The Good
Senior Member
- May 26, 2010
- 185
- 119
Leo nimebahatika kupata chanjo katika kituo cha jirani. Vitu viwili ambavyo nimeviona na nadhani kuna haja ya wahusika kuvifanyia kazi ni hivi
1. Booking
Jana nilifanya on-line booking na kuweka tarehe ya leo katika kituo nilichochagua
Nilipofika kituoni nikakuta hawana taarifa yoyote ya on-line booking na kila kitu unaanza upya.
Ni vizuri wahusika wakaliangalia hili maana huko tuendako iwapo watu watajitokeza kwa wingi kutakuwa na ucheleweshaji mkubwa kwa watu kujaza taarifa zao upya
2. Cheti
Cheti kinachotolewa hakina ubora kabisa. Nilitegemea kwa kuwa nilifanya on-line booking basi taarifa ningeziona na baada ya chanjo ningepata electronic certificate chenye barcode ambayo itamwezesha mtu yoyote kuhakiki uhalisia wa cheti pindi kitakapohitajika
Kwa cheti hiki ambacho hakina security feature yoyote very soon kila mtu atakuwa nacho na tatizo litakuwa kwa watanzania watakaokuwa wanasafiri kwenda nchi zinazohitaji ushahidi wa chanjo
Cheti chetu nina mashaka hakitakuwa kinatambulika
Naomba haya mawili wahusika wayafanyie kazi ili kuongeza ubora wa huduma na kuifanya kuwa inayotambulika kimataifa