Guru Master
JF-Expert Member
- Jan 14, 2017
- 226
- 594
Nimekumbuka kisa cha mfalme mmoja wa nchi iliyo chini ya jua ambaye alipenda sana kuvaa na kusifiwa kwa mavazi aliyokuwa akivaa. mfalme alitengenezewa mavazi yenye rangi mbalimbali kama vile hudhurungi,samawati na hata kijani kiwichi. alitembea na nguo zake zenye kumeta meta kila sehemu na watu walimfisia sana kuwa hakika mfalme ajua kuvaa. mfalme alitafuta mafundi washoni toka kwenye miisho ya dunia akitaka vitamba vyenye rangi na darizi mbalimbali ili mradi akidhi kiu yake ya kuonekana mtanashati.
walitafutwa mafundi washoni toka pembe za dunia wakaja mfanyia nguo za kupendeza mfalme. na mfalme alikuwa akipita mtaani kwa madoido watu wamwone akiwa kwenye gari lake la farasi la wazi. watu waliambiwa wajipange pembeni ya barabara ili waje mtizama mfalme. huu ulikuwa utaratibu wa kila mara pale mfalme anapokuwa na vazi jipya. raia walijipanga barabarani kwa mistari kumtizama na kumshangilia mpaka akimaliza kuzunguka mjini halafu wakarudi kuendelea na shughuli zao za kuhangaika na maisha magumu.
siku moja mfalme aliamka usiku wa manane akawaza sasa atavaa nguo kwa week ijayo kuwaonesha wananchi nguo mpya. akapata wazo kuwa awaite washauri wake wote na mawaziri.wakaja wakitetemeka na kumsabahi "mfalme uishi milele" akainua kichwa chake kutikisa kuwa ameipokea salamu ile. mawaziri na washauri wale walikuwa wamekuja wengine wakiwa na nguo za kulalia,wengine wakiwa pekupeku na wengine wamejifunika tu mashuka. wakawa wameinama mbele ya mfalme akiwataka ushauri. katika kutaka ushauri akawaambia kuwa anahitaji nguo ambao dunia nzima wakimwona amevaa watamshangaa na kustaajabu.
wale washauri wake wakamwambia hilo linawezekana na usiku huo huo ikapigwa baragumu mji mzima wakusanyike.wakakusanyika mpaka kufika alfajiri hakuna aliyekuwa amesalia kwake. mfalme akatangaza tenda hiyo kwa mafundi ushoni wote nchi ile iliyoko chini ya jua. wakaja toka miisho yote ya dunia. katika hao mzee mmoja akasema anaweza mshone nguo mfalme ambayo hiyo nguo ni ya utukufu. nguo ambayo itamsaidia kuwagundua wabaya wake na pia wenye dhambi ambao wanakwamisha juhud zake nzuri za maendeleo kwa nchi ile.
mzee huyu akapewa kazi hiyo akasema atachukua siku tano kuishona. akaishona na kabla ya kuipeleka kwa mfalme akamawambia kuwa nguo ile inaonekana kwa watu ambao ni watakatifu.walio na dhambi hawawezi kuiona ile nguo. mfalme akatangaza ujio wa nguo ile ya ajabu. kuwa sasa atapata nafasi ya kugundua watenda dhambi na wabaya wake. mzee yule akaja na nguo ile ikulu kumletea mfalme. mfalme aliitizama ile nguo.hakuona kama kuna nguo mikononi mwa mzee yule.ila akakumbuka kuwa ile ni nguo ambayo kama una dhambi huwezi iona. haraka akasema ni nguo nzuri. na hajawah kuona material mazuri na rangi za kuvutia kama zile duniani.
akatangaza siku iliofuata kile mtu asimame barabarani kuona ngio ya mfalme na akawakumbusha wenye dhambi kuwa sasa kiama chao kinakuja maana wao hawataiona. basi asubuh mfalme akaanza kutembezwa kila kona ya jiji.watu walimtizama kwa kumshangaa...midomo ilibaki wazi wakishangilia na kufuruh kumwona mfalme. yeye alitabasamu na kugeuza kichwa huku na kule kwa madaha akipunga mkono. na siku hiyo kulikuwa na shangwe kubwa sana nchini pale. bahati mbaya katoto kamoja ambako hakakuwa kamesimama na wazazi wake kakaropoka. "heeeeh...mfalme leo kaamua kutembea uchi" watu wakashtuka na kukaziba mdomo kale katoto.
baadaye wakarudi ikulu mfalme akauliza wanalionaje lile vazi. mawaziri na wasaidizi wake wakasema kwa kweli ni vazi zuri kabisa ambalo lilishonwa na mungu mwenyewe kupitia mwanadamu. akiwa anakula akamuuliza waziri mkuu hili vazi lina rangi gani.. waziri mkuu akajibu nyekundu si nyekundu,nyeupe si nyeupe,kijani si kijani,nyeusi si nyeusi,hudhurungi si hudhurung yaani hata ni ngumu kusema.
akiwa na mkewe chumbani akamwambia walale.... mkewe akajisahau na kutamka "leo umekuja chumbani umeshavua nguo kabisa" mfalme akashtuka na kuhisi kuwa mkewe ni mwenye dhambi. akamuita kuhani haraka aje amchukue mke wa mfalme akampime dhambi zake. akiwa anatembea hivi mtoto mwingine akamwonesha mama yake "mama angalia ile dudu ya mfalme inaning'inia. mfalme alkasirika sana akasema yule mtoto akamatwe lakini kwa mujibu wa katiba ya nchi ile mtoto wa miaka 4 alikuwa akihesabiwa kuwa ni mtakatifu. ikabidi watu mbalimbali waulizwe kuhusu vazi la mfalme.......
ikaja kubainika mfalme alikuwa hajavaa vazi lolote toka siku ile ya kwanza ya maonesho ya vazi jipya. alikuwa akitembea uchi. washauri wake na mawaziri hawakuweza mwambia maskini. mpaka mtoto mdogo alipokuja kulizungumza hilo.
"kuweni watu wema na msio na dhambi"