Vibaka wamerudi mtaani kwa wingi

Vibaka wamerudi mtaani kwa wingi

Bururu

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2016
Posts
877
Reaction score
584
Naomba Jeshi la Polisi hasa mitaani mje kusaidia maana vibaka wamerudi kwa wingi sana. Hii sio siasa ni reality kabisa na siandiki kwa mihemuko!

Kuna kipindi tulianza kulala milango wazi lakini kwa sasa wanakata mpaka madirisha
 
Vibaka hawajawi kuisha hata kipindi cha mwendazake, ila sasa hivi vyombo vya habari viko huru kutangaza huo uhuni. Ulifumbwa macho na propaganda mfu ndio maana unaleta huu uzi kwa rejea za utawala wa mabavu.
 
Juzi huku Manzese panya road wameibuka upya kule Tanga kuna watoto wa Iblisi , huku Sirro anashughulika kwa kutumia rasilimali nyingi kwa bastola moja yenye risasi tatu za kumbambikizia jeshi mstaafu
Aaah Dunia msongamano ----Ndala Kasheba RIP
 
Wezi hawajawahi kupungua au kuisha ishu ni uzembe wa vyombo vyetu vya usalama kuanzia serikali za mitaa Hadi kwa IGP, maelekezo ya Rais yapo wazi kabisa na sio kazi ya Rais kuja kukamata vibaka ishu ni kureport wizi kwa wingi imfikie mwenyewe ili awaambie watu wake au awabadilishe.
 
hivi huyu Sirro ameshastaafu? Mbona hasikiki au ndio madhara ya chanjo? Na wale wa barabarani ndio kabisaaaa wanachukua za kupiga kiwi mpaka wanakera, ila tutafika tu.

Mama naye yuko kwenye ndege tena anaenda Misri, akirudi sijui Dubai ilimradi tu, yetu macho bana. Mbuzi wa bwana heri.....
 
Hao polisi wana mtandao nao hao vibaka, ushuhuda ulisikika ukisema, "...wakitukamata tunawamegea wanatuachia..."
 
Back
Top Bottom