A
Anonymous
Guest
Mimi ni mmoja wa wanafunzi wa Shahada ya Udaktari wa Mifugo ambao tunatarajia kufanya internship ya mwaka mmoja kabla ya kupata usajili wa kufanya kazi kama madaktari wa mifugo.
Leo tumekutana na Naibu Msajili wa Baraza la Madaktari wa Mifugo Tanzania (VCT) ambaye alitueleza utaratibu wa usajili wa internship. Katika maelezo yake, alisema kuwa tangu mwaka 2021 kati ya wahitimu 356, ni wahitimu 106 pekee waliojiandikisha na kufanya internship.
Takwimu hizi zinaonyesha kuwa kuna changamoto kubwa katika mfumo. Swali ni kwa nini wahitimu wengi hawafikii hatua hii muhimu?
Changamoto kubwa ni ukosefu wa ufadhili. Internship ni programu ya muda wote (full-time programme), lakini veterinary interns wengi hawapati mshahara wala posho ya kujikimu. Mhitimu anatakiwa kugharamia chakula, malazi na usafiri kwa mwaka mzima bila kipato.
Tulielezwa kuwa VCT ni msimamizi wa sheria na haina mamlaka ya kuamua suala la malipo, na pia interns hawapati posho kwa sababu si "watoa huduma". Lakini internship yenyewe iliwekwa ili kuwajengea wahitimu uwezo katika diagnosis, disease surveillance, management na maeneo mengine muhimu ya taaluma.
Kwa mujibu wa National Internship Guidelines, kuna mifumo mbalimbali ya ufadhili wa internship kupitia Serikali, mwajiri au mfumo wa cost sharing. Tunahitaji kufahamu: Veterinary internship ipo kwenye mfumo upi wa ufadhili?
Hatudai mshahara mkubwa. Tunaomba kuwe na utaratibu wa kuwasaidia interns angalau kwa posho ya kujikimu. Hata kama kituo hakiwezi kutoa malipo makubwa, msaada mdogo unaweza kusaidia intern anayefanya kazi muda mrefu katika kituo.
Pia tuliambiwa kuna uwezekano wa kupata msaada wa TSh 150,000 kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu kwa ajili ya nauli ya kwenda kituo cha internship. Tunathamini hatua hiyo, lakini bado kuna changamoto ya uwazi kuhusu utekelezaji wake, kwani wahitimu wengi hawajui kama msaada huo umewahi kutolewa, umetolewa kwa nani na utaratibu wa kuupata ukoje. Zaidi ya hapo, kiasi hicho hakiwezi kutatua gharama za maisha ya mwaka mzima.
Tunapoangalia nchi jirani kama Kenya ambako veterinary interns hulipwa, na baadhi ya kada nyingine Tanzania zinazopata posho wakati wa internship, tunajiuliza kwa nini veterinary interns wameachwa nyuma wakati taaluma hii ina mchango mkubwa katika afya ya jamii, usalama wa chakula na uchumi wa taifa.
Hili si suala la sisi pekee. Tunaliibua kwa ajili ya vizazi vijavyo vya wanafunzi wa Veterinary Medicine. Internship ni muhimu kwa kujenga madaktari wenye uwezo, lakini isiwe kikwazo kinachowafanya wahitimu washindwe kupata usajili kwa sababu ya ukosefu wa uwezo wa kifedha.
Tunaiomba Serikali, Wizara husika na VCT kutafuta mfumo endelevu wa kuhakikisha kila mhitimu mwenye sifa anapata nafasi ya kufanya internship bila uwezo wa kifedha kuwa kikwazo.