Mbunge wa Musoma Mjini (CCM) Vedastus Manyinyi amesema Serikali inapaswa kusikiliza kilio cha wananchi kuhusu kikokotoo kwani wao wanataka wapatiwe pesa zao zote na siyo kupewa kwa utaratibu mpya uliopo.
"Hili suala la kikokotoo lipo wazi, siku za nyuma wastaafu wale walikuwa wanalipwa karibu nusu ya mafao yake halafu hiki kingine analipwa kidogo kidogo. Na kwa sababu yule mtumishi siku anaajiriwa alikuwa anajua kabisa kwamba baada ya muda fulani atastaafu, kwahiyo tafsiri yake alikuwa anajiandaa akijua kwamba akistaafu atapata fedha yake, ataendelea na maisha. Sasa leo unapomkata na kumrudisha hadi kwenye 1/3 halafu unasema hizo zingine utamlipa kila mwezi zaidi, mwisho anapata frustration, baada ya miaka 5 anapoteza maisha" amesema.
Ameongeza, "Sasa mimi naanza kujiuliza, hii najua ni Serikali ya wananchi, na hao hao wananchi wao mapenzi yao wanapenda walipwe pesa za kutosha ili maisha yake yaendelee. Sasa wewe Serikali inakuhusu nini, useme mimi sikulipi hivi badala yake naendelea kukulipa nusu nusu"
Amemuomba Waziri Ndejembi kwenda kushughulikia suala hili.
Naye Mbunge wa Arusha Mjini (CCM) Mrisho Gambo akizungumzia suala la Kikokotoo amesema changamoto inayoona ni Serikali kushindwa kutafuta mbinu sahihi za kushughulikia suala hili, badala yake wameenda kumuadhibu mtumishi ambaye yeye ni victim wa haya.
Pamoja na mambo mengine, Gambo ameshauri Serikali irejeshe fedha zote ilizokopa kwenye mifuko ya hifadhi ili kurejesha uhai wa mifuko hiyo.
Jamaa ameongea Point sana ubaya ni wote wanaohusika nakufanyia kazi hili, hawana Muda nalo kwasababu kikokotoo kipya kinaathiri watumishi wa chinii tu...wenzetu wabunge na mawaziri wao wakistaafu wanalipwa mafao yao yote kwa mkupuo na mbaya zaidi ni mafao ambayo hawakuwahi kuchangia kama watumishi wanavyokatwa kwenye mishahara.