A
Anonymous
Guest
Tuliitwa Dodoma kuhudhuria semina elekezi, tukasafiri kwa gharama zetu na tukakaa Dodoma siku tatu kwa gharama zetu na hatukulipwa gharama hizo kama inavyotakiwa kwa mujibu wa kanuni za utumishi wa umma.
Tulipewa barua za kuelekea kwenye vituo vya Kazi, nilihamisha familia kutoka Karagwe kwenda Lindi kwa gharama zangu nikijua zitarejeshwa kwa mujibu wa kanununi za utumishi wa umma.
Hadi sasa hatujalipwa pesa hiyo ya kujikimu wala pesa ya semina elekezi na hakuna majibu ya kwanini hatujalipwa.Kibaya zaidi bado kuna watumishi wa 2024 nao wanadai pesa hiyo wamelipwa nusu nusu au roborobo yaani pesa inaharibiwa.
Taasisi nyingine zimeshalipa hadi watumishi walioajiriwa mwezi wa nne mwaka huu. Veta kuna shida kubwa kwenye suala la hela tunachezewa mno hata pesa za extra duty allowances hazilipwi kwa wakati na ipasavyo.