Southern Giant
JF-Expert Member
- Sep 1, 2018
- 933
- 1,912
Zahanati ya Tambukareli iliyopo kata ya Azimio wilaya ya Temeke DSM, ambayo ni tegemeo kwa wananchi wa kata ya Azimio na maeneo jirani imeanza kugubikwa na viashiria vya rushwa, hali inayotia doa huduma za afya na kuathiri maisha ya wagonjwa na wateja kwa ujumla.
Malalamiko kutoka kwa wananchi wanao hudumiwa hapo yanaonesha kuwepo kwa viashiria mbalimbali vya vitendo vya rushwa vinavyodhoofisha imani kwa zahanati ya tambukareli.
Hii ni baada ya wafanya biashara walio enda kupima afya kwa nyakati tofauti tofauti kama sheria zinavyoelekeza lakini cha ajabu bwana afya wa kata ya azimio halmashauri ya manispaa ya temeke, mkoa wa dar es salaam kwa kushirikiana na mtumishi wa zahanati ya tambukareli aliyejitambulisha kama daktari waliwapima wafanyabiashara hao na kuchukua pesa zao bila ya kuwapa control namba ya malipo ya serikali au stakabadhi halali ya malipo hayo.
Pesa hizo zimekusanywa katika shule ya Msingi Azimio, shule ya sekondari Kichanga, Shule ya msingi Mwangaza, Shule ya msingi Sokoine na Shule ya msingi Twiga, wafanya biashara walitozwa viwango tofauti tofauti ikiwa ni Tsh 15,000 na wengine Tsh 20,000 walipo hoji kuhusu risiti hakukuwa na majibu yanayoeleweka.
Baadhi ya Viashiria Vilivjiookeza;-
1. Malipo Yasiyo Rasmi: Baadhi ya wateja hasa mama lishe na baba lishe kutozwa gharama zisizo na risiti, kinyume cha taratibu rasmi za malipo ya hospitali (serikali).
Athari wa hili jambo ni pamoja na;-
1. Kukosekana kwa mapato serikalini: Fedha zinaingia katika mifuko ya watu wachache wala dili badala ya kuingia serikalini ili zisaidie maendeleo ya afya kwa jamii zetu.
2. Kudorora kwa Imani ya Jamii: Wananchi wanapoteza imani na hospitali, hali inayoweza kusababisha ongezeko la chuki kwa serikali kutokana na watu kutozwa gharama tofauti tofautii Tsh 15,000 na wengine Tsh. 20,000 bila ya kupewa risiti .
3. Uharibifu wa Taasisi: Hospitali inachukuliwa kama eneo la biashara binafsi badala ya taasisi ya huduma kwa umma.
Wito wetu kama wana jamii: Jamii tunaomba uongozi wa Wizara ya Afya, vyombo vya dola, na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) kuchunguza kwa kina tuhuma hizi na kuchukua hatua kali dhidi ya wahusika. Hii itasaidia kurejesha imani ya wananchi na kulinda haki ya kila mmoja kupata huduma bora za afya.