#COVID19 Uzoefu nilioupata katika mapambano ya kupigania uhai dhidi ya maamubikizi ya maradhi ya virusi vya corona Covid-19/ SARS COV2 variant

Asante sana kwa kushea uzoefu huu muhimu! Kaka yangu alikuwa anatibiwa Covid-19 huku hali ikizidi kuwa mbaya mtoto wake ambaye ni daktari akaingilia kati na kugundua ni viral neumonia akabadilisha dawa. Leo kaka ni mzima wa afya. Madaktari wetu wanatibu kwa mazoea tuwe makini!
 
Kabisa aisee tuwe makini sana na afya zetu
 
Pole Sana mkuu kumbe umepitia changamoto hii pia?
Yap na kama isingelikuwa madaktari wa hospitali ya mkoa mmoja sasa hivi angelikuwa na wadhifa tofauti. Nisingelikuwa na mke. Kitu nilichojifunza ni kuwa wengi wanaokufa ni wale wanaoumwa na kuzembea. Yeye anajiogopa kwa kukisia ni malaria tu kumbe ni ponjongoro ishaingia. Hawa wafuasi wa Tototundu wanadhani hii ponjongoro inaua siku mbili tu. La hasha inaanza taratibu na inachukua si chini ya siku 10. Ubovu ni kuwa akizidiwa hapo anapelekwa hospitali na kesho yake anakatika.

Ni vyema tukawa tunapashana habari si tu kushadidia vifo bali jinsi ya kujiokoa kama wewe ulivyofanya. Usisahau tunaambiwa watu 103 million washaambukizwa ni 2.3 million wametutoka hapa duniani. Hii ina maana ukiipata hii ngwangule possibility ya kufa ni 0.02. Hivyo ukiupata ni kuchakarika ili kuokoa maisha yako maana probability ya kupona ni asilimia 99.8
 
Kwani Covid inapimwa mavi??[emoji44][emoji44]
Ukiumwa hata kama dalili ni za ugojwa wa corona lakini dr anaweza kuona umuhimu wa kukuandikia vipimo vingine ili ku-rule out matatizo mengine au kuchunguza kitu chochote wanachoona kinafaa.
 
Ukiumwa hata kama dalili ni za ugojwa wa corona lakini dr anaweza kuona umuhimu wa kukuandikia vipimo vingine ili ku-rule out matatizo mengine au kuchunguza kitu chochote wanachoona kinafaa.
Shida Vijana wanaamini kipimo kipya cha kichina kuwa unaingizwa inchi kadhaa sehemu ya hajakubwa
 
Tafadhali eleza ulivyopona ili tuchukue notes
Corona kila mtu anaugua kwa namna yake. Kuna wanaopoteza uwezo wa kunusa tu na hawana dalili nyingine yoyote na hawatumii dawa yoyote na wanapona. Huyo jamaa inawezekena kabisa hakutumia chochote. Watu wengi walio chini ya miaka 30 na hawana matatizo mengine mara nyingi hawatumii dawa na dalili zake zinakuwa siyo kali. Kitu kingine ambacho nime-note kinachangia ni ''how active someone is''. Kwa watu wanaokaa ofisini tu na hawafanyi mazoezi au kazi nzito pia ni hatari. Watu kama wabeba zege, makuli na watu wa kazi za shuruba hata wakiugua hawazidiwi sana.
 
Tafadhali eleza ulivyopona ili tuchukue notes
Nashukuru Mungu ni kama imeisha yenyewe tu maana siwez sema nimekunywa sana ile mix ya limao na tangawiz,nilikua nakunywa asubuhi na jion, pia ilinikuta nafanya mazoezi kila alfariji nilisimama tu wakat naumwa maana ni heavy ukitembea kidogo tu hoi. Nilikua nakunywa paracetamol kichwa kutuliza kichwa japo hazikua zinanisaidia sana. Mungu ni mwema sana si unaona kuna wengine inawasumbua kiasi cha kuwapelekea kutumia gharama kubwa na hata pengine hawaponi pia.
 
Pole sana umetueleza jinsi ulivyotumia dawa zote hizo na umesema ukifanya mazoezi hali ya upumuaji wako ikawa vizuri sema wazi ni mazoezi au hizo dawa zilikusaidia?
Huwo mlolongo wote ningekuwa mimi ningekuwa nishajifia zangu maana nahisi haipungui 5M+ mimi ningemwambia bimkubwa ninyonge nikafaidi wanawake 75 peponi.
 
Dawa ulizoorothesha watu wasinakili na kuanza kumeza kama chakula!! Natoa ushauri kwamba dawa yoyote zingatia ushauri wa daktari.
 
Hivyo Daktari aliniandikia dawa zingine ambazo ni: Vitamin C 1000mg 2/52, Vitacap 1tab 2/52, Azithromicin 500mg, Rivaroxaban10mg 2/52, Paracetamol 1g 2/52, Cefpodoxime 200mg 1/52, Dexamethasone 6mg IM Stat, Dexamethasone 6mg 5/7, Ivermectin 18mg 5/7
Vipi usalama wa ini mana naona ni sumu ningi sana hii
 
Huwo mlolongo wote ningekuwa mimi ningekuwa nishajifia zangu maana nahisi haipungui 5M+ mimi ningemwambia bimkubwa ninyonge nikafaidi wanawake 75 peponi.
Huna aibu utani una mahala pake yaan kuna watu ilibidi mbaki Facebook tu ndio Hadhi yetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…