Viazi vitamu vya kuchemsha na nazi

Viazi vitamu vya kuchemsha na nazi

willzkichaa

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2013
Posts
422
Reaction score
190
Habari wapendwa!
Hapa naomba ku sharevaina nyingine ya chakula cha ki- bachelor na cha fasta kidogo.

Naamini sio muda wote unakua na mood ya kupika ila unakuta una nenge/gwanda/njaa na ukahitaji msosi wa fasta na pia ukizingatia vitambi na presha tunaziepuka. Leo nawaletea pishi la haraka na lililojaa virutubisho vya kutosha. Tuanze kazi...

Mahitaji ni viazi vitamu,
1397070727571.jpg

Karoti, chumvi na sukari

1397070766601.jpg

Maandalizi;
Menya viazi na uvikate katika ukubwa utakaoupendelea. Na kisha tia kwenye maji na uoshe kwani vikipigwa na upepo au ubaridi huwa vinaunda kama utando mweusi.

1397071004505.jpg

Kata karoti katika maumbo madogo (usiisage)

1397071161412.jpg

Chemsha viazi na tia chumvi (weka maji mengi kiasi) kisha funika viive

1397071241097.jpg

Na vikianza kuiva. Mwaga maji na uweke masafi (hapa weka kiasi na ikibidi yasipite kimo cha wingi wa viazi) maji yakianza pungua weka nazi na usifunike kwani tui litakatika. Pitisha mwiko kuchanganya nazi kote. Kisha acha kiendelee kuiva.

1397071545649.jpg

baada ya dakika kumi weka sukari (kama utapendelea) na karoti ulizoziandaa.

1397071815057.jpg

Hapo acha maji yapungue na yatajitengeneza mchuzi/supu yenyewe. Ila ukiona supu nyepesi waweza ponda viazi vilaini vilivyomo ndani kuongeza uzito wake.

1397071919125.jpg

Hapo acha kiive na baada ya dakika 15 waweza kuepua na ku serve.

1397072253830.jpg

P.S. Hicho ni chakula cha watu watatu na kinalika hadi asubuhi. Viungo na mahitaji
weka upendavyo. Karibuni.
 
Huyu samaki nimemmis sana

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums

Karibu Mwanza. Kachumbari ya matango ingenichelewesha. Naanza kua addicted na hiki chakula. Ntaanza weka iliki kwa mbali kuongeza ladha na harufu tofauti.
 
Hahahahhahaah sawa itabidi ukodi mvuvi maana nala sana samaki....

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums

Hahahahah Ntakupa mawasiliano yao. ukapande hadi mitumbwi na oven.
 
Hakuna mbadala wa nazi

Mh. Kiukweli sidhani kama kuna mbadala. Kama hutaki kuweka nazi basi osha tu viazi halafu chemsha.

Wanaume tumerahisishiwa kazi hapo ukiwa na pakti yako moja ya nazi mambo yanaenda. Kwa matokeo mazuri ni bora uweke nazi
 
Mkwe subiria mwanangu akupikie usimalize maneno utakula hadi utafune vidole kwa utamu....

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums

Hehehe nasubiri vya mke wangu labda nitavipenda,viazi vitamu sivipendi kwa sababu ukila ni kama havikai vizuri tumboni,yaani kama imeganda tumboni vile
 
Back
Top Bottom