[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Uwe unasema ni copy vya mchina maana mwenzako anakushangaa hiyo bei yako na bai anayoijua
Sent using
Jamii Forums mobile app
Bora umesema wewe. Mimi nilitaka kusema lakini siku hizi naamua ubishi gani nianzishe na ubishi gani nimezee.
Ubishi mwingine unaweza kushusha viwango, heavyweight aingie ulingoni na featherweight inaweza kuwa mashitaka baadaye buree.
Isije kuonekana habari za "Huu ubishi wa Kiranga tu, anataka kubisha kila kitu. Hata ukimwambia yeye ni Kiranga atakuuliza "Kiranga ni nini, na utajuaje huyu Kiranga na huyu kiranga na huyu si Kiranga na huyu si kiranga?"".
Mie mtoto wa Mchafukoge mjini nimecheza draft na Carl Lewis Salamander, pedigree ya Azania Front since linajengwa 1903, mji umenifuata sijaufuata mji. Nimemezea mengi. Pengine mwenzetu anatengeneza mingo zake, nikasema nisimuharibie biashara.
Nikajua labda kapata contena la dili. Kwa kweli mengine sijali.
Katika mfumo wa dog eat dog, na "Makufuli" haya yalivyofungwa kwenye hela, mtu akipata kontena la dili mimi ni nani nimsilibie?
Back to basics.
Clarks kwa bei hiyo umesafirishaje? Kodi umelipaje?
Ninavyo hapa kibao, Clarks, Florsheim Cole Haan, Nike, Adidas etc, vingine hata kuvivaa sijavivaa, vingine vimebahatika kuvaliwa mara moja, nataka kuvitia kwenye pipa kubwa, kisha meli niwapelekee watu TZ wavae, maana hapa kwangu vitaoata vumbi tu bila kuvaliwa. Granted mimi mteja wao mzuri Clarks, mpaka vingine wananipa bure kwa promotion, lakini, kwa bei hii nilitaka kusema kumbe ninaotaka kuwapeleke bora wanunue huko huko.
Mbona bei nzuri sana?
Ila nikapata maswali mengi ya quality.
Dar kuna duka langu moja la Clarks lipo hapa karibu na CBE, nafikiri mtaa wa Zanaki pale, kuna wahindi fulani nilikuwa nanunua sana Clarks boots kwao, walikuwa wananipa sana deals lakini hawakufikia bei hizi, labda miaka mingi imepita, maana hapo zaidi ya miaka 20 imepita.
Lakini all in all, Clarks at 50,000 lazima muuzaji atakuwa kafanya utaalamu fulani hivi.
Kama ni genuine basi hajalipia kodi au kontena la deal, au la, ndiyo mambo ya "Mchina".
Sent using
Jamii Forums mobile app