Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Umeanza fujo!😜Naona tv nyingine inajisogeza yenyewe
Polee Cc ephen_Vibaka wameniibia smart TV size ya 48" mpya kabisa ambayo niliinunua juzi tu![]()
![]()
Waliingia ndani kwa kuvunja dirisha usiku wa manane, wala sikusikia chochote walipokuja ila nilipoamka asubuhi nilikuta TV haipo sebuleni na vyuma vya dirisha vikiwa vimekunjwa hadi kuwezesha mwizi kuingia na kutoka kwa kupitia hapo dirishani.
Ninapanga kwenda kwa mganga wa kienyeji ili kurejesha smart TV yangu.
Naomba kama kuna mganga wa kienyeji hapa jf mwenye uwezo wa kupiga ramli hadi vibaka walioiba TV yangu wapatikane, ajitokeze hapa nimpe kazi mara moja.