Very sorry Eliza, I lied to you huu ndio ukweli

Niliendelea kuwasiliana na wewe kwa njia ya simu local calls as that time mambo ya social network yalikuwa hayajasikika sana.

We became very good friends japokuwa hatujawahi kuonana hata kidogo, sijui ni kwanini hata wazo lakutumiana picha hatukuwa nalo.
Kila siku ilikuwa nilazima tuzungumze na mara nyingine ilituchukua hadi usiku mrefu sana, uliweza kunipigia simu kwa saa kadhaa tukizungumza mambo ya maisha na kwa kweli wewe ndiye uliyekuwa mzungumzaji mkuu.

Nakumbuka ulianza hadi kuniunganisha na ndugu zako, (one of ur young sister) na ilitokea yeye kufurahia sana mawasiliano yetu.

One day uliniagizia kuja kwenu nakumbuka ulisema ni Boko magengeni ndiyo kituo na ulinipa maelekezo vizuri ila sijawahi kuja kwenu.
Kila nikija Dar nilitamani kufika ila mambo yakawa mengi sikufika. Kutokufika kwangu hakukutisha mawasiliano yetu, na hata neno la Mungu ulinipa sana.

Kosa langu lililonifanya nikuombe msamaha kwa sasa ni hili hapa.
Nakumbuka siku nikiwa Dar na nikakujulisha ulitaka sana sana tuonane, na mimi nilikubaliana na wewe kuwa this time we should see each other, kiukweli utaratibu tuliuweka tukutane Mwenge, ila mimi nilichelewa kufika na wakati niko njiani uliniambia unaenda Muhimbili kulikuwa na mgonjwa kwa hiyo hata nikfika Mwenge itabidi nikusubirie tu...
Sikuona tabu kwa upande wangu kwasababu nilikua nimeongozana na wenzangu wawili sikupata shida kukusubiana, tulisubiri pale huku tukifanya mambo mengine tu..
Ilichukua muda sana kuja nakumbuka uliniandikia meseji ukanielekeza nipande basi zinazoenda Posta nishukie Kituo kinachoitwa Pam beach tutakutana hapo.
Nadhani ulikuwa hujui kama sikua peke yangu.
Tulipanda daladala na tukashukia Pam beach kama ulivyoagiza bahati nzuri bado tulifika kabla yako,
Tulikaa ile sehemu ya abiria wanakokaa kusubiria daladala, uliniambia ulikuwa karibu sana and u will be there after few minutes....
Kweli ukaja nikakuona ulivyokuwa unaanza nipigia simu ili unibaini, kwa ustadi mkubwa kwenye ile simu nikafuta mlio, nilikuona vizuri mno Eliza wewe ni mrefu maji ya kunde na mwili wako umejajaa kidogo...

Nilikupungia ili ujue ndiyo sisi uje.
Ukaja kwa madoido yote kabisa ukaniuliza who is Derick here? Na mimi bila kuchelewa nikanyosha kidole kumwelekea yule jamaa niliyekuwa nae...(nilikuwa na wenzangu wawili mmoja Me na mwingine Ke).
Basi Eliza ulimkumbatia mshikaji kwa hisia kweli kweli, kitu kilichomshangaza kwani hata wao nilikuwa sijawaambia kuwa nakutana na mtu ambaye sijawahi kukutana nae kabisa.

Basi kuanzia hapo picha ikawa inaanza kuharibika kumbuka wewe na mimi tumewasiliana kwa muda mrefu kwa hiyo lazma kila utakachoniuliza nijibu...
 
Bo bo bo booooongeeeeee la mistakeeeeee!
 
Si uandike yote pembeni ndo upaste huku...
 
hahaha what's ur poit bro
 
nilikua sijajua Bangi ya Dodoma waliyoisifia ChembaSquad ni kali ivi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…