VETA: Waliopoteza au kuharibikiwa vyeti watapatiwa vyeti vipya badala ya Result Slip ila watalipia

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imepokea taarifa za malalamiko yaliyotolewa kupitia baadhi ya vyombo vya habari kuhusu suala la utoaji wa vyeti mbadala kwa wahitimu waliopoteza vyeti au vyeti vyao kuharibika.

Pia soma ~ VETA Makao Makuu wanatuambia tuliopoteza vyeti hatuwezi kupata mbadala, wanasubiri mabadiliko ya sheria. Hii ni sawa kweli?

VETA imekuwa ikipokea maombi mengi ya vyeti mbadala kutoka kwa wahitimu wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi. Katika kipindi cha mwaka 2025/2026, jumla ya maombi 33 ya vyeti mbadala yalikuwa yamepokelewa.

Kutokana na unyeti wa suala la utoaji wa vyeti vya kitaaluma/ujuzi, VETA imekuwa ikichukua tahadhari kubwa ili kuhakikisha kuwa hakuna mianya ya udanganyifu au matumizi mabaya ya vyeti.

Kwa sababu hiyo, awali wahitimu waliokuwa wamepoteza vyeti vyao walikuwa wakipatiwa waraka maalum unaoambatana na hati ya matokeo (Result Slip) ili kuthibitisha sifa zao za kitaaluma/ujuzi.

Hata hivyo, baada ya VETA kupata taarifa kuwa waraka huo ulikuwa haukubaliki katika baadhi ya taasisi na mamlaka zinazohitaji uthibitisho wa sifa za wahitimu, Mamlaka imeboresha utaratibu wake na sasa imeweka utaratibu wa kutoa vyeti mbadala kwa wahitimu waliopoteza vyeti vyao.

Utaratibu huu umeandaliwa kwa kuzingatia viwango vya usalama na uthibitishaji ili kuendelea kulinda uhalali wa vyeti vya VETA na kuzuia uwezekano wa udanganyifu.

Kwa hiyo, wahitimu wote waliopoteza vyeti au walioharibikiwa na vyeti vyao na wanaohitaji kupatiwa vyeti mbadala wanaombwa kuwasilisha barua rasmi ya kuomba cheti mbadala, ikiwa na maelezo ya kupotea/kuharibika kwa cheti kinachoombwa na kuambatisha nyaraka zifuatazo:

Barua ya uthibitisho wa kuhitimu mafunzo ya ufundi stadi kutoka chuo chenye ithibati alichohitimu mafunzo

Nakala ya tangazo la upotevu wa cheti lililochapishwa kwenye Gazeti la Serikali.

Cheti halisi kilichoharibika (kwa wale ambao vyeti vyao vimeharibika)

Taarifa ya upotevu wa cheti kutoka Jeshi la Polisi (Loss Report).

Nakala ya kitambulisho halali, ambacho kinaweza kuwa Kitambulisho cha Taifa (NIDA), Kitambulisho cha Mpiga Kura, Leseni ya Udereva au barua ya utambulisho kutoka kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji/Mtaa yenye taarifa kamili za mawasiliano ya ofisi husika.

Malipo kwa ajili ya uchakataji wa cheti mbadala, yatafanyika kupitia Namba ya Malipo (Control Number) ambayo mhitimu atapewa baada ya maombi yake kukaguliwa na kuthibitishwa. Ugharamiaji wa malipo utakuwa kama ifuatavyo:

Upotevu wa cheti cha Ufundi Stadi kwa mara ya kwanza: TSh 100,000.
Upotevu wa cheti cha Ufundi Stadi kwa mara ya pili: TSh 150,000.
Upotevu wa cheti cha Ufundi Stadi kwa mara ya tatu: TSh 200,000.
Maombi ya vyeti mbadala (yakiwa pamoja na viambatisho vyake) viwasilishwe kwa:

Mkurugenzi Mkuu,
Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi
VETA Makao Makuu,
12 VETA Road.
41104 Tambukareli,
P.O. BOX 802, DODOMA
Barua pepe: [email protected] au [email protected]

Baada ya kupokea maombi yaliyokamilika na kuthibitisha uhalali wa nyaraka zote zilizowasilishwa, VETA itatoa cheti mbadala ndani ya siku 14.

VETA inawashukuru wahitimu wote kwa uvumilivu wao wakati wa kuboresha utaratibu huu muhimu. Mamlaka itaendelea kuboresha huduma zake ili kuhakikisha wahitimu wanapata huduma bora, kwa wakati na kwa kuzingatia misingi ya uwazi, uwajibikaji na usalama wa nyaraka za kitaaluma.

Imetolewa na:
Sitta Peter
Meneja Uhusiano kwa Umma na Masoko
Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA)
 
Wazo zuri
 
Back
Top Bottom