Amalinze
JF-Expert Member
- May 6, 2012
- 6,780
- 5,305
Habari wana JF,
Luther Vandross Snr,aliyezaliwa mwaka 1919 alioana na mpenzi wake wa utotoni Mary Ida(Aliyezaliwa 1922) akiwa na umri wa miaka 27.Vandross snr na Mary walibahatika kupata watoto wanne wakiwa ni Patricia,Ann,Lawrence na kitinda mimba Luther Vandross jr.Baba yake luther alikuwa ni msanifu wa samani na mama yake alikuwa ni nurse.Kipaji cha Luther jr kilichangiwa sana na Dada yake Patricia ambaye alikuwa kwenye kundi matata sana la The Crest lililovuma na kibao kikali cha 16 candles miaka ya 50's.
Ilipofika mwaka 1959 Baba yao Mzazi Mzee Luther Vandross Snr alifariki kwa ugonjwa kisukari hivyo ikamlazimu mama mary kushikilia msikani.Katika Pilika za kukabiliana na maisha hivyo familia ikajikita katika fani ya mziki na fashion,Luther,Lawrence na Patricia wakajikita kwenye muziki huku Ann akijikita kwenye Uanamitindo.Lawrence alijikita zaidi kama manager wa wasanii.
Mwaka 1986 Lawarence,Luther pamoja na wasanii wawili waliokuwa anawamaneji,walipata ajali mbaya iliyosababisha kifo cha brother wake Luther Vandross Lawrence aka Larry.Maisha yaliendelea hivyo hivyo huku Luther akizidi kupata mafanikio ya kimziki kwani kwa mwaka 1985 alinunua mercedenz mpya ya mwaka 1985 ambayo ndio hiyo aliyopata ajali.
Mwaka 1993 Familia hiyo ilipata pigo jingine la kuondokewa na Dada yao Patricia vandross kutokana na complications za kisukari.Baada ya miaka 6 naye dada yao Ann Vandross alitangulia mbele ya haki kwa ugonjwa wa Asthma.Baada ya kifo cha Ann familia ya Vandross ilibakiwa na watu wa wiwili tu yani Luther na Mama yake Mzazi(Mary Ida).
Mwaka 2003 Luther alipata Stroke iliyosababisha kuwa katika comma kwa mda wa miezi miwili hali iliyosabisha kuzorota kwa afya yake,mbali ya stroke Luther pia alikuwa anasumbulia na sukari pamoja na presha.July 2005 Luther vandross aliaga dunia.Miaka mitatu baadae yaani 2008 pia mama yake Luther alifariki dunia kwa complications za kisukari na Pressure.

Baba Mzazi wa Luther Vandross akiwa na Mke wake(Mary Ida) miaka ya katikati ya 1950.

Luther Vandross(Kushoto) Akiwa na Baba yake Pamoja na Lawrence Larry(Kaka yake)

Luther Vandross akiwa na Mama yake Mzazi.

Luther Vandross(1951-2005)