Uzoefu wa matumizi ya gesi kwenye gari

Uzoefu wa matumizi ya gesi kwenye gari

Wajuzi wa mambo hapa naomba msaada wenu wa uzoefu, ninataka kufunga mfumo wa gesi kwenye TOYOTA - IST.

Naomba kujua nitegemee kupata shida gani kwenye hiyo gari mi nachojua ni kuwa nita-save matumizi ya mafuta, naomba mnipe tahadhari ili nijue kama niendelee na huu mchakato au niachane nao maana hasara ikiwa kubwa kuliko faida ni shida
Ulivyofanya uchunguzi uliambiwa ukiweka ges inakulaje na petrol inakulaje,isije ikawa tofauti yake ni ndogo sana kwani nasikia hivyo vigari ni vinanusaga balaa
 
Matumizi ya Gesi kwa modification za Bongo lazima uharibu gari
Unafahamu chochote kuhusu ufungwaji wa gesi kwenye magari na taasisi (wataalamu) zinazofunga hiyo mifumo hapa Tz? Hebu fanya ka utafiti kidogo. Hebu pita DIT upate maarifa. Otherwise, pita YouTube uwasikie wataalamu kutoka DIT wakifafanua kuhusu hili.
 
Back
Top Bottom