Lady Whistledown
JF-Expert Member
- Aug 2, 2021
- 1,147
- 2,008
Mwanamuziki huyo wa Nigeria amekosolewa vikali kwenye mitandao ya Kijamii baada ya kuvaa gauni lenye 'ngao' iliyowazuia wahudhuriaji wengine kuonekana na kuona mbele.
Gauni hilo jeupe lililokuwa na ngao iliyofunika kichwa chake, lilizua sintofahamu baada ya picha kusambaa ikimuonesha mwalikwa mmoja akikunja shingo yake ili kuweza kutazama jukwaani.
Watumiaji wengi wa Twitter walikerwa na kukosoa kitendo hicho kwa kumwita Tems "mkorofi", mwenye dharau na asiyejali wengine.