Wiki ijayo tarehe 28/10 watanzania wote tunaenda kupiga kura kuchagua Rais, wabunge na madiwani
Jambo moja ambalo kila mmoja anapaswa alitambue ni kwamba kura yako ni siri yako.
Maana yake ni kwamba unaweza kuwa unampenda sana au ni rafiki wa karibu na Lissu lakini bado unaweza kumpigia kura yako Magufuli na wakati huo huo Lissu hawezi kujua kama umempigia kura Magufuli. Unaweza kufanya hivyo na bado urafiki wenu na Lissu ukaendelea bila hata matatizo unaweza kunywa nae hata chai, unaweza hata kumdanganya kuwa nimekupigia kura wewe na ukamshangilia na asijue, huo ndio uzuri wa kura ya siri.
Kura ya siri haina uadui wala ugomvi mpigie kura unayemuamini na urafiki wenu/wako bado utaendelea baada ya uchaguzi.
Kuna uwezekano mkubwa tarehe 28/10 Lissu akampigia kura Magufuli.
KURA NI SIRI YAKO