Uzoefu wangu wa msikiti chuoni Uskochi na Hamza Rijal

Uzoefu wangu wa msikiti chuoni Uskochi na Hamza Rijal

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
1547753960306.png

Castle
Ikiwa nafanya kazi na Zanzibar Integrated Land and Environmental Management (ZILEM) ndani ya Commission of Lands and Environment (COLE) tukifadhiliwa na Finish International Development Agency (FINIDA), Idara zilizokuwemo ndani ya Programu hiyo ilikuwa Department of Land and Registration, Department of Survey and Mapping na Department of Environment.

Alikuja Primatologist kutoka University of Florida akasewa mie niwe Field Assistance wake katika kazi zake za Conservation of Red Colobus Monkey, akavutiwa na utendaji wangu wa kazi aka suggest nifanye Special Masters Program ya Wildlife inayofundishwa University of Florida kwa miaka 3, wakati huo huo Gent University ipo Belgium wame ni offer Masters Program ya 2 years ya Environment and Sanitation huku nimeomba Master Program ya Agriculture juu ya kilimo katika aerable land Huko Hebrew University. Sasa hamu yangu ilikuwa nende USA au Israel, kwa USA niliona vacation nitajitupa kwa brother itakuwa mteremko kwa Israel ndoto zangu siku zote ilikuwa nende Hijja kisha nende nikazuru Baitul Muqadas na nikaione Taj Mahal.

Kikao cha Kamati Tendaji/Executive Committee kikaja na maamuzi yafwatayo, USA nisende kwani gharama za Masters zinasomesha watu 3 UK, Gent mie sio line yangu kuna mtu kafanya Chemistry hio itakuwa appropriate na Hebrew University ni ya Kilimo kwa hiyo nitafute University za UK ndio nikaangukia Aberdeen University huku Hebrew University familia akishika bendera dada yangu akipinga hilo anasema kuwa roho zao zitakuwa juu juu.

Nikapata Admission ya kufanya Masters Degree in Ecology, nilipofika katika darasa letu tulikuwa watu 11, nilikuwa mie kutoka Tanzania, Malaysia mmoja, kutoka Thailand mmoja na mmoja kutoka Ecuador sisi wageni na Waiengereza wenyewe 7. Kijana kutoka Malaysia kuniona Muislamu akafurahi sana siku ya pili akanipa time table ya Sala akanionyesha Msala ambao upo karibu na Chuo tukisali Ijumaa na sala zote. Ilipofika Summer ikabidi tubadilishwe makazi nikahamia kwenye flats nyengine sio zile ambazo tukikaa mwanzo. Nikikaa flat hiyo na kijana kutoka Greek, Zambia na Gambia. Jamaa wa Ki-Gambia akiweka Afro huyu mie nikidhani ni Mkristo kmbe na yeye akidhani mie kutoka Rwanda kwa hiyo siyo Muislamu. Siku hio ilikuwa joto sana nikamuona kishasali Magharibi anavuta uradi, nikastaajabu sana. Sasa na yeye siku hiyo akanikuta na tawadha kwenda kusali, akastaaajabu sana, basi kwenye mazungumzo kila mmoja akamuelezea mwenzake alivyokuwa akimdhania mwenzie.

Ingekuwa naandika kitabu huo wote ni utangulizi ninalotaka kuliesema ni hili.

Kuna jumba kama castle limewekewa vyumba kwa deparments mbalimbali kama wana activities zao watapewa sehemu watumie. Vijana wa Ki-Malaysia wako wakakamavu wakenda kuomba wapewe chumba cha kusalia kwani Msala ambao tunaosalia ni Waislamu wengi tunakuwa tunabanana na wengine wanasali mpaka kwenye hodhi yaani pakutawadhia.

Sikiliza, mkubwa wa Department ya Theology alivyowauliza, huo msala upo wapi? Akafahamishwa, akasema mtatuhakishia vipi kama mtautumia kama inavyotakiwa, akapewa assurance, akasema mtapata jawabu bada ya wiki 2, baada ya wiki 2 kupita wakakabidhiwa jamaa tuwe tunasali, ikawa sahal kwani wanafunzi wengi wakawa wanasali hapo tulipopewa na kule kwa awali kwenye Msala wakawa zaidi ni wafanyakazi na watu wanaoishi katika maeneo ya karibu.

Shabash, Wakiristo ikdi ikawaingia na wao wakenda kuomba wapewe chumba cha kufanya Ibada tena kwa Jumapili. Yule head wa Dept ya Theology akawambia kwani mupo wangapi? Aidha akawambia kuna Kanisa la Catholic na Protestant hata asilimia 10 ya waumini hawafiki kutokana na ukubwa wa hayo makanisa.

Mmoja akasema mbona Waislamu mumewapa sehemu ya kuabudia? Hapa ndipo patamu

Aliwambia Waislamu walikuja kuomba kupatiwa pahali pakufanyia ibada na wao wanasali mara 5 kwa siku, mie nilifaya uchunguzi wangu kwanza nikaona siku ya Ijumaa kwenye Msala wanajaa na hichi chumba tulichowapa kinajaa, sio hilo kila nyakati za sala wanakuwepo wanasali wanaume na wanawake na wanapeyana mafunzo ya dini yao. Akawambia mkinihakikishia mtakuwa kama Waislamu basi kesho nitakupeni, lakini mkishindwa nitakung’anyeni. Mmoja wao akasema hatuwawezi Waislamu wameshikamana na dini yao hata wapo nje ya nchi zao.

Mzungu tena Ulaya tena mwana taaluma ya dini kafahamu umuhimu wa kufanya ibada na aawaelewa Waislamu na kawapatia pakufanya ibada, leo inasikitisha hayo yaliopo Dodoma mtu anayeitwa Professor anacheza ugoma aioujuwa unaopigwa kutoka Washington DC. Waislamu hawana fujo, lakini wanawekwa kwenye uwonevu ambao utakuja kuwa na madhara huko mbele.

Mwenye kuonewa anatabu mmoja nayo kukubali kuonewa na kuvumilia lakini kuna wakati atakuja kusema na liwe litalokuwa, wakati huo huo haunsimile na sio wakati wa mzaha, ninawausia jamaa wa Kikristo kuamini kuwa Waislamu sio maadui, Muislamu wakweli haui mtu hafanyi ugaidi kwani mafundisho katika Qur’an hayamuongozi kwenda huko. Lebanon imeraruka kutokana na ubaguzi na ugozi ulitopea kutengwa kwa Waislamu. Tanzania ilivyokuwa kisiwa cha amani, kwahio tusikichafue.
 
Seat ya mbele nasubiri material zaidi

"ᴬᵐᵇⁱᵗⁱᵒⁿ ᶜᵃⁿ ᵇᵉ ᵃ ᵛⁱʳᵗᵘᵉ ʷʰᵉⁿ ⁱᵗ ᵈʳⁱᵛᵉˢ ᵘˢ ᵗᵒ ᵉˣᶜᵉˡˡ"
 
nimekuwa watatu kuusoma uzi wote...tena asubuhi
 
Mzee said udini umekufanya uzeeke mapema.
Wazanzibari wenzio wanatumia fursa kula ndani JMT we unakonda sababu ya udini

Angalia mzee hadi nuru umepoteza
Sababu ya kumchukia nyerere ambaye hayupo duniani
Aibu sana kwa mzee kama wewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shekhe Muhammed said ... Naomba hostoria ya taj mahal na sehem ulizotaja ukasema unatamani ungefka Hapo Baytul maqdis
 
Asante Maalim Mohammed Said, kwa simulizi murua baada ya mapumziko ya kumbukumbu ya Muungano wetu adhimu uliasisiwa na Nyerere na Karume, kufuatia yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya January 1964.
P
 
Mzungu tena Ulaya tena mwana taaluma ya dini kafahamu umuhimu wa kufanya ibada na aawaelewa Waislamu na kawapatia pakufanya ibada, leo inasikitisha hayo yaliopo Dodoma mtu anayeitwa Professor anacheza ugoma aioujuwa unaopigwa kutoka Washington DC. Waislamu hawana fujo, lakini wanawekwa kwenye uwonevu ambao utakuja kuwa na madhara huko mbele.

Mwenye kuonewa anatabu mmoja nayo kukubali kuonewa na kuvumilia lakini kuna wakati atakuja kusema na liwe litalokuwa, kutokana na ubaguzi na ugozi ulitopea kutengwa kwa Waislamu.
Nimeipenda hii the motive behind.
Yaani mzungu anawaelewa Waislamu na kuwapatia mahali pa kufanya ibada tena ulaya ambako Ukrustu umetamalaki, halafu hapa Tanzania ambapo Waislamu ni wengi zaidi ya Wakristo, mtu anyimwe pa kuswalia?. This is impossible. Tuelezee zaidi Dodoma kumetokea nini?, naamini sio lile tukio la Kondoa, yule mama inambidi apumzishwe tuu.
P
 
Asante Maalim Mohammed Said, kwa simulizi murua baada ya mapumziko ya kumbukumbu ya Muungano wetu adhimu uliasisiwa na Nyerere na Karume, kufuatia yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya January 1964.
P
Muungano uadhimu wake umetokea wapi?
 
Muungano uadhimu wake umetokea wapi?
Ndoa ni jambo adhimu, nchi mbili kuungana na kuwa nchi moja, hili sio jambo dogo, ni jambo adhimu.

Si wengi mnatambua kuwa Muungano ndio siku muhimu kuliko hata siku ya uhuru.

P
 
Back
Top Bottom