Very sorry Eliza, I lied to you huu ndio ukweli

Very sorry Eliza, I lied to you huu ndio ukweli

Rabboni

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2015
Posts
1,096
Reaction score
1,588
Nimekutafuta kwa muda mrefu, sijafanikiwa kukupata!! Naamini kabisa utakuwa member hapa JF.. and this is the only way for me to confess and let you to know the truth!! I got ur number kupitia kipindi kimoja cha usiku kilichokuwa kinarushwa na Kiss Fm, presenter wa hiki kipindi alikuwa anaitwa Tobby, sijui kama bado kina exist au lah!! it was in 2008..at that time nilikuwa Dodoma wewe Dar Ulinipiga simu kwenye kile kipindi na ukasema unatafuta rafiki baada yakutokea kutokuelewana kati yako na boyfriend wako.

Namba yako iliniingia kichwani mwangu as u mentioned it. At the same night nikajaribu kukucall but simu yako ilikuwa busy sana, Haikunipa shida kwani niliamini patakucha, na ikawa hivyo, asubuhi yake nikajaribu tena.. Ikaita bila kupokelewa, nikaamua kupotezea Kwenye mida ya saa nne u called me, wow! Ile hallo yako tu ilinitetemesha, nikajua hujui kiswahili kabisa!! Niliogopa kidogo coz kwenye huo uwanja siko vizuri sana. Swali lako la kwanza nilikuwa, who is this? ...Ur talking to Derick!! uongo wa kwanza huu, hili halikuwa jina langu and i don't know kwa nini nilitamka jina hili.

I found ur missed call, what is up? why did u call me? Nikakujibu i just got ur number from Radio yesterday as u need friend for chatting and exchanging ideas, Ukasema, ahaa ur welcome, u asked me where are you? Nikakuambia Dodoma, hapa ni kweli!! Tukaongea mawili matatu pale basi ukata simu, baada ya kama saa moja hivi nikakutext . Do you know Swahili? ilichukua another three hours for you to reply, Yes I know Swahili much, mi ni mtanzania bwana! Good, nikakuambia unaongea kama mtu asiyejua kiswahili kabisa!! But i like the way u talk, ukaniambia hata mimi naongea vizuri. Ahaa, mwanaume naongeaje vizuri wewe? unanitusi kijanja eeh.

Mawasiliano yangu na Wewe yaliendelea poa sana, tulianza kupigia simu mara kwa mara,
Tulizoeana vizuri kweli!!
Nakumbuka ulianza kunipa injili eneo ambalo naona uko vizuri!!
Eliza uliniandikia bible verses nyingi sana, ulikipenda kitabu cha Isaya!
Mara nyingi tukiongea kabla hatujaagana ulisali, i remember many of ur prayers!!
Nilikuwambia niko dodoma chuo kikuu, huu ulikuwa uongo pia! Dodoma nilikuwa sina deal ya maana zaidi ya udeiwaka wa hapa na pale!! nilijitahidi sana kujiweka kichuo, sometimes nikuambie kuwa niko class kumbe napeleka matenga ya nyanya kongwa.

Tulizoena sana Eliza kumbuka kuna kipindi ulishindwa kulala tusipozungumza, ulini encourage kwa mambo mengi sana. Uliongea na mimi kwa upole, sana sana ukinihusia kulishika neno la Mungu.
Tukawa marafiki wa kweli bila hata kuonana.
Tulianza kupata hamu ya kuonana, kumbuka ishu ilikuwa chuo na wewe shughuli zako hapo Dar ambazo zikuwahi kuzijua pia.
Elie uliniambia unafahamu lugha saba za kimataifa..
Uliniambia umeshakwenda nchi nyingi Duniani, I trusted u! uwezo wako wakuelezea mambo ulikuwa mkubwa sana, unamzidi lara 1 kidogo (sijui yeye anazungumza lugha ngapi)!

Niliendelea kuwasiliana na wewe kwa njia ya simu local calls as that time mambo ya social network yalikuwa hayajasikika sana.

We became very good friends japokuwa hatujawahi kuonana hata kidogo, sijui ni kwanini hata wazo lakutumiana picha hatukuwa nalo.
Kila siku ilikuwa nilazima tuzungumze na mara nyingine ilituchukua hadi usiku mrefu sana, uliweza kunipigia simu kwa saa kadhaa tukizungumza mambo ya maisha na kwa kweli wewe ndiye uliyekuwa mzungumzaji mkuu.

Nakumbuka ulianza hadi kuniunganisha na ndugu zako, (one of ur young sister) na ilitokea yeye kufurahia sana mawasiliano yetu.

One day uliniagizia kuja kwenu nakumbuka ulisema ni Boko magengeni ndiyo kituo na ulinipa maelekezo vizuri ila sijawahi kuja kwenu.
Kila nikija Dar nilitamani kufika ila mambo yakawa mengi sikufika. Kutokufika kwangu hakukutisha mawasiliano yetu, na hata neno la Mungu ulinipa sana.

Kosa langu lililonifanya nikuombe msamaha kwa sasa ni hili hapa.
Nakumbuka siku nikiwa Dar na nikakujulisha ulitaka sana sana tuonane, na mimi nilikubaliana na wewe kuwa this time we should see each other, kiukweli utaratibu tuliuweka tukutane Mwenge, ila mimi nilichelewa kufika na wakati niko njiani uliniambia unaenda Muhimbili kulikuwa na mgonjwa kwa hiyo hata nikfika Mwenge itabidi nikusubirie tu...
Sikuona tabu kwa upande wangu kwasababu nilikua nimeongozana na wenzangu wawili sikupata shida kukusubiana, tulisubiri pale huku tukifanya mambo mengine tu..
Ilichukua muda sana kuja nakumbuka uliniandikia meseji ukanielekeza nipande basi zinazoenda Posta nishukie Kituo kinachoitwa Pam beach tutakutana hapo.
Nadhani ulikuwa hujui kama sikua peke yangu.
Tulipanda daladala na tukashukia Pam beach kama ulivyoagiza bahati nzuri bado tulifika kabla yako,
Tulikaa ile sehemu ya abiria wanakokaa kusubiria daladala, uliniambia ulikuwa karibu sana and u will be there after few minutes....
Kweli ukaja nikakuona ulivyokuwa unaanza nipigia simu ili unibaini, kwa ustadi mkubwa kwenye ile simu nikafuta mlio, nilikuona vizuri mno Eliza wewe ni mrefu maji ya kunde na mwili wako umejajaa kidogo...

Nilikupungia ili ujue ndiyo sisi uje.
Ukaja kwa madoido yote kabisa ukaniuliza who is Derick here? Na mimi bila kuchelewa nikanyosha kidole kumwelekea yule jamaa niliyekuwa nae...(nilikuwa na wenzangu wawili mmoja Me na mwingine Ke).
Basi Eliza ulimkumbatia mshikaji kwa hisia kweli kweli, kitu kilichomshangaza kwani hata wao nilikuwa sijawaambia kuwa nakutana na mtu ambaye sijawahi kukutana nae kabisa.

Basi kuanzia hapo picha ikawa inaanza kuharibika kumbuka wewe na mimi tumewasiliana kwa muda mrefu kwa hiyo lazma kila utakachoniuliza nijibu...

Sasa baada ya lile picha, Eliza ulizungumza kwa furaha sana, nakumbuka ulikuwa ukitabasamu sana bila kuchelewa ulisema tuende Mwenge sehemu tulivu tupige stori mbili tatu, jamaa yangu na yule dada niliyekuwa nae walikuwa wameshaanza kuusoma mchezo sasa, bahati nzuri mchizi naye alikuwa mjanja sana hakubabaika kabisa, kila ulilomuuliza alisema yah yah na hakuweka neno la ziada as alikuwa hajui kabisa ajibu nini, tukiwa ndani ya gari jamaa alikuwa akinitumia text akinisihi sana nikwambie ukweli kwani nilimweka kwenye wakati mgumu sana, nilimwambia nitakuambia tukifika Mwenge.

Duh hali ilikuwa ngumu sana kwa jamaa yangu kwa sababu uliendelea kumpigisha stori azizozijua kabisa!!
Mbaya ni pale ulipompigia mdogo wako, ambaye niliwahi kuzungumza nae ukimsimulia jinsi ulivyoniona na jinsi nilivyo, maskini ulikuwa unaongea na mdogo wako juu ya mtu asiye sahihi na yule uliyezoea kuongea nae kila siku.
Bahati nzuri mimi na rafiki yangu ni warefu tuliendana ila kidogo tu.
Tulifika Mwenge ukatupeleka sehemu na ukasema tuseme chochote...
And that time nahisi ulikuwa umeshaanza kupata mashaka kwani kuna point ulimuuliza jamaa yangu akaikosea majibu kabisa,
Ulimlalamikia kidogo ukimuuliza umesahau haraka hivyo? Ulijitahidi sana kuelezea lakini mchizi ilibidi amute tu as alikuwa haelewi kabisa hiyo habari.
Ukimya ulitawala kidogo then ukatext ukasema ''Derick ur so handsome''...
Leo nimedhibitisha nilichokuwa nakiamini.
Roho na mwili wangu vimefurahi sana kukuona. Niliisoma kijanja wala siku ijibu.
Ulinitext tena ukiniambia ningekuambia mengi but not here coz of ur friends presence sitaweza, karibu sana nyumbani kwetu.
Hapa nilijibu tu thanks!
Tuliendelea na stori nyingi nyingi as ulikuwa main speaker ulituambia sana habari zako...
Hapo sisi wengine watatu tulikuwa wasikilizaji tu, jamaa yangu alinitumia ujumbe akaniambia nikusaidie kumwambia ukweli? Nilimzuia nikamwambia nitakuambia mwenyewe.
Yule dada mwingine alishauelewa mchezo tayari na aliniandikia pia akinisisitizia nikuambie ukweli ili mshikaji wangu awe huru.

Kuna muda ulipiga simu home kwenu kwa mdogo wako, na ukataka aongee na mimi, mshikaji alipata wakati mgumu na kiukweli sauti zetu hazikuwa zinaendana.
Nilijipanga kukuambia ukweli ila nilikosa kabisa gia yakuanzia. Eliza ulikuwa mwongeaji sana, ulitusifia sana ila ndiyo hivyo nilikudanganya, wakati wakuondoka ulifika na kwa mara nyingine ulimkumbatia tena jamaa yangu kwanza then ukatuhagi na sisi at last ulihag the right person.. wewe ukaelekea Boko sisi tulielekea Mlimani ( udsm) jamaa yangu alikuwa anasoma pale.
Nakumbuka dakika kumi na tano hazikuisha uliniandikia meseji ndefu kama waraka, ukielezea tu jinsi ulivyoniona na ulivyofurahi niliwaonyesha marafiki zangu ule ujumbe, kiukweli walinilaumu sana.

Niliujibu ujumbe wako kwa kifupi tu.
Uliandika tena ukiniuliza nimekuonaje then mbona hukuwa na raha most of the time?
Nilijibu nikijaribu kukusifia na mimi ili zile sifa ulizonipa ziendane kidogo...
Tuliendelea na mawasiliano na uliniomba sana nifike kwenu kabla sijarudi Dodoma...

Sikuweza kuja kwenu na bado sikuweza kukuambia ukweli.
Tulipoteza mawasiliano na mpaka sasa sijui ulipo na hujui nilipo.
Bahati nzuri nilishaajiriwa sasa sifanyi tena udeiwaka na siishi Dodoma tena.

Ninaamini Eliza unaweza kuwa member wa hili jukwaa na kwa sasa bila shaka utakuwa ushaolewa labda na una watoto kabisa.
Nisamehe Nilikuelekezea kwa mtu tofauti, na kwa sababu hii elewa sasa the another person was the right one.
Barikiwa sana na Asante kwa sababu utanisamehe.
 
Its a long story, nitaiendeleza na kama Eliza atajitokeza atadhibitisha kuwa nastahili kumwomba msamaha...
 
Malizia simulizi yako ueleweke, au kama vipi niuzie niimalizie mimi.
 
Inawezekana kabisa Eliza ni mmoja ya watu maarufu sana hapa jf
 
Nimekutafuta kwa muda mrefu, sijafanikiwa kukupata!! Naamini kabisa utakuwa member hapa JF.. and this is the only way for me to confess and let you to know the truth!! I got ur number kupitia kipindi kimoja cha usiku kilichokuwa kinarushwa na Kiss Fm, presenter wa hiki kipindi alikuwa anaitwa Tobby, sijui kama bado kina exist au lah!! it was in 2008..at that time nilikuwa Dodoma wewe Dar Ulinipiga simu kwenye kile kipindi na ukasema unatafuta rafiki baada yakutokea kutokuelewana kati yako na boyfriend wako.

Namba yako iliniingia kichwani mwangu as u mentioned it. At the same night nikajaribu kukucall but simu yako ilikuwa busy sana, Haikunipa shida kwani niliamini patakucha, na ikawa hivyo, asubuhi yake nikajaribu tena.. Ikaita bila kupokelewa, nikaamua kupotezea Kwenye mida ya saa nne u called me, wow! Ile hallo yako tu ilinitetemesha, nikajua hujui kiswahili kabisa!! Niliogopa kidogo coz kwenye huo uwanja siko vizuri sana. Swali lako la kwanza nilikuwa, who is this? ...Ur talking to Derick!! uongo wa kwanza huu, hili halikuwa jina langu and i don't know kwa nini nilitamka jina hili.

I found ur missed call, what is up? why did u called me? Nikakujibu i just got ur number from Radio yesterday as u need friend for chatting and exchanging ideas, Ukasema, ahaa ur welcome, u asked me where are you? Nikakuambia Dodoma, hapa ni kweli!! Tukaongea mawili matatu pale basi ukata simu, baada ya kama saa moja hivi nikakutext . Do you know Swahili? ilichukua another three hours for you to reply, Yes I know Swahili much, mi ni mtanzania bwana! Good, nikakuambia unaongea kama mtu asiyejua kiswahili kabisa!! But i like the way u talk, ukaniambia hata mimi naongea vizuri. Ahaa, mwanaume naongeaje vizuri wewe? unanitusi kijanja eeh.
nipigie maana waongea poa...sana.hebu inbox,mambo hayo fresh sana kwangu.
 
Wa tz bhana, hebu hiyo stori usiendelee kusimulia hapa, weka kwenye nakala haraka kisha nitafute ili hicho kitabu tukiingize kwenye mtaala wetu, hii stori inawafaa sana wanafunzi wa form 3.
 
Mawasiliano yangu na Wewe yaliendelea poa sana, tulianza kupigia simu mara kwa mara,
Tulizoeana vizuri kweli!!
Nakumbuka ulianza kunipa injili eneo ambalo naona uko vizuri!!
Eliza uliniandikia bible verses nyingi sana, ulikipenda kitabu cha Isaya!
Mara nyingi tukiongea kabla hatujaagana ulisali, i remember many of ur prayers!!
Nilikuwambia niko dodoma chuo kikuu, huu ulikuwa uongo pia! Dodoma nilikuwa sina deal ya maana zaidi ya udeiwaka wa hapa na pale!! nilijitahidi sana kujiweka kichuo, sometimes nikuambie kuwa niko class kumbe napeleka matenga ya nyanya kongwa.

Tulizoena sana Eliza kumbuka kuna kipindi ulishindwa kulala tusipozungumza, ulini encourage kwa mambo mengi sana. Uliongea na mimi kwa upole, sana sana ukinihusia kulishika neno la Mungu.
Tukawa marafiki wa kweli bila hata kuonana.
Tulianza kupata hamu ya kuonana, kumbuka ishu ilikuwa chuo na wewe shughuli zako hapo Dar ambazo zikuwahi kuzijua pia.
Elie uliniambia unafahamu lugha saba za kimataifa..
Uliniambia umeshakwenda nchi nyingi Duniani, I trusted u! uwezo wako wakuelezea mambo ulikuwa mkubwa sana, unamzidi lara 1 kidogo (sijui yeye anazungumza lugha ngapi)!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom