VENGU (Joseph Shamba) anaumwa, kalazwa Muhimbili tumuombee na kumjulia hali

Pole vengu lakini ni nini hasa chanzo cha kulazwa? I mean anaumwa ni nini?
 
nakushukuru Rais Kikwete kwa Moyo wako wa Huruma kwa kumjulia Mgonjwa Josef hali. Inaleta tumaini na faraja kwa tunaompenda msanii wetu. Asante kwa kutoa muda wako kwa jambo hilo ambalo hata familia ya Vengu wamepata faraja. Mheshimiwa, Vengu ndio alikuwa mzima wa afya akifanya kazi yake na kutuburudisha, ghafla tunasikia yuko hoi kiasi hicho, hivyo kama inawezekana kupata tiba pengine ninaomba naye apatiwe. Mungu akubariki Mheshimiwa Rais na uendelee kuwa na moyo huo wa kuwatia faraja wagonjwa.
 

Mungu fanya kitu..huyu jamaa uwa ananifurahisha akiigiza kama Mrema...CCM wampeleke India maana ni mwanachama wao..Namuombea sana apone jamani...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…