VAT ya 18%

VAT ya 18%

Nsibwene

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2017
Posts
227
Reaction score
160
VAT YA 18% ni kubwa sana na imekaa muda mrefu. Ukiwauliza watu wa TRA wanasema hawawezi kushuhsha sababu ya walipaji ni wachache, na wachache hao wengine ni wadanganyifu.

Nafikiri serikali asilimia ya ikipungua unaongeza wigo wa watu kulipa VAT, sababu wanaona ni kiasi si kikubwa. Hii 18% ikipungua hata kama itafika 16% tutaongeza walipaji nna kufidia pengo la 2% lililopungua.

Natamani serkali iwe na malengo kuwa baada ya miaka kadhaa hii VAT itapungua kuwa kiasi fulani. Tusiwe waoga kuona kwamba hatutapata kile tulichopanga. Ni muda mwafaka wa kupunguza VAT ya 18%.
 
Nchi inapoimarika kiuchumi kitu cha msingi ni kuangalia kodi sina uhakika nchi za Afrika mashariki zinachaji VAT kiasi gani. Aanyejua atusaidie.
Tanzania tulianza na VAT 20% sikumbuki mwaka baadaye ikabadilika kuwa 18%. Tangu hapo hakuna badiliko tena. Unajua kwa kila 100/= kuchukua 18/= si kiasi kidogo. Naamini walipa kodi wengi huwa wanapiga chenga sababu ya hii.
Wachumi Wizara ya Fedha ndio wanadai kuwa walipaji wa kodi ni wachache. Ndio maana wanaogopa kupunguza hiyo 18%.
Je, hii 18% VAT haiathiri wafanyabiashara wa nje kuja kuwekeza Tanzania?
 
Sasa ni watu wa Tra au Sheria ndio unalazimisha iwe asilimia 18?
 
VAT inalipwa na watu wote nchini kupitia bidhaa na huduma mbalimbali 😀. Huyo TRA anayesema wanalipa wachache anatakiwa kupigwa viboko hadharani.
 
Back
Top Bottom