Vancouver na Mapokezi ya FIFA 2026; Jengo la Science World Sasa ni limekuwa Mpira adidas Trionda!

Vancouver na Mapokezi ya FIFA 2026; Jengo la Science World Sasa ni limekuwa Mpira adidas Trionda!

Fascinating

Senior Member
Joined
May 14, 2025
Posts
146
Reaction score
351
Kama umekuwa ukipitia mitandao ya kijamii hivi karibuni, bila shaka umekutana na picha za mabadiliko mapya ya jiji la Vancouver. Muonekano wa jiji hilo umechochewa rasmi na joto la kukaribisha Kombe la Dunia 2026, na safari hii wameamua kuonyesha ubunifu mkubwa sana katika majengo ya jiji hilo ili kuendana na shamlashala za Kombe la Dunia.

VANCOUVER.jpg


Jengo maarufu lenye umbo la duara la Science World limevishwa muonekano mpya kwa kutumia vipande maalum 131 ili lifanane kabisa na mpira wa adidas Trionda, mpira rasmi na alama ya mashindano hayo kwa mwaka 2026. Jengo hili, linalopewa jina la utani la "The Beautiful Dome" (Duara la Zuri), limekaa pembezoni mwa ufukwe wa False Creek, hatua chache kutoka uwanja wa BC Place ambapo mechi za mashindano hayo zitachezwa.

Kutoka Expo ‘86 Hadi Kuwa Alama ya Soka​

Kwa wale wasiofahamu historia ya usanifu na kubadilishwa matumizi si mara ya kwanza kwa jengo hili hususani kwenye kukaribisha majukwaa ya kimataifa:

science-world-built-vancouver-archives-web.jpg

  • Maonyesho ya Expo: Muundo wake ambao ndio huo wa duara, ulijengwa kama banda la muda kwa ajili ya Maonyesho ya Kimataifa ya Expo '86 World's Fair.
  • Kituo cha Sayansi: Baada ya maonesho kuisha halikubomolewa, lkwa ustadi mkubwa iligeuzwa kuwa kituo cha sayansi cha na kutumia jina hilo la Science World, mpaka sasa.
  • Kugeuzwa Mpira 2026: Miaka 40 baada ya kujengwa kwake, unaweza kudhani bwana Bruno Freschi alijua kwamba ubunifuwake ungekuja kukutana na matumizi sahihi. Canada kuwa mwenyeji wa Mashindani makubwa ya mpira kumefanya jengo kupata muonekano ambao wengi wanadhani ndio makusudi ya kujengwa kwake. Mbali na muonekano wake wa nje unaovutia, jengo hilo kwa sasa linakaribisha maonyesho ya kwanza ya Soccer & Technology (Soka na Teknolojia) kutoka Makumbusho ya FIFA kwa ukanda wa Amerika Kaskazini.
scienceworldca_IG.jpg


Kama mmoja wa miji 16 mwenyeji, Vancouver haitoi tu kiwanja cha soka chenye kiwango cha juu cha BC Place, Pia inatoa moja ya mandhari nzuri zaidi ya kwa wageni wa mashindano haya kutoka duniani kote, ikichanganya milima mirefu ya theluji na fukwe za Bahari ya Pasifiki.

Wakuu kama mtu utapataa bahati ya kuwa British Columbia kwa ajili ya mechi hizi, hakikisha unapiga picha ukiwa upande wa Southeast False Creek ili kupata muonekano mzuri zaidi wa jengo hili!

bf1325e9-2eb8-429e-afcb-286f4c0a4fa8.png
 

Attachments

  • ⚽️ Science World has officially transformed into a giant FIFA World Cup 2026 match ball as Van...jpg
    ⚽️ Science World has officially transformed into a giant FIFA World Cup 2026 match ball as Van...jpg
    345.5 KB · Views: 17
  • scienceworldca_IG.jpg
    scienceworldca_IG.jpg
    119.7 KB · Views: 25
  • -FWEBP-S2560.webp
    -FWEBP-S2560.webp
    287.5 KB · Views: 17
Back
Top Bottom