Uzushi/upotoshaji kuhusu ujasiriamali

The List

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2017
Posts
1,732
Reaction score
4,924
Wasalaam wakuu,

Ujasiriamali kwa miaka ya hivi karibuni imekuwa ni jambo linalohubiriwa sana. Watu wa kada mbalimbali wamelisemea kama jambo la kher, na matokeo yake mwitikio kutoka kwa watu mbalimbali umeonekana kwa kuthubutu, kubuni na kuanzisha miradi kwa lengo la kujiajiri. Sio hivyo tu hata baadhi ya waajiriwa wamethubutu kuacha kazi na kujiingiza ktk ujasiriamali.

Uanzishwaji wa shule, makongamano, maonyesho, mashindano na pia kuibuka kwa wahasimashaji wa masuala ya wajasiriamali ni kiashirio cha umaarufu wa dhana hii.

Shuhuda za watu mbalimbali waliopata mafanikio kwa uthubutu wao ktk ujasiriamali imekuwa pia kichocheo kikubwa cha watu wengi kujiingiza ktk ujasiriamali.

Pamoja na mafanikio hayo, upande wa pili kuna kundi kubwa la watu linalolaani ujasiriamali. Kundi hili ni la watu 'waliotendwa' na ujasiriamali.

Na kwa ukweli usiopingika kundi hili ni kubwa kuliko la wale waliofanikiwa. Wengine ni walioacha kazi za kuajiriwa na kwa sasa wanatamani tena kurudi uko, wengine ni wanafunzi walioacha vyuo na kufikri wao pia wanaweza kuwa the next Zuckerback, Bill Gates marehem Steve Jobs na wengineo.

Kundi hili kubwa linalolaani kuhusu ujasiriamali ni kundi liliochagua ujasiriamali aidha kwa kupotoshwa au kuwa na mategemeo makubwa kuliko uhalisia.

Huu binafsi nauiita upotoshaji/uzushi amabao watu wengi humezeshwa kuhusu ujasiriamali na wakiingia uko na kukuta matokeo tofauti basi hubaki ktk simanzi.

Apa nitakupata THE LIST ya uzushi/upotoshaji kuhusu ujasiriamali ambao watu wengi huwaacha ktk simanzi.

Mosi, utajiri/pesa, nafikiri hii inaweza kuwa sababu kubwa. Watu wengi huingia kwenye ujasiriamali kwa mahesab au makadirio makubwa. Mtu anapiga hesab nikiweza kulima tikiti kwa miez mitatu ni milionea au nikiwa na laki5 nikifuga kuku ndani ya miez 6 nitakuwa multimillionair. Ujasiriamali una hela, tena nzuri lakini kama kipaumbele chako ni pesa tu nafikir unahitaj kufikir marambili. Facebook ilikaa miaka 7 kabla haijaanza kuleta faida, yaani kwa miaka saba hao jamaa pesa ilikuwa inawatoka bila return yoyote. Na kama ulikuwa hujui Kampuni ya Amazon mpaka leo haijaweza kuleta r'eal revenue' zaid ya 'operating cost.'

Uhuru. Mwanadamu ni kiumbe anaependa uhuru na huwa mnyonge pale anapoukosa. Iwe ni kwenye maisha ya binafsi au ya kuajiriwa mwanadamu hupenda kuwa huru. Watu wengi huhisi kubanwa na waajiri wao na hivyo kuwanyima uhuru na hivyo huamua ku'opt' ujasiriamali kwa imani watakuwa huru. Iko hivi kama unaona kufanya kazi masaa 8 au 9 unabanwa basi tambua hufai kuwa mjasiriamali. Kwa takwimu tu 'an average entrepreneur hufanya kazi kwa zaidi ya masaa 16-18 kwa siku'.

Umaarufu, hii pia ni kichocheo kikubwa cha watu kuchagua ujasiriamali. Ukweli usiopingika ni kwamba sote tunawafahamu watu kama Tai lopez, Vusi Thembekwayo, Ellon Musk n.k kwa mafanikio yao ktk ujasiriamali. Ni sababu nzuri lakini unahitaji uwe na sabab kubwa zaid kuliko umaarufu tu, Warren Buffet ilimchukua miaka zaid 15 kuwa recognised kama ceedible investor.

