Sio kwa mujibu wa Quran! Kwa mujibu wa Quran, majini ni miongoni tu mwa viumbe wa Mwenyeji Mungu vilivyoumbwa nae huku wakiwa wamefanana na binadamu kwenye suala la utashi! Lakini kwa kukengeuka tu, wakawa wanafanya yale yanayomchukiza Mwenyezi Mungu hadi pale miongoni mwao siku moja waliposikia Quran na kutoa hiyo kauli kwamba "Nasi tulijua kuwa hatutomshinda Mwenyezi Mungu duniani,wala hatuwezi kumponyoka kwa kumkimbia." Kauli hiyo inaonesha kwamba, pamoja na uovu waliokuwa wanafanya lakini walifahamu uwepo wa Mungu na nini wajibu wao mbele ya Mwenyezi Mungu! Ni kama ambavyo leo hii wanadamu tunavyofanya uovu usiomithirika wakati tunafahamu tufanyayo ni machukizo kwa Mwenyezi Mungu! Na pia tunafahamu katu hatuwezi kumshinda Mwenyezi Mungu, sema ndo vile tumekuwa Watumwa wa Shetani kuliko kuwa watumishi wa Mwenyezi Mungu!
Sasa katikati ya uovu wetu huu, watokee wengine miongoni mwetu watubie kwa Mwenyezi Mungu kwa matendo! Waamue kuacha yale yote yaliyo machukizo kisha ndipo wanakuja kusema "Nasi tulijua kuwa hatutomshinda Mwenyezi Mungu duniani,wala hatuwezi kumponyoka kwa kumkimbia." Kwamba, twafanya uovu wote huu sio kwamba hatujui uwepo wa Mwenyezi Mungu na yale yamchukizayo; au si kwamba wakati uliopita palikuwa na historia inayotuhusu watu kama sisi, bali ni vile tu tumeshukiwa na maono na kuamua kwa dhati kurejea kwa Mwenyezi Mungu!