambapo: nikapoteza uwezo wa kunusa na kudetect harufu, nikapoteza uwezo wa kutambua ladha za chakula na vinywaji, pia nikakosa hamu ya kula kabisa, Homa, Kikohozi kikavu ambacho nikikohoa mpaka sehemu ya nyuma ya kichwa inauma.

Ilipofika siku ya Jumapili tarehe 31 January 2021 usiku wa kuamkia tarehe 01 February 2021 hali ilikuwa mbaya sana nikaanza kukohoa sana usiku na kidogo kidogo nikaanza kuhisi kupoteza uwezo wa kupumua. Nilipoamka asubuhi niliomba gari ya ofisi ikanifuata nyumbani na kunipeleka Shree Hindu Mandal Hospital Arusha. Nilifika Hospital saa 4 lakini mpaka namuona Daktari ilikuwa saa 8 maana foleni ya wagonjwa waliokuwa wanasubiri kuonana na Daktari ilikuwa kubwa sana.

Nilipoingia kwa Daktari sikuwa na mambo mengi ya kumweleza zaidi ya kumpa historia fupi ya ugonjwa wangu. Na kumwambia kuwa ninajihisi tayari nimeshapata maambukizi ya Covid-19 na nahitaji kufanya kipimo na kuanza matibabu. Daktari akaniambia niende chumba cha Xray nikapige Chest Xray. Nilipopiga na kumrudishia ile picha Daktari aliniambia picha inaonesha sehemu ya chini ya mapafu yangu tayari ilikuwa imeanza kuathirika sababu ilikuwa na kitu kama ukungu ambao ndio ute ute kama gundi unaohisiwa kutengenezwa na virusi vya Covid-19 ambavyo baadae vinaziba matundu ya hewa. Hivyo akaniandikia mchanganyiko (cocktail) wa dawa kadhaa za Covid-19 ambapo niliandikiwa dawa zifuatazo:
Cetriaxone 1g od 5/7, Gentamycin 160mg od 5/7, Dexamethasone 6mg 5/7, Junior Aspirin 75mg od 10/7, Ibuprofen 400mg 5/7 and Lansoprazole 30mg od 10/7

Pamoja na dawa nilizoandikiwa pia nilipewa sindano za Cefriaxone Injection 1000mg od 5/7 ambazo nilichoma kwa muda wa siku 5 kuanzia Jumatatu tarehe 01 hadi 05 February 2021. Sindano ya kwanza nilichoma Arusha pale pale Shree Hindu Mandal Hospital na zingine 4 zilizobakia nilikuja kumalizia hapa Dar es Salaam Aghakhan Hospital Mbezi Beach. Changamoto niliyokuwa naipata kila baada ya kuchoma hizo sindano za power safe mwili ulikuwa unalegea sana na kupata maumivu makali lakini baada ya muda zinanipa nguvu upya.

Ilipofika Jumatano tarehe 03 February 2021 mara baada ya kuchoma sindano nikaanza kuhisi hali mbali katika upumuaji wangu nikamwaleza daktari ikabidi wanitundikia drip mbili na kunichoma sindano ya Hydrocortisone akaniambia nikanunue Pulse Oxymeter na BP Machine ili niweze kujipima na kumonitor kiwango cha oxygen katika damu yangu na pindi saturation ya oxygen SPO2% ikishuka chini ya asilimia 90 basi inabidi nifanye utaratibu wa kuelekea aidha Rabbininsia Hospital au Aghakhan Hospital kwa ajili ya kuweza kupata kuongezewa oxygen.

Mke wangu alikimbia kwenda Nakiete Pharmacy Mbezi Beach na kununua vifaa hivyo na aliporudi nilipojipima nikakuta oxygen percentage iko kiasi cha 84-89% i.e. below 90% Nilipompigia daktari akaniambia anafanya utaratibu wa kuweza kunipatia mtungi wa oxygen. Lakini haikuwezekana badala yake ilinibidi nianze kupambana na mazoezi ya kuyafanya mapafu yangu yaweze kujiendesha yenyewe bila kutegemea mashine. Niliona video clip moja ikionesha zoezi lililookoa maisha ya wengi huko Marekani kwa kufanya Proning Position Exercise. Nilianza kufanya mazoezi hayo kwa msaada wa mke wangu na kidogo kidogo nikaanza kuona matumaini ya hewa kujaa katika mapafu na kuanza kupumua kwa vizuri kiasi. Nimeendelea na mazoezi mpaka sasa sikuwahi kuwekewa oxygen.

Ilipofika Jumapili tarehe 07 Febraury 2021 niliwasiliana na Daktari baada ya kuwa naendelea kubanwa pumzi wakati wa usiku nae akaniunganisha kwa Daktari aliyekuwa kitengo cha Dharura pale Aghakhan Hospital na kunitaka haraka niende pale hospital. Nilipofika kwa kweli daktari alinipokea kwa bashasha na mwenyewe bila ya kumsubiri muuguzi akanichukua vipimo vya awali alinipima vipimo vyote kisha akaniomba fomu za historia za matibabu niliyoyapata toka nilipoanza kupambana na Covid-19. Akazisoma na kisha akaniingiza katika chumba cha uchunguzi wakanitoa sampuli za damu na kuzipeleka maabara kwa uchunguzi wa CBC, Malaria, Temtin, CPR & Odimer kisha nikachukuliwa kupelekwa Chumba cha Mionzi kwa ajili ya Chest Xray. Huko nako nikakutakana na vijana ambao kwa kweli walikuwa tayari wamejipanga na kuniomba niwaeleze namna ambavyo najisikia ili iwe rahisi kujua aina ya picha watakazohitaji kuzipiga. Haikunichukua dakika 15 tayari nikawa nimepiga picha na majibu yameshamfikia daktari.

