The List
JF-Expert Member
- Mar 25, 2017
- 1,732
- 4,924
Wasalaam wakuu,
Ujasiriamali kwa miaka ya hivi karibuni imekuwa ni jambo linalohubiriwa sana. Watu wa kada mbalimbali wamelisemea kama jambo la kher, na matokeo yake mwitikio kutoka kwa watu mbalimbali umeonekana kwa kuthubutu, kubuni na kuanzisha miradi kwa lengo la kujiajiri. Sio hivyo tu hata baadhi ya waajiriwa wamethubutu kuacha kazi na kujiingiza ktk ujasiriamali.
Uanzishwaji wa shule, makongamano, maonyesho, mashindano na pia kuibuka kwa wahasimashaji wa masuala ya wajasiriamali ni kiashirio cha umaarufu wa dhana hii.
Shuhuda za watu mbalimbali waliopata mafanikio kwa uthubutu wao ktk ujasiriamali imekuwa pia kichocheo kikubwa cha watu wengi kujiingiza ktk ujasiriamali.
Pamoja na mafanikio hayo, upande wa pili kuna kundi kubwa la watu linalolaani ujasiriamali. Kundi hili ni la watu 'waliotendwa' na ujasiriamali.
Na kwa ukweli usiopingika kundi hili ni kubwa kuliko la wale waliofanikiwa. Wengine ni walioacha kazi za kuajiriwa na kwa sasa wanatamani tena kurudi uko, wengine ni wanafunzi walioacha vyuo na kufikri wao pia wanaweza kuwa the next Zuckerback, Bill Gates marehem Steve Jobs na wengineo.
Kundi hili kubwa linalolaani kuhusu ujasiriamali ni kundi liliochagua ujasiriamali aidha kwa kupotoshwa au kuwa na mategemeo makubwa kuliko uhalisia.
Huu binafsi nauiita upotoshaji/uzushi amabao watu wengi humezeshwa kuhusu ujasiriamali na wakiingia uko na kukuta matokeo tofauti basi hubaki ktk simanzi.
Apa nitakupata THE LIST ya uzushi/upotoshaji kuhusu ujasiriamali ambao watu wengi huwaacha ktk simanzi.
Mosi, utajiri/pesa, nafikiri hii inaweza kuwa sababu kubwa. Watu wengi huingia kwenye ujasiriamali kwa mahesab au makadirio makubwa. Mtu anapiga hesab nikiweza kulima tikiti kwa miez mitatu ni milionea au nikiwa na laki5 nikifuga kuku ndani ya miez 6 nitakuwa multimillionair. Ujasiriamali una hela, tena nzuri lakini kama kipaumbele chako ni pesa tu nafikir unahitaj kufikir marambili. Facebook ilikaa miaka 7 kabla haijaanza kuleta faida, yaani kwa miaka saba hao jamaa pesa ilikuwa inawatoka bila return yoyote. Na kama ulikuwa hujui Kampuni ya Amazon mpaka leo haijaweza kuleta r'eal revenue' zaid ya 'operating cost.'
Uhuru. Mwanadamu ni kiumbe anaependa uhuru na huwa mnyonge pale anapoukosa. Iwe ni kwenye maisha ya binafsi au ya kuajiriwa mwanadamu hupenda kuwa huru. Watu wengi huhisi kubanwa na waajiri wao na hivyo kuwanyima uhuru na hivyo huamua ku'opt' ujasiriamali kwa imani watakuwa huru. Iko hivi kama unaona kufanya kazi masaa 8 au 9 unabanwa basi tambua hufai kuwa mjasiriamali. Kwa takwimu tu 'an average entrepreneur hufanya kazi kwa zaidi ya masaa 16-18 kwa siku'.
Umaarufu, hii pia ni kichocheo kikubwa cha watu kuchagua ujasiriamali. Ukweli usiopingika ni kwamba sote tunawafahamu watu kama Tai lopez, Vusi Thembekwayo, Ellon Musk n.k kwa mafanikio yao ktk ujasiriamali. Ni sababu nzuri lakini unahitaji uwe na sabab kubwa zaid kuliko umaarufu tu, Warren Buffet ilimchukua miaka zaid 15 kuwa recognised kama ceedible investor.
Kumbuka kati ya biashara 10 zinazoanzishwa kila mwaka ni 3 tu hufika mwaka wa tatu. Na pia kwa biashara zaid ya 100 zinazoanzishwa kila mwaka ni asilimia moja tu ya biashara hizo humaliza mwaka.
Unahitaji kuwa na sababu/motive nzito za kuchagua ujasiriamali zaid ya hizo tajwa apo juu kama unataka kuwa mjasiriamali mwenye mafanikio endelevu, zaidi ya hapo baki shule au kwenye kibarua chako.