HOJA VETA waache kutumia wastaafu kutunga na kusahihisha mitihani

HOJA VETA waache kutumia wastaafu kutunga na kusahihisha mitihani

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
A

Anonymous

Guest
Kuna tabia ya VETA kipindi cha kutunga na kusahisha mitihani, wanawatumia wastaafu na watumishi wasiokuwa wa VETA. Mfano: mtihani wa mwezi wa sita wa Level III uliofanyika 2026: kuna kituo x (naomba kuhifadhi jina la kituo) kilisimamiwa na mwalimu wa sekondari na ilihali watumishi wa VETA wapo na wanahitaji hizi fursa kwa ajili ya kukua katika kada zao.

Pia kwenye kusimamia mimi nilikuwepo kwenye semina ya mwaka jana mwezi 11. Alikuwepo mzee mstaafu katika wasimamizi: swali kwa mamlaka. Je ni kuna nini kuilichojificha juu ya urasimu huu kwa mamlaka ya VETA?

Kituo kilichosimamiwa kilikuwa VETA DAKWA kinachopatikana Morogoro (jina la msimamizi kutoka sekondari mwl. Peter), Sera za VETA haziruhusu hivyo hii inaonyesha kuna wachache ambao wameamua kunufaika nyuma ya pazia kwa kuweka wasimamizi wasio kuwa watumishi husika wa mamlaka, na pia kuondoa umakini katika zoezi nyeti la kitaifa.
 
Unataka wasimamie wa VETA unaowajua wakupenyezee desa
Wewe kwanza utakuwa mlugaluga huwa mna mihemko na kukurupuka tu
Hakuna mtihani wa kufuzu utasimamiwa na mwalimu wako, acha utoto na komaa kusoma upasi kihalali
 
Unamjibu kitaalamu au unamfokea na kumtukana kwa kadiri ya ulivyojisikia tu?
 
Unataka wasimamie wa VETA unaowajua wakupenyezee desa
Wewe kwanza utakuwa mlugaluga huwa mna mihemko na kukurupuka tu
Hakuna mtihani wa kufuzu utasimamiwa na mwalimu wako, acha utoto na komaa kusoma upasi kihalali
Vyuo vikuu vyote duniani kote mitihani inasimamiwa na walimu wenyewe. Huenda kanuni za VETA haziruhusu anafundisha asimamie mitihani ya kuhitimu.
 
Back
Top Bottom