Kumbuka kati ya biashara 10 zinazoanzishwa kila mwaka ni 3 tu hufika mwaka wa tatu. Na pia kwa biashara zaid ya 100 zinazoanzishwa kila mwaka ni asilimia moja tu ya biashara hizo humaliza mwaka.

Unahitaji kuwa na sababu/motive nzito za kuchagua ujasiriamali zaid ya hizo tajwa apo juu kama unataka kuwa mjasiriamali mwenye mafanikio endelevu, zaidi ya hapo baki shule au kwenye kibarua chako.

 
Vizuri Mkuu.
Nimejifunza Kitu.
 
Kufanya biashara, kujiajiri ni kipaja ambacho wengi wetu tunadhani tunacho....ukweli ni kwamba sio kitu ambacho ni rahisi kama watu wanavyofikiri
 
Hata kama kuna ukweli kiasi lakini kufeli ktk ujasiliamali ni sawa na huko kuajiliwa then ukafukuzwa kazi au mkataba wa ajira ukaisha,zote hizo ni moja ya kitu tunaita MAISHA,so kusema ujasiliamali ni uzushi si kweli,kuna wajasiliamali pia wanaosema kuajiliwa ni kushikiwa akili na kupoteza muda wa kupata zaidi,na ndivyo ilivyo.we ungesema kua kuajiliwa na ujasiliamali vyote vina changamoto zake maana ni utafutaji uleule..ila yote kwa yote hata mimi hapa hunirudishi tena kwenye kuajiliwa.

JAH RASTAFARI MORNING AFRICA
 
Tatizo letu tunashindwa kutambua changamoto katika kila jambo hvyo ulivyovisema vyote ni changamoto ambavyo sisi tuliobobea tunasema ndo ujasiliamali wenyewe sisi wajasilia mali autumnalii au kuamini katika success we always believe in failure that's why we already apply different tactics ili tusurvive
Nakubaliana na wew kwenye suala la muda coz ujasiliamali ni devoting time and energy coz mimi nafungua duka 12:00 asubuhi nafunga saa 5:00 au 6:00 usiku

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kufanya biashara, kujiajiri ni kipaja ambacho wengi wetu tunadhani tunacho....ukweli ni kwamba sio kitu ambacho ni rahisi kama watu wanavyofikiri
Mkuu Shangani uko sahihi ujasiriaamli sio kwa kila mtu lakini kila mwenye nia anaweza
 

Mkuu G'taxi umeni qoute vibaya sijasema ujasiriamali Ni UZUSHI bali hoja zangu zimezungumzia UZUSHI/UPOTOSHAJI unaohusishwa na dhana nzima ya Ujasiriamali

Na ninafikiri nitakuwa mtu wa mwisho kupinga Ujasiriamali. Infact nakupa pongezi kuachana na maisha ya kushikiwa akili na kuthubutu kuwa boss wa maisha yako.
 
Lazima uwe na passion ili ufanikiwe,watu wengi wanafanya kwa mkumbo ni wachache wanaofanya kwa maridhio ya nafsi zao.

Mimi nimeshaanzisha biashara 10,nane zimekufa,mbili ziko hai..na bado naendelea kufungua nyingine.kumbuka nimeajiri watu kadhaa kwahiyo naisaidia jamii yangu.

Ila kuajiliwa nahisi inabidi uwe na roho ngumu zaidi
 
Nitakuja kwa kina ngoja kwanza niendelee kusoma mawazo ya watu,maana kam niliweza kuwekeza 8000(elfu nane)na nikaitii na kufanikiwa hata ukinipa kazi ya mshahara wa milion 3 take home nakuona mwendawazimu tu,vip tuseme ni uzush??? Ntarud

Sijajua ulitaka kumaanisha nini apo Xav bero, lakini kama ulimaanisha umewekeza 8000 na ikarudisha ROI nzuri na ya kueleweka huo ni uthubutu mzuri. Lakini nafikiri tunahitaji kuutizama ujasiriamali zaidi ya kuwa chanzo cha ridhiki, vinginevyo kama pesa ikikata utauona ujasiriamali ni uzushi.
 
UJASIRIMALI

Kwanza tutambue kwamba Ujasiriamali upo wa aina mbili ambao ni
- Born
- Made

Born ni wale walio zaliwa na talents na inaaminika kwamba wavunbuzi wengi wa enzi hizo walikuwa Born ukiachukua watu kama Honda na wakina Michael Dell na wakina Henery Ford.

