Value ya Mchezaji Husika Kisoka

Value ya Mchezaji Husika Kisoka

Linguistic

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2021
Posts
3,669
Reaction score
8,268
Hizi kelele za Tshabalala ni za kutaka kuongeza value ya mchezaji sehemu husika au katika soko na sio jambo baya kutafuta njia ya kumnadi mchezaji thamani ipande.

Ila

Kuna njia nyingi za kufanya thamani ikapanda esp mchezaji akiwa katika kiwango bora. Moja ya njia nzuri kabisa ni kuboresha mahitaji ya mchezaji kutokana na thamani yake ukaenda kwa uongozi na kudai hivyo vitu mkiwa mezani bila hata kupiga kelele na mkifika kwenye mwafaka mzuri tu.

Kupiga kelele nje can help sometimes kama kelele zikiwa nzuri kwa kutaka backup ya fans wapige pressure kwa uongozi au wenye uhitaji waone ndio chance ya wao kuweka turufu zao kumpata mchezaji.

Ila

Madhara yake ni ukipiga kelele hovyo unaweza kukosa unachotaka na kuharibu image yako na ya mchezaji kwenye future soko na hata mahusiano ya sehemu alipo.
 
Yanga lazima itapata mwekezaji mwenye fedha nyingi.

Kwa sababu, kuna vacuum kubwa kwenye soka la Tanzania na kuna kundi kubwa la mashabiki wa mpira ambao ukiwekeza vizuri utapata pesa ya maana.

Hilo likitokea, ndipo mpira wa Tanzania utaanza kukua kwa kasi, na hili litatokea muda si mrefu.

Kibiashara, hilo lipo wazi na halina ubishi na soon, wachezaji wataanza kuheshimiwa.
 
Kelele ni njia ya kihuni isiyo rasmi na hata Tshabalala ana forum nzuri tu ya kuzungumza na uongozi wakakubaliana au kutokubaliana. Mwisho wa siku image na brand ya mchezaji ni muhimu sana kwa kesho yake. Again, huu mkataba w Tshabalala sio wa kwanza na ya awali iliisha na kujadiliana namna ya kuuboresha na pande zote mbili ziliridhia na kusaini.

Meneja anapotoka hadharani na kutaja anacholipwa mchezaji ni kidogo na anaenda mbali zaidi na kutaja majina ya watu na mifano ni ule mpira wetu wa kihuni pale Kinesi na Lucky Rangers! In fact wa kulaumiwa wa kwanza ni yeye.
 
Kelele ni njia ya kihuni isiyo rasmi na hata Tshabalala ana forum nzuri tu ya kuzungumza na uongozi wakakubaliana au kutokubaliana. Mwisho wa siku image na brand ya mchezaji ni muhimu sana kwa kesho yake. Again, huu mkataba w Tshabalala sio wa kwanza na ya awali iliisha na kujadiliana namna ya kuuboresha na pande zote mbili ziliridhia na kusaini....
Hizi siyo kelele, ni pressure kutoka kwa washabiki. Ambao ndiyo wanaoongoza mpira duniani.
Haziepukiki, zipo natural.
 
Simba ni kubwa kuliko mchezaji yoyote wamepita watu hatari huyo Zimbwe aende kokote anapoona kuna hela nyingi wala hatumzii wala wasitutishe
 
Tshabalala aende anapoona kunamfaa..analeta uswahili ndani ya Club kubwa.
 
Shida ipo kwa meneja wa mchezaji.
Meneja kama kweli unajiamini hakuna haja ya kupuyanga maneno machafu mitandaoni,awasiliane na timu kuhusu mchezaji wake timu ikizingua unamuuza mchezaji wake huko PSG kwenye malipo mazuri,kama huyo meneja ana hiyo exposure ya kuuza wachezaji klabu zenye malipo mazuri na soka safi kuzidi Simba.
 
Hizo kelele ni uhuni na zina gaharama kubwa sana kwa timu.
Nakuhakikishia kwa jinsi Dauda alivyoongea,iwapo Simba watafungwa tarehe 8,kuna washabiki wengi mno watarudi nyuma.
Kwani tunaanza kuwa na mashaka soka letu linaammriwa na wahuni kama akina Dauda.
Kama yanga wanatoa maslahi makubwa kwa wachezaji wazawa,kwa nini watu waanze kumu attack CEO kwa kuzungumzia wanja na lipshiner?Hii si ni dhihaka kwa wanawake?

Kwa nini anawachongea wachezaji kwa washabiki kuwa walikuwa na pre contract yanga?Tuna uhakika gani kama hawa wachezaji hawakuongea zaidi ya hiyo pre contract?

Yanga wamebakiza kuifunga Simba ili waendelee ku maintain washabiki wao na tofauti na hapo mashabiki watarudi nyuma sana.Je huoni kunatengenezwa mazingira ya kuuza mechi hiyo ili kuwapa nguvu wapenzi wa yanga?

Binafsi kelele za Dauda zimenifanya nisiwe na matarajio yoyote katika mechi ya tarehe 8 kwani kuna wahuni wameshaiamulia.

Kama una bet ipe yanga tu maana uhuni wao tumeshaugundua.
Na mwana Simba nenda uwajani ukijua kipigo kinawezekana kwani mazingira inaonesha yameandaliwa na maandalizi yanaendelea kwa kasi sana.
Lengo ni chuki za wahuni dhidi ya Mo na Barbara.
 
Back
Top Bottom