Veterinary medicine is the best
- Uahkika wa ajira ni mkubwa kutokana na uhitaji wa madaktari wa mifugo nchini. Pia vets wanachukuliwa sana katika kufundusha vyuo hata vya medics, research institutes n.k. Pamoja na serikali kujitahidi kuajiri sana vets mwaka 2008-2011, bado nafasi ni nyingi kutokana na hawa watu kuwa na soko katika maeneo tofauti. Ukisoma vet, unaqualify kusoma coz nyingi sana masters. Mshahara wao ni mzuri serikalini maana wanaanzia TGS F, tofauti na wengine wanaoanzia TGS D.
Tatizo la vet ni kuwa utasoma miaka at least 5,na unaweza kurudia hadi ikawa 7, shule yao imetait sana na ukifika inabidi ukomae sawa na shule. Competition kwa miaka ya karibuni imekuwa kubwa kidogo, nadhani ni kutokana na kuhakikishiwa mkopo au grant ya 100%, lakini pia kutokana na ubora wa coz
Biotechnology is the second
Uhakika wa ajira serikalini sio mkubwa sana, ingawa potentially upo juu, kutokana na hawa watu kuhitajika kwenye research na mahosipitalini. Pia wanaajiriwa sana kwenye institutes kama TBS, TFDA, na mkemia mkuu. Ni kozi nyepesi sana, ukikomaa una uhakika wa kuibuka na class nzuri ya degree, hali inayokuweka katika mazingira mazuri sana ya kupata masters na kuwa kumpeititve kwenye ajira.
Chance ya kupata mkopo hasa kuanzia mwaka huu ni ndogo ila ipo
Agribusiness is the last
Kati ya ulizozitaja, hii hapa ni ya kubahatisha zaidi kwenye ajira. Hata hivo kutokana na ubora wa elimu ya SUA, hawa jamaa mtaani wako competitive sana ukifananisha na kozi nyingine za biashara na uchumi toka vyuo vingine. Uzuri wa hii kozi ni kuwa ukibahatisha ajira, mara nyingi inakuwa na jiwe kubwa hasa kwenye sekta binafsi. Uwezukano wa kupata ajira serikalini ni mdogo sana.
Chance ya kupata mkopo wa kusoma, hasa kwa mwaka huu ni ndogo sanaaaa.