Baada ya dakika kadhaa daktari alikuja katika chumba changu akiwa na computer inayoonesha picha ya xray na majibu ya vipimo vya damu. "Alichokisema Daktari ni kuwa kutokana na combination ya picha ya xray na majibu ya vipimo vya damu ni dhahiri kuwa mapafu yangu yameathirika na kuwa nina viral pneumonia ambayo inatoa 90% of suspicious covid-19 infections."

Hivyo Daktari aliniandikia dawa zingine ambazo ni: Vitamin C 1000mg 2/52, Vitacap 1tab 2/52, Azithromicin 500mg, Rivaroxaban10mg 2/52, Paracetamol 1g 2/52, Cefpodoxime 200mg 1/52, Dexamethasone 6mg IM Stat, Dexamethasone 6mg 5/7, Ivermectin 18mg 5/7

Kwa kweli baada ya kupata maelekezo hayo na kuchomwa sindano na kwenda kuchukua dawa basi tukagundua kuwa zile Dexamethasone tablets nilizokuwa nimepewa kule Arusha Shree Hindu Mandal mfamasia alikosea kiwango cha dose badala ya kunipa vidonge 12 vyenye ujazo wa 0.5mg ili kufikia kiwango cha 6mg kilichoandikikwa na Daktari alinipa kipakti chenye vidonge 10 tu vyenye jumla ya 5mg ambazo ni chini ya mahitaji ya dose ya siku moja. Hivyo kwa kipindi chote cha wiki nzima nimekuwa nikinywa 0.5mg kwa siku badala ya 6mg.

Siku moja baada ya kutumia dawa mpya usiku niliolala sikupata changamoto za kupumua kabisa na maumivu ya mwili, viungo na kukohoa usiku hakivunitokea tena. Leo nina siku ya 3 toka nimeanza upya matumizi ya dawa na kweli namshukuru Mwenyezi Mungu naendelea vizuri kwa kweli.

ANGALIZO: Naomba aina za madawa na vidonge nilivyoandika katika waraka huu visitumike bila ushauri na maelekezo ya daktari.

Katika mapambano haya ya siku 21 dhidi ya virusi vya Covid-19 napenda kumshukuru kwa dhati Mwenyezi Mungu Allah SW kwani yeye ndie amenipitisha katika mtihani huu mgumu. Kipekee nimshukuru mke wangu ambaye amekuwa nami kipindi chote cha kuugua kwangu. Siwezi kuwasahau ndugu, jamaa na marafiki kwa mawazo, sala na dua zao.

Shukrani nyingi ziwaendee madaktari wafuatao waliochukua hatua za kupambania hali yangu ya kiafya: Dr. Hamad K. Said - Shree Hindu Mandal Arusha, Dr. Vedasto Florian - Bank of Tanzania, Dr. Chuwa - Aghakhan Hospital na Dr. Kilalo, M - Emergency Physician Aghakhan Hospital na Dr. Mazna - Aghakhan Hospital Mbezi Beach.

Ni mimi ndugu yenu.


Abdul Aziz Mbaruk
Muathirika wa Maambukizi ya Virusi vya Covid-19
Mob: +255 796 584386

10 Februari 2021
 
Kwa Mizunguko yote hiyo na ukilinganisha na vipato (uchumi) wa mtanzania, ni wachache sana wanaweza kuchomoka! Mungu atupganie tu, vingnevyo yale yale ya mizoga (miili ya wafu) kutapakaa kila mahali lazima yatokee!
 
Mkuu kwenye vipimo vya mavi (stool test) majibu yalitokaje?
 
Kwa Mizunguko yote hiyo na ukilinganisha na vipato (uchumi) wa mtanzania, ni wachache sana wanaweza kuchomoka! Mungu atupganie tu, vingnevyo yale yale ya mizoga (miili ya wafu) kutapakaa kila mahali lazima yatokee!
Kwani kuna ulazima wa kufata iyo mizunguko alopitia yeye?
 
Dogo wee mwenyewe unaishi kwa shemeji yako. Ungekuwa serious wewe kwanza kwa kujituma kufanya kazi na kujitegemea.
Jaribu kuwa serious kwenye mambo serious.

Ni sentence ndogo inayotumia asilimia chache ya brain cells kuilewa.
 
Mpumbavu ni yule anaewambia watu huu ugonjwa haupo pamoja na wale wote wanaomsujudia ukiwamo wewe.
Umeona wanaume wanatoa solution si wapuuzi nyie kuelezea matatizo tu. Usiharibu uzi wa muungwana.

Swali langu kwa Mwanzisha uzi: je hakuna aliekueleza utumie colchicine?
 
Back
Top Bottom