Made
Hawa ni wale wanao tengenezwa na Mazingira kwamba wana jifunza kutoka kwa wanoa waona Chukulia kama Wahindi au hata Wachina au hata Wabongo.

UJASIRIAMALI
Kwanza tuelewe kwamba Ujasiriamali haufundishwi hakuna chuo Duniani cha kufundisha Ujasiriamali kinacho onekana ni njia za kupiga pesa.

KWA NINI UJASIRIAMALI HAUFUNDISHWI?

Kwa sababu ujasiriamali ni Spirt kuna Spirt ambayo humuongoza mtu na pia hata kuna Hormon fulan sitazungumxia hizo Hormon my be next time.

Ujasiriamali ni Passion- Passion haifundishwi

Ujasiriamali ni Commitment- Hakuba mpaka sasa chuo cha kufundisha commitment.

Ujasiriamali ni Confidence- Hakuna chuo cha kufundisha.

Ujasirimali ni Risk- unahitaji kutake risk kitu kisicho fundishwa.

UJASIRIAMALI=MAPENZI

Hakuna chuo cha kufundisha mapenzi, hakuna chuo cha kufundisha jinsi ya kupenda mtu.

Kuna chuo cha kufundisha jinsi ya kudumisha mapenzi.

kufall in love huwa ni mtu kuwa ni spirt ya kumpenda mtu na ndo pale ambapo huwa kuna watu kujiua au unakataliwa una try hata mara 1000.

Sasa basi zile try za kufall in love ndo zile tray za mjasiriamali kujaribu na kuto kata tamaa kamwe.

Ndo walikuwa nazo wakina Thomas Edson.


Unahitaji kuwa na passion kubwa sana kuweza kuwa mjasiriamali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na Ujasiriamali mara nyingi inaaminika huwa na uwezo wa kuona kesho. Huweza kupredict kesho.

Angalia wakina Michale Dell waligundua lini komputa na leo ni lini.

Henery Ford aligundua lini Gari na leo ni lini wapo wengi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MWISHO.

Objective ya Mjasiriamali sio pesa wala utajiri ila pesa au utajiri huwa ni matokeo.

Mjasiriamali lengo lake sio pesa ila pesa huja baada ya kusolve tatizo kwenye jamii

Thomas Edson hakuwa anatafuta pesa bali alitaka kutatua changamoto za kwenye jamii.

Jamaa wa fb ukimuuliza alikuwa hatafuti pesa ila pesa imekuja kuwa ni matokeo ya yeye kusolve tatizo sasa ndo hapo leo hii yeye ni Bilobare kupitia Facebook

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Namvumi King nafikiri umenielewa vibaya, sijazungumzia changamoto za ujasiriamali nimesema kuhusu Uzushi/upotoshwaji unaohusishwa na dhana nzima ya ujasiriamali nikiwa na maana ya kuwa hisia au kweli ambayo mtu anajengewa kichwani kwa kusikia au kifundishwa.

Pia hongera kwa ubobezi wako maana kuamka saa 11 na kifunga saa 11 si mchezo
 
Halafu unakuta mwalimu/ mwezeshaji wa ujasiriamali kwenye kongamano hana hata biashara au mradi wowote. Labda kama huo uwezeshaji ndio ujasiliamali wake ingawaje haufundishi huo.
 
Mkuu ulishawahi kujaribu ujasiria mali ukakushinda? au ni mawazo yako tu?
 
Mkuu ulishawahi kujaribu ujasiria mali ukakushinda? au ni mawazo yako tu?
Boss wng ulichoqoute na ulichouliza vina mahusiano gani?

Any way kuhusu maswali ako huwa sijaribu ts either i do it or nut, i dnt do reheasals.

Kuhusu kushindwa, huwa sishindwa its either i win or learn

Kuhusu mawazo yng, yes ofcourse ni mawazo yng mkuu[emoji4]
 
wewe ni mmoja kati ya watu wenye nidhamu ya uoga utaendelea kutumikishwa mpaka uzeeni mwako mi nilifikiri labda ulishawahi jaribu ukashindwa. Walio fanikiwa ktk ujasiriamali ni wengi tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…