Flamegood
Senior Member
- Oct 27, 2018
- 129
- 293
Habari wana JF,
Mimi ni mzaliwa wa Arusha tena mjini(manispaa) Ungalimited, nimekuwa pale nakamaliza elimu yangu yote hadi advance mwaka 2017
Nimeshuhudia vibaka wengi wakiwaliza watu mali zao[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] yaani sio poa, majamaa wanahitaji certficate of crime' maana wana ujuzi sana katika sanaa hiyo.
Sasa bwana, kuna siku nilijipitisha mitaa ya Matejoo, me kipindi hicho nilikuwa sipoi maana nilikuwa bonge la bishoo tena ukizingatia sina majukumu yoyote zaid ya kusoma. Hivyo pesa zangu zote za pocket money nilizopewa na wazazi ziliishia kwenye LOOKING (Mavazi na Urembo)
Nakumbuka Matejoo nilikuwa naenda kuwatembelea wanangu niliosoma nao basi nikawa nadunda dunda kama tenesi na mwendo wa maringo ukicheki shingo kafa Mjusi (vyeni vya kutosha).
Basi nikawakuwa majamaa wamejibanza chocho flani hivi wanapata vitu vyao(mimoshi tu) nilisita kidogo nikataka nibadili njia kwa kuwa nilijua tuu kwa jinsi nilivyokuwa lazima wangenitamani 'Na vile majamaa hawapendi masharobaro mh', ile nataka kubadilisha njia nikaaikia "OYAAA VIPLO BABUU NJOO KWA HUKUUUU" niliposikia hivyo nikajua mh' tayari. Ila mawazo yakanijia kwamba nisiende bali nikimbie kwa sababu iwe isiwe hawa jamaa nikienda waliponiita hakika wataniacha uchi.
Bwana bwana, kukimbia ndipo tatizo lilipoanzia maana majamaa waliunga na mimi, ilibidi nielekee upande wenye watu wengi(sokoni) labda pengine majamaa wataloose mind lakini wapi! Tena nilipofika pale sokoni ndipo waliponivaa tena wakiongea mambo siyaelewe.
Wahuni;"TWENDE NYUMBANI UKANYWE DAWA TWENDEEEEE
Mimi: [emoji15][emoji15][emoji15]DAWA?
Wahuni: EEEEEH RASHID TWENDE UKANYWE DAWAAA (majamaa walikuwa wakiongea kwa sauti na vurugu wakinivuta kunibeba ili waondoke na mimi huku watu wakishangaa na kushindwa kuelewa nini kinachoendelea pale.
Watu: NI NINI JAMANIII? HE! NI MWIZI AU JAMANI MTAMUUMIZA (ni sauti za watu walikuwa wakiulizana wakati mimi nikijaribu kujitetea kutoka mikononi mwa jamaa) ndipo mmama mmoja mwenye hekima alipojitosa pale kisha akajaribukuwauzuia wale jamaa kwa kuwauliza nini tatizo.
Wahuni:amna tatizo mamalai ila huyu ni mdogo wetu huwa ana tatizo la kiakili ndo tunamuondoa huku sokoni asije akaleta vurugu ili tumpeleke nyumbani akameze dawa zake za kutuliza kichaa.
Mama: Ahaaaa, kumbeee(mimi niliposikia mama ameridhika na majibu yale ndipo nilipoamua kujaribu kujitetea tena kwa nguvu zote "AAAAAAAH HAWA JAMAA NI WAONGO MAMA WANATAKA WANIIBIE TUU"
Wahuni: Si unaona mamalai huyu kijana akili zake zishaanza kumuovertake sasa sisi tumuibie nini mdogo wetu
mama;hahaha basi muwaisheni.
Dah! Nakumbuka baada ya yule mama kutoa lile jibu ndipo majamaa walinibeba kwa nguvu zote kuelekea maskani yao, mimi nilijua tuu kinachoenda kunitokea ila majamaa walinibana kiasi cha kukata tamaa. Dah! Nakumbuka hii siku niliondoka na ngeu ya uso tena nikiwa na boxa.
Lengo la huu uzi ni kutaka kufahamu ni nani mwingine alishawahi kubananishwa na vibaka A-TOWN?
Naitwa LASCOO, FLAMEGOOD
Sent using Jamii Forums mobile app