mcTobby
JF-Expert Member
- Feb 16, 2018
- 7,894
- 22,679
Kuna msemo wa kijerumani huwa unasema hivi;JeDem das Seine.
Kwanza niwape salamu zangu na pia poleni kwa stress za uchaguzi.. Najua mambo ni mengi lakini things will work out.👊👊👊
Leo nnalo la kushare nanyi. Kaa makini tumakinike
Katikati ya nchi ya Ujerumani kulikuwa na eneo fulani lililozungukwa na misitu mizito ya miti mida ya usiku sana kulikuwa na party ilikuwa inaendelea. Hakika hii ilikuwa ni party maalum ya watu maalumu.
Eneo hili ilipoandaliwa hii sherehe Ilikuwa ni nje kabisa ya mji lililojulikana kama coesfeld ambapo lilikuwa limezungukwa na misitu mizito ya pine kwenye mkoa wa Mun̈ster. Na jumba hili ambapo sherehe ilikuwa ikiendelea lilikuwa ni jumba au kasri la zamani sana lililoitwa Varlar ambalo lilijengwa Zama za kati ( medieval times ).karne ya 15 huko.
Kasri hili lilikuwa limezungukwa na misitu mizito kiasi kwamba lisingeweza kuonekana kwa urahisi na wapita njia au hata angani mtu akiwa kwenye ndege. Ndani ya kasri hili siku hiyo lilikuwa limepambwa na kupambika na picha za bendera ya swastika ya Nazi kwenye kuta za jengo hili pamoja na manjonjo mengi ambapo wageni hawa walikuwa wakila na kunywa kwa furaha kabisa katika karamu hii .
Nje ya kasri hii napo kulikuwa bize kumetengenezwa na kuandaliwa vizuri kabisa kwa ajili ya uzinduzi maalum uliotarajiwa kufanyika muda mchache majira ya usiku huu wa party.
Nikudokezee kidogo tu, kasri hili la varlar zamani lilikuwa ni monastery ambapo makasisi wa kidini wa kikatoliki karne ya kuanzia karne ya tano walikuwa wakiishi hapo kabla ya ukatoliki kupigwa marufuku karne ya 14 huko Ujerumani.
Sasa lilikuwa limebadilishwa na hata ukoka uliooteshwa kuzunguka kasri(ambapo ukoka huo ulitumika kama sacred place ya ma kasisi kufanyia ibada na meditation) ulikuwa umeondololewa na uwanja kuzunguka kasri hili kuwa clear kabisa kwa ajili ya shughuli maalumu.
Hivyo theluji kali ya usiku ilikuwa imeifunika eneo lote kuzunguka kasri hii ya varlar. Ikumbukwe usiku huu ulikuwa ni wa desemba 9 mwaka 1944 na theluji nzito ya baridi ilikuwa inaonyesha ubabe wake kwa ukali haswa. Nao wahandisi na mafundi kutoka jeshi la Nazi nao walikuwa bize wakichakarika usiku huu nje ya kasri hili kwa ajili ya kufanya marekebisho na matengenezo ya mwisho mwisho ya hapa na pale kwenye mitambo hii maalumu iliyosimikwa nje ya kasri hili kwa ajili ya uzinduzi uliotarajiwa kufanyika muda mchache ujao.
Yeap! Mitambo hii haikuwa nyingine bali ni platifomu za chuma ambazo zilikuwa maalumu kwa ajili ya launchpad za roketi . Kwa wasiojua launchpad ni eneo maalumu ambalo hutumika kusimika mitambo ya kurusha roketi ambazo zinabeba makombora au satellite kwa ajili ya kurushwa hadi angani. Wataalamu wa physics hususaniexf, kwenye mambo ya escape velocity watakuwa wanaelewa.
Sasa basi nje ya kasri hili la varlar matayarisho yalikuwa ni kama yamekamilika. Launchpad (ambazo ni mobile) hizi zilikuwa tayari zimewekwa roketi .Na kila roketi ilikuwa na kombora(war head) aina ya V-2.
Kombora hili ndio ilikuwa silaha ya kisasa kuwahi kutengenezwa kwa wakati huo na jeshi la Nazi, likiwa na uwezo wa kusafiri angani hadi kwenye target iliyokusudiwa. Kombora hili (roketi+warhead) lilikuwa na urefu wa futi 46 na uwezo wa kubeba vilipuzi vyenye uzito wa paundi 2000 ambazo ni sawa na kilogramu 907 hivi.
Kombora hili lilikuwa na uwezo wa kusafiri umbali zaidi ya maili 190 kwa spidi mara tatu ya ile spidi ya sauti. Kwa mfano toleo la kwanza la kombora hili lililojulikana kama V-1,lilisumbua sana .kwa maana ya kwamba lilileta uharibifu mkubwa kwenye majiji makubwa barani ulaya kama London .
Sasa ilitarajiwa kombora hili la V-2 lingekuwa hatari kubwa zaidi kuliko toleo la kwanza .Kutokana na sifa ya kombora la V-2 ilitarajiwa lisingeweza kutunguliwa na ndege yoyote ya jeshi la Allied (ufaransa, uingereza na Russia).
Hii ni kwa sababu kombora hili lilikuwa na uwezo wa kusafiri umbali mrefu angani( high cruising altitude) na lilikuwa na uwezo kushuka kwa kasi sana hadi kwenye target(speed of descent). Hivyo lisingekuwa rahisi kwa kombora hili kutunguliwa.
Kwa mfano waziri wa propaganda au tunaweza kusema ni msemaji serikali (gersonn msigwa wa Nazi😎) wa kipindi hiki wa Ujerumani bwana Joseph goebbels aliwahi kunukuliwa kuhusu silaha hii nzito na akaisifia kwa uwezo wake na kuipa jina silaha hii "wunder waffe" au silaha ya ajabu 'wonder weapon'.
Sasa tukirudi kwenye sherehe hii ndani ya kasri la Varlar, miongoni mwa wageni wa heshima waliohudhuria alikuwa ni Walter Dornberger.
Huyu kwa CV yake alikuwa na cheo cha meja jenerali ndani ya jeshi la Hitler. Huyu bwana alikuwa ni in charge akisimamia mradi wa utengenezaji wa roketi kwenye idara ya kijeshi ya Ujerumani iliyojulikana kama German army's weapon department. Pia alikuwa na shahada ya uhandisi kutoka chuo kikuu cha mjini Berlin .huyu bwana ndiye aliyetoa wazo la kusimika hizi launchpad katika eneo hili la varlar kwa ajili ya uzinduzi.
Mgeni mwingine aliyekuwepo katika hafla hii ndani ya hili kasri alikuwa ni kijana wa miaka 32 ambaye alikuwa ndiye mastermind katika utengenezaji wa hizi roketi zilizokuwepo hapo nje ya kasri hili la varlar. Kijana huyu alitambulika kama Wernher von Braun.
Wengine ambao walikuwa ni wageni wa heshima katika sherehe hii alikuwepo pia Walther Riedel ambaye alikuwa ni mwanasayansi wa ngazi za juu kutoka taasis ya Rocket design bureau.Na mwingine wa nne alikuwa ni Heinz Kunze mwakilishi kutoka wizara ya maswala ya kijeshi iliyojulikana kama Reich ministry of rearmament and war production ya Ujerumani.
Hii shughuli au hafla ilikuwa ya kutoa nishani na medali kwa wageni hawa maalum na ilisimamiwa na waziri wa maswala ya kijeshi wa Ujerumani bwana Albert Speer.
Wageni hawa waalikiwa waliihudhuria hii hafla ndani ya kasri hili la varlar, sio kula na kunywa tu bali kuvishwa medani na nishani kwa kuutambua mchango wao na kazi njema kabisa ya mikono yao katika utengenezaji wa roketi hizi za V-2. Na la zaidi kuzifanyia UZINDUZI.
Kama unaelewa na kutambua mambo ,utajiuliza ni uzinduzi wa aina gani huu ilihali ni silaha yenyewe ni bomu tena la moto sio la maji?. Huu Haukuwa uzinduzi tu wa kukata utepe na mkasi kama wa kuzindua kisima cha maji huko kijijini mwembetogwa na bro jumaa aweso , au kuzindua barabara huko sumbawanga na na Madelu the heir.🤪🤪Nop!.
Na nikukumbushe hii shughuli ilikuwa inafanyika usiku sana ,tena eneo la siri lililozungukwa na misitu mizito ya pines. Kwa hiyo utagundua shughuli hii ilikuwa na usiri kiasi gani.
Ni kwamba uzinduzi huu ulitakiwa kuifanyia majaribio bidhaa hii mpya yaani kombora la V-2 kama kweli italeta matokeo waliyoyatarajia. Hakika huwezi amini kombora hili lilipaswa kurushwa hadi sehemu fulani ndani ya ulaya kama special sapraizi kwao. Au Special package 📦📦.
Sasa ukiachana na uzinduzi huu Maalum uliokuwa ukitarajiwa kufanyika usiku wa siku hii nataka nikurudishe nyuma kidogo Nikupe picha kamili ........