Mr pianoman
JF-Expert Member
- May 22, 2019
- 2,595
- 6,264
Wakuu naongea kwa ushahidi kabisa kilipo kituo kikuu cha Polisi Arusha kuna kamsitu pembeni na ndani ya hako kamsitu kuna njia za waenda kwa miguu wanapita basi imegeuka fursa kwa vibaka na mateja kuwatapeli waenda kwa miguu wakijifanya ni polisi.
Hao vibaka na mateja wanatapeli watu kwa njia tofauti tofauti kuna wengine wanaambiwa wamepita sehemu ambayo polisi wamezuia watu kupita hivyo unatakiwa uchague moja utoe hela au wakupeleke kituoni. Hapa wengi wamepigwa ukizingatia ni kweli kituo unakiona kile pale.
Njia nyingine wanakuvizia ukojae wanakuja wakijifanya wamepewa jukumu la kuzuia watu wasikojoe. Sio mbaya kulinda mazingira yasichafuliwe lakini je ni kwanini itumike njia danganyifu ya kutapeli watu kwa kujifanya wewe ni polisi? Na wala mamlaka husika haiwatambui hao watu.
Njia nyingine ukikaa wanakucheki wewe ni mtu wa aina gani wanakuja kukutapeli.
Hii ni aibu mtu kutapeliwa mchana kweupe karibu kabisa na kituo kikuu cha polisi na huo mchezo watu wote wanaofanya biashara pale karibu wakiwemo na bodaboda wanajua je ni kweli polisi hawajui?
Kama ni kweli Polisi wote waliopo pale kituo kikuu cha Polisi Central Arusha hawajui hili suala ni hatari kwa kweli maana mateja na vibaka wapo sebuleni.
Kuna majeshi yanamaeneo makubwa yenye misitu na vichaka ila huwezi kukuta vitu kama hivi vikitendeka kwenye maeneo yao.
Polisi Arusha hao watu wapotezwe hapo wanachafua taswira ya jeshi la polisi kwa kujifanya na wao ni polisi.