World Logistics Company
Member
- Jun 1, 2021
- 99
- 104
Wadau wa Biashara na Ujasiriamali,
Tumeona humu kuna wazoefu wa biashara hizi za mazao ya kilimo, bila shaka ni sahihi kuleta jambo hili kwenu ili tubadilishane uzoefu.
Pichani ni mzigo wa nafaka za mahindi uliagizwa na mteja wetu wiki kadhaa zilizopita. Mzigo huu ulitokea nchini India na tukausafirisha hadi mkoani Arusha kwenye kiwanda (jina limehifadhiwa) kikubwa tu.
Je, ni bidhaa gani nyingine huagizwa kwa wingi kutoka India? Ni kwanini baadhi ya wafanyabiashara wanaagiza mazao ya kilimo nje licha ya kufahamika kuwa hapa nchini pia zinazalishwa nafaka kwa wingi?
Sisi kama wadau wa usafirishaji, tuna utayari wa kusafirisha pia bidhaa zinazotokea nchini kwenda nje ya nchi ili kukuza soko la bidhaa zetu. Kama hapa kuna wadau wanaofanya biashara ya kutuma mizigo nje ya nchi, nao tungependa kupata maoni yao.