Viashiria vya msingi vya kuzingatia kabla ya kununua hisa za kampuni husika

Joined
Aug 26, 2022
Posts
64
Reaction score
124
Moja ya swali muhimu la kujiuliza ni: “Nawezaje kuchagua kampuni bora ya kuwekeza?”

Leo tuzungumzie qualitative fundamental factors ambazo ni muhimu sana kwa wawekezaji wa muda mrefu wanaotaka kupata ongezeko la thamani na pia magawio.

  • Elewa Biashara ya Kampuni
Wekeza tu pale unapofahamu kampuni inafanya nini na inatengeneza fedha vipi.
Mfano: Ukinunua hisa za CRDB inabidi uelewe kuwa CRDB ni benki na bishara yake kubwa ni kutoa mikopo - hivyo basi hata ukipata taarifa yake ya kifedha ni muhimu kuzingatia ubora wa mikopo.

  • Chagua Viongozi wa Sekta husika (Market Leaders)
Nunua hisa za kampuni zilizo miongoni mwa Top 3 katika sekta zao.
Mfano: Benki kubwa kama CRDB na NMB peke yao zinashikilia karibu 50% ya mikopo yote nchini, jambo linalowapa nafasi ya kuongoza sokoni.

  • Angalia Aina ya Ushindani:
Kampuni yenye ushindani mdogo, au hata yenye monopoly (kutawala soko), huwa salama zaidi na faida zao hutabirika.

  • Rekodi ya Kifedha Thabiti
Chagua kampuni ambazo kwa angalau miaka 3 mfululizo zimeonyesha ukuaji chanya kwenye: Faida, Mali na Uwekezaji.

  • Uwiano wa Mali na Madeni:
Kampuni yenye mali nyingi kuliko madeni ina uthabiti na uwezo mzuri wa kustahimili misukosuko ya uchumi.

  • Viongozi Bora
Uongozi bora ni moyo wa kampuni. Hakikisha kampuni ina viongozi wenye rekodi nzuri ya kusimamia biashara kwa ufanisi.

  • Gharama za Riba (Finance Costs):
Angalia kiwango cha riba kinacholipwa. Ni vyema kisizidi 50% ya faida kabla ya riba na kodi (EBIT).

  • Gharama za Uendeshaji Ndogo:
Kampuni yenye ufanisi na gharama ndogo za uendeshaji inabaki na faida kubwa zaidi kwa wawekezaji.

  • Road Toll Business:
Hizi ni kampuni zinazopata mapato kila mara bila kujali wateja wanataka au hawataki.
Mfano: DSE – kila unapouza au kununua hisa, au kila bondi inauzwa, wao hupata sehemu ya mapato. Ni biashara yenye uhakika wa kipato.

Kwa kifupi, usiwekeze kwa bahati nasibu. Chagua kampuni ambazo unaelewa vizuri, zina nafasi kubwa sokoni, rekodi nzuri kifedha, viongozi imara na mtindo wa biashara unaohakikisha mapato ya muda mrefu.
 
Kwa sasa utamshauri mtu awekeze kwenye hisa za kampuni zipi? We see CRDB current price imedrop from 1600 to 1140, in market for traders ukiangalia graph yake unaweza sema ipo in correction phase, is it a good time to buy ? With the principle of buy low and sell high? Naomba view yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…