VETA na wizara husika msifanye maamuzi ya kukurupuka

VETA na wizara husika msifanye maamuzi ya kukurupuka

Kibwetelo

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2018
Posts
732
Reaction score
599
Habari za jioni wakuu,

Hii kitu inaudhi sanaaa, yaani wanafunzi wametengeneza project zao kwa gharama halafu mnakuja ghafla tu eti mwaka huu hakutakua na project . Hivi mlikuwa wapi muda woote huo mpaka wanafunzi wametumia gharama zao ndio mnakuja kusitisha hivyo

Hivi mnakurupukaga tu, Haya sasa wametumia muda mwingi kutengeneza project mngesema mapema muda ule wautumie kusoma haya mambo ya kukurupukaga mnafeli sana wizara ya elimu mno.
 
Sasa Mtoa maamuzi anakula ,anaishi atakavyo kwani kuna ishu
 
af mamb km hy unaweza usiyaelewe vzuri hadi yakukute, polen sn ndugu zetu
 
Habari za jioni wakuu,

Hii kitu inaudhi sanaaa, yaani wanafunzi wametengeneza project zao kwa gharama halafu mnakuja ghafla tu eti mwaka huu hakutakua na project . Hivi mlikuwa wapi muda woote huo mpaka wanafunzi wametumia gharama zao ndio mnakuja kusitisha hivyo

Hivi mnakurupukaga tu, Haya sasa wametumia muda mwingi kutengeneza project mngesema mapema muda ule wautumie kusoma haya mambo ya kukurupukaga mnafeli sana wizara ya elimu mno.
Mkuu, kwani project kwa wanafunzi/wanachuo si sehemu ya mafunzo? Mimi naona hakuna walichopoteza, bali wamejifunza kwa vitendo. Hii hutumiwa hata mashuleni na walimu wajanja wanaotaka wanafunzi wao wasome, huwaambia wanafunzi kuwa wiki ijayo kutakuwa na mtihanj. Wanafunzi wanasoma kwa bidii halafu siku ya mtihani mwalimu anawaambia mtihani umeaahirishwa mpaka itakapotangazwa tena! Sasa hapo utasema mwanafunzi amepoteza?
 
Mkuu, kwani project kwa wanafunzi/wanachuo si sehemu ya mafunzo? Mimi naona hakuna walichopoteza, bali wamejifunza kwa vitendo. Hii hutumiwa hata mashuleni na walimu wajanja wanaotaka wanafunzi wao wasome, huwaambia wanafunzi kuwa wiki ijayo kutakuwa na mtihanj. Wanafunzi wanasoma kwa bidii halafu siku ya mtihani mwalimu anawaambia mtihani umeaahirishwa mpaka itakapotangazwa tena! Sasa hapo utasema mwanafunzi amepo
Project zao hua zinaasesiwa na watu wanaosimamia mitihani baada ya kumaliza mtihani lakini mwaka huu wameambiwa kutakua na interview sijui isiyohusisha project hapo ndo tatizo kwamba hawajui wataulizwa nn
 
Back
Top Bottom