Tony Laurent
JF-Expert Member
- Jan 5, 2011
- 5,606
- 7,032
Kuhusu Hii thread- Credit zote ziende kwa mwamba Joel Nanauka. Nimeichukua kama ilivyo kutoka kwenye akaunti yake ya Twitter @jnanauka- hili jina jipya la Twitter la X linanitatiza sana silipendi.
Twende sasa moja kwa moja kwenye mada yetu ya niliyocopy and na kupaste.
HEKIMA 7 ZA UONGOZI NILIZOJIFUNZA MWAKA 2024
1. Kila unachokipigania kwa KUFA na KUPONA, kinaweza KUMUONDOA mwingine au KUKUONDOA wewe.Wakati mwingine anayeshinda sio yule mwenye NGUVU bali ni suala la “TIMING” tu. Unaweza kumuondoa mwingine ila kabla wewe HAUJAKIPATA ukaondoka pia.
2. Wengi wanaokosoa kwa HASIRA bila kusema MBADALA, ni kwa sababu wanahisi wamekosa FURSA, wapo ambao wakipewa watakuwa kama wanaowakosoa.
3. Nafasi unayoitaka kwa kumuamini MUNGU, kuna mwingine anaitaka au kuendelea kuwa nayo pia kwa kuamini ATAFANYA LOLOTE linalowezekana.
4. Njia rahisi ya kujua kiongozi aliyepoteza UWEZO wake ni VITISHOkwa wenzake na kuhakikisha ANAWANYANG’ANYA kila walichonacho hata kile WANACHOSTAHILI.
5. Mtu anayepata NAFASI bila kuwa na UWEZO, ni rahisi kupoteza hiyo nafasi kwa kutumia muda mwingi KUWASHAMBULIA wenye uwezo na kujizungushia na WASIO
NA UWEZO.
6. Wapo WATAKAOKUSAPOTI wakiona unakaribia KUSHINDA, mwanzoni hautawaona. Wapo watakaokupinga kwa sababu WANAJUA utashinda na kwa sababu ya waliyokufanyia wanajua haitawezekana kwao kuwa KARIBU na wewe.
7. Wapo wenye NAFASI wanaoweza kukusaidia na ULITARAJIA wakusaidie, ila wanakutana na VIPINGAMIZI wasivyoweza KUVIWEKA WAZI vinavyowafanya WASHINDWE kukusaidia. Nawe ukifika hizo level utaelewa.
See You At The Top