Uzuri wa kiatu hiki uko wap?

Mambo ya Gen Z hayo.

Kuna siku dogo wa kike alivaa liyebo la ajabu, kubwa afu lina mamipira mengi hata sehemu ya kutumbikiza mguu haionekani ila yeye alikua analipenda balaa.
Gen Z hao, fashion zao utaumiza kichwa bure
 
Leo tu Church kuna kijana kaja kavaa hilo likiatu na suruali ya jeans pana chini halafu juu kavaa sweta kubwa sana la round na kwa ndan kavaa shati la kola so kola kaiweka vizuri shingoni halafu sweta limechomekewa. Aisee yule kijana amekua kama model maana watu wamemwangalia sana na yeye hakuwa na habari na mtu kashika biblia yake na kitabu cha nyimbo safi kabisa
 
Du!aisee hata kanisani kumbe wapo😳😳
 
Nimechekaaa had baas, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mkuu we uzito ulijuaje bila kuvaa mzee wetu???πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Mkuu we uzito ulijuaje bila kuvaa mzee wetu???πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Bahati nzuri nikiwa nasoma hii mada hapa Morogoro nilipitia pale mzunguko karibu na crdb kuna vijana wanauza, nikajiridhisha.
 
Bahati nzuri nikiwa nasoma hii mada hapa Morogoro nilipitia pale mzunguko karibu na crdb kuna vijana wanauza, nikajiridhisha.
Uliwezaje mkuu maana lile likiatu mi nikilitazama tu naliogopa
 
Kama kijana akivaa,binafsi sioni tatizo coz kila zama na kitabu chake,
Ila akivaa mkongwe ndio nitashangaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…