the horticulturist
JF-Expert Member
- Aug 24, 2012
- 1,959
- 1,907
Mkuu myplusbee unaelewaje kipengele hiki cha 72:11-14????
""Nasi tulijua kuwa hatutomshinda Mwenyezi Mungu duniani,wala hatuwezi kumponyoka kwa kumkimbia.""
Je neno hili halionyeshi kulikuwa na wakati ulipita uliokuwa na historia ya hawa viumbe??
Hatuwezi ikiwakilisha jaribio lililopita na Hatutomshinda ikiwakilisha ukweli waliokuja kuugundua Baadae.
Hivi kama Mungu anakuambia zinaa inamchukiza, halafu wewe unaamua kuifanya zinaa tena kwa fujo! Hivi huoni hapo unashindana na Mwenyezi Mungu?! Hata mzazi akikuambia usifanye hiki na kile, halafu wewe unaendelea tu kukifanya; hivi huoni kwamba unajaribu kushindana na mzazi wako?!Mkuu myplusbee kuali ya kwamba ""Hatutomshinda duniani"" huoni kauli hii ikionyesha kuliwahi kuwa na mashindano??
Haiwezekani kuwa waliwahi kushindana??
EXACTLY!! Na hapa ndipo watu wanapochanganya! Wakimuona Sheikh Yahya anazungumzia ulinzi kwa kutumia majini, watu wanadhani ndio Uislamu wenyewe huo wakati Quran imeshasema wazi kwamba, hakuna ulinzi wowote zaidi ya ule unaopewa na Mwenyezi Mungu! Sasa sidhani hata huyo pagan anaamini Jini ndie Mwenyezi Mungu!!Usitazame muislam anafanya nini tazama Qur-ani inasemaje.
Mambo hata ya utabiri,nyota kiislam hayaruhusiwi lakini utakuta masheikh ndio zao hizo kuelezea kesho ya mja
Kwa hiyo ndo majini yakarudi kumuabudu Mwenyezi Mungu baada ya kushushwa aya ya quranSio kwa mujibu wa Quran! Kwa mujibu wa Quran, majini ni miongoni tu mwa viumbe wa Mwenyeji Mungu vilivyoumbwa nae huku wakiwa wamefanana na binadamu kwenye suala la utashi! Lakini kwa kukengeuka tu, wakawa wanafanya yale yanayomchukiza Mwenyezi Mungu hadi pale miongoni mwao siku moja waliposikia Quran na kutoa hiyo kauli kwamba "Nasi tulijua kuwa hatutomshinda Mwenyezi Mungu duniani,wala hatuwezi kumponyoka kwa kumkimbia." Kauli hiyo inaonesha kwamba, pamoja na uovu waliokuwa wanafanya lakini walifahamu uwepo wa Mungu na nini wajibu wao mbele ya Mwenyezi Mungu! Ni kama ambavyo leo hii wanadamu tunavyofanya uovu usiomithirika wakati tunafahamu tufanyayo ni machukizo kwa Mwenyezi Mungu! Na pia tunafahamu katu hatuwezi kumshinda Mwenyezi Mungu, sema ndo vile tumekuwa Watumwa wa Shetani kuliko kuwa watumishi wa Mwenyezi Mungu!
Sasa katikati ya uovu wetu huu, watokee wengine miongoni mwetu watubie kwa Mwenyezi Mungu kwa matendo! Waamue kuacha yale yote yaliyo machukizo kisha ndipo wanakuja kusema "Nasi tulijua kuwa hatutomshinda Mwenyezi Mungu duniani,wala hatuwezi kumponyoka kwa kumkimbia." Kwamba, twafanya uovu wote huu sio kwamba hatujui uwepo wa Mwenyezi Mungu na yale yamchukizayo; au si kwamba wakati uliopita palikuwa na historia inayotuhusu watu kama sisi, bali ni vile tu tumeshukiwa na maono na kuamua kwa dhati kurejea kwa Mwenyezi Mungu!
Sio majini bali baadhi ya majini! NI kama kwa binadamu tu! Hata baada ya Quran kushushwa, sio wote walianza kumuabudu au wanamuabudu hadi leo!Kwa hiyo ndo majini yakarudi kumuabudu Mwenyezi Mungu baada ya kushushwa aya ya quran
Hapana mkuuupo hai??