Uchaguzi 2020 Uzuri wa kura ya siri

Kura yangu nampa Lisu,za magufuli zitapelea.
Kura yako ni siri yako....unaweza kusema hadharani kuwa utampigia Lisu lkn ukiingia ktk chumba cha kupigia ukiwa peke yako unaweza mpigia Magufuli bila hata Lisu kujua na bado maisha na urafiki ukaendelea kama kawaida.
 
Sisi Watanzania tuliowengi tutamchagua Rais Magufuli kipenzi cha Watanzania

Yule mropokaji na msaliti wa Nchi Lissu atapigiwa kura na robert tu
 
hakikisha unapiga kura yako kwa usahihi.
1.piga Kura kwa mtu mmoja tu.
2. weka alama ya tiki/vyema ktk kiboksi kimoja tu

3. hakikisha alama yako ya tiki isitoke nje ya mstari wa kiboksi.

4. usiweke alama nyingine yoyote ktk karatasi ya kupigia kura.

5. usiandike jina lako wala namaba yako ya simu, usiandike chochote zaidi ya alama ya tiki.
KURA YAKO NI SIRI YAKO MWENYEWE

6. hakikisha karatasi yako ya kupigia kura imepigwa muhuri wa tume
 
Na kinyume chake pia ni sahihi. Kwahiyo unaweza kuwa mwanaCCM kindakindaki na bado ukampa TAL kura yako
 
Sisi Watanzania tuliowengi tutamchagua Rais Magufuli kipenzi cha Watanzania

Yule mropokaji na msaliti wa Nchi Lissu atapigiwa kura na robert tu
Robert A hajaandikishwa kuwa mpiga kura kwani hana vigezo! sasa wewe unaanzaje kusema uongo? TAL atapigiwa kura na wananchi watanzania wanao-ukataa Udanganyika
 
Kura ni siri yako mchague kiongozi unaye amini atatatua kero ktk jimbo lako.
fanya maamuzi sahihi trh 28
 
Kura ni kwa JPM
mambo ya siri yashapitwa na wakati.sasa ni zama za uwazi na ukweli.
 
Hata tukiambizana ukweli bado kura ni siri yako, hata wagombea hawajui nini anacho fikiria mpiga kura mpaka pale matokeo yatakapo toka.

Huo ndio uzuri wa kura ya siri inakupa nafasi ya mwisho ya kidemokrasia wewe mpiga kura kutimiza wajibu/haki yako ya kikatiba ya kumchagua kiongozi unaye mtaka.
 
Kura ni siri yako, nenda kapige kura yako bila wasiwasi wala hofu, kuwa huru kumchagua kiongozi ambaye umemsikiliza sera zake na kumuelewa.

Hii ndio demokrasia tuliyo nayo watanzania kila baada ya miaka 5 tunamchagua kiongozi tunaye mtaka.
 
NEC watoe fomu za matokeo ili waepuke kupewa kesi ya wizi kwa kukusudia maana haiingii akilini ufanye uchaguzi alafu ugome kutoe fomu ya matokeo ya kusithibitisha hata ushindi bila kuweka matokeo wazi hapo utakuwa unajitakia kesi ya wizi kwa kukusudia.
 
Ondoa shaka mwaka huu NEC imejipanga kufanya uchaguzi wa viwango vya hali ya juu,
kwanza wametuhakikishia vifaa vyote vya kupigia kura vitafika vituoni kwa wakati, kila kitu kitakuwa wazi na haki,
ondoweni wasiwasi.
ila dosari ndogondogo za kibanaadam huwa hazikosekani, hata ktk uchaguzi wa Marekani haukosi dosari....sembuse sisi
 
ndio uzuri wa demokrasia ya kupiga kura ya siri, unachagua kitu roho inapenda bila wasiwasi
 
kura ya siri haina unafiki sio kama kura ya wazi.
kesho mapema wazee, vijana, wadada na kina mama shime tudamke asubuhi mapema tukatimize ndoto zetu.
 
Wanaccm tutalinda kura za magufuli